CAG Kichere: Licha ya kupewa Ruzuku ya Tsh. Bilioni 31.55, ATCL imepata hasara ya Tsh. Bilioni 56.64, ongezeko la 61% kutoka hasara ya Mwaka 2021/22

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
3,739
13,502
Fuatilia yanayojiri wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akipokea Ripoti ya CAG na TAKUKURU kwa mwaka 2022/23, Ikulu ya Chamwino, Dodoma, leo Machi 28, 2024.

View: https://www.youtube.com/watch?v=6yQwHaO3rEA

MKURUGENZI MKUU WA TAASISI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA TAKUKURU CP SALUM RASHID HAMDUNI

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU), CP Salum Rashid Hamduni anawasilisha Taarifa ya Utendaji kazi wa TAKUKURU kwa Mwaka 2022/2023, Ikulu Mkoani Dodoma, leo Machi 28, 2024.

Amesema walifanya tathmini ya Miradi 1,800, walibaini Miradi 171 yenye thamani ya Tsh. Bilioni 143.3 ilibainika kuwa na utekelezaji hafifu na hivyo kuanzisha uchunguzi.

Akizungumzia tatizo la Ujenzi wa Vituo vya Mafuta katikati ya Makazi ya Watu linaongezeka, CP Salum Rashid Hamduni, amesema walifanya Uchambuzi kuhusu Mfumo wa Uzingatiaji wa taratibu za Ujenzi wa Vituo vya Mafuta katika Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani ambapo Vituo 38 vilihusika.

Asilimia 79 ya Vituo vilivyochambuliwa vilizingatia Sheria kwa kuwa na Vibali vya Ujenzi kutoka Halmashauri ambapo Ujenzi umefanyika, Asilimia 21 ya Vituo havikuwa na leseni wakati zoezi la Ufuatiliaji linafanyika.

Pia, walibaini Ongezeko la maombi ya Ubadilishwaji wa Matumizi ya Ardhi kutoka Matumizi ya awali na kuwa Matumizi ya Vituo vya Mafuta, pamoja na tatizo la Ujenzi wa Vituo vya Mafuta katikati ya Makazi ya Watu linaongezeka na kuleta Changamoto ya Usalama wa Watu waishio karibu.

MDHIBITI NA MKAGUZI MKUUU WA HESABU ZA SERIKALI, CHARLES KICHERE
Ukaguzi umebaini MSD ilitoa zabuni ya ununuzi wa vifaa vya maabara ambavyo ni vipimo vya COVID 19 kwa kampuni ambayo haikuwa mtengenezaji wa vifaa hivyo kinyume na makatwa ya zabuni, pia ilinunua vifaa hivyo bila kufuata ushauri, baada ya kufika kwa vifaa hivyo wataalamu walibaini havifai kwa matumizi yetu na tayari MSD ilikuwa imelipa fedha zote.

Mashirika ya Umma yanayojiendesha kibiashara yamepata hasara. Mwaka 2022/23, ATCL imepata hasara ya Tsh. Bilioni 56.64, sawa na ongezeko la 61% kutoka hasara ya Mwaka 2021/22 iliyokuwa Tsh. Bilioni 35.24. Ikumbukwe kuwa Shirika hili lilipokea ruzuku ya Tsh. Bilioni 31.55 kutoka Serikalini.

Shirika la reli limepata hasara ya Tsh. Bilioni 100.70 licha ya kupewa ruzuku ya Tsh. Bilioni 32.81 kutoka Serikalini.

TANOIL imepata hasara ya Tsh. Bilioni 76.56, ongezeko la Bilioni 68.72 kutoka hasara ya mwaka 2021/22.

Shirika la Posta limepata hasara ya Tsh. Bilioni 1.34.

NHIF umeendelea kupata hasa kwa mwaka wa 5 mfululizo ambapo mwaka 2022/23 umepata hasara ya Tsh. Bilioni 156.77. Hata hivyo, NHIF imeikopesha Serikali Bilioni 208 ambazo hazijalipwa hadi sasa.

CAG2.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka 2022/23 kutoka kwa Charles Kichere Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 28 Machi, 2024.​

Takukuru .jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea Taarifa ya Utendaji Kazi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kwa Mwaka 2022/2023 kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo CP. Salum Hamduni Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 28 Machi, 2024.
- Ripoti 21 za CAG zatua Bungeni kwa ajili ya kuanza kujadiliwa

- Ripoti kuu ya Mwaka ya Ukaguzi wa Ufanisi Mwaka wa Fedha 2022/23

- Ripoti Kuu ya Mwaka ya Ukaguzi wa Serikali za Mitaa kwa Mwaka wa Fedha 2022/23

- Ripoti kuu Mwaka ya Ukaguzi wa Serikali Kuu kwa Mwaka wa Fedha 2022/23

- Ripoti kuu ya Mwaka ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo ya Mwaka wa Fedha 2022/23

- Ripoti kuu ya Mwaka ya Ukaguzi wa Mifumo ya TEHAMA ya mwaka wa Fedha 2022/23

- Ripoti ya mwaka ya Mdhibiti na Mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali kuhusu ukaguzi wa Mashirika ya Umma kwa mwaka wa Fedha 2022/23
 
Attachments

  • Ripoti_Kuu_ya_Ukaguzi_wa_Mashirika_ya_Umma_Kwa_Mwaka_wa_Fedha_2022.pdf
    12.6 MB · Views: 5
  • Ripoti_Kuu_ya_Ukaguzi_wa_Serikali_za_Mitaa_kwa_Mwaka_wa_Fedha_2022.pdf
    16.4 MB · Views: 2
  • Ripoti_Kuu_ya_Ukaguzi_wa_Mifumo_ya_TEHAMA_kwa_Mwaka_wa_Fedha_2022.pdf
    12.5 MB · Views: 1
  • Ripoti_Kuu_ya_Ukaguzi_wa_Miradi_ya_Maendeleo_kwa_Mwaka_wa_Fedha.pdf
    4 MB · Views: 6
  • Ripoti_Kuu_ya_Ukaguzi_wa_Serikali_Kuu_kwa_Mwaka_wa_Fedha_2022_23.pdf
    4.5 MB · Views: 2
  • Ripoti_Kuu_ya_Ukaguzi_wa_Ufanisi_kwa_Mwaka_wa_Fedha_2022-23.pdf
    6.1 MB · Views: 2
Sasa matokeo ya uwasilishwaji huo niyapi? Naona kama vile wanakamilishatu utaratibu lakini wizi upo palepale kila mwaka.
Bora huyu anapokea ripoti na tunajuwa ubovu na ufisadi wote. Kuliko DIKTETA Magufuli yeye aliposomewa ripoti ya upotevu wa Tsh 1.5 Trillion akamfukuza kazi CAG Prof Assad.

Bahati mbaya Bunge ndilo lenye kuchukua hatua. Ila Bunge lenye UTAAHIRA aliloliacha Magufuli unategemea lifanye nini? Bunge lina wabunge 99.999% wa CCM.

Simtetei Samia kwa kutochukua hatua kwenye ropoti ya mwaka 2021/22 kama tulivyotarajia. Nchi hii inaendeshwa kwa Katiba na utawala wa Sheria. Rais hawezi kusomewa ripoti leo halafu kesho aseme kamata fulani na fulani peleka Mahakamani. Tutakuwa tuarudia UHAYAWANI uleule wa Magufuli aliyejaza watuhumiwa magereza lakini hakuna hata kesi moja aliweza kuimaliza hadi anakufa.

Upo utaratibu nankuna vyombo vya kufanya hayo mambo. Na mwenye majukumu makubwa ni Bunge.

Katiba inaruhusu Wabunge kupiga kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu kama maagizo ya CAG hayatekelezwi. Kura zikipigwa na wakashinda wanaosema hawana imani basi Rais anavunja cabinet.
 
Fuatilia yanayojiri wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akipokea Ripoti ya CAG na TAKUKURU kwa mwaka 2022/23, Ikulu ya Chamwino, Dodoma, leo Machi 28, 2024.

View attachment 2946606

Shida ya hizi REPORT znakuwaga kama ni TAARIFA za habari.

Hazinaga ACTION au special audit kwa maeneo ambayo yameonekana yanaupotevu wa mali na upigaji.

Itatolewa kama habari kisha itajadiliwa kwenye mitandao na itashia hivyo.

Hakuna action kwa wabadhirifu.

Hence, kwangu mm report ya CAG , ni story book kisichokuwa na tija. Ni upotezaji wa muda na fedha maaana gharama kubwa inatumika kuandaa report ambazo hazina tija wala action
 
Bora huyu anapokea ripoti na tunajuwa ubovu na ufisadi wote. Kuliko DIKTETA Magufuli yeye aliposomewa ripoti ya upotevu wa Tsh 1.5 Trillion akamfukuza kazi CAG Prof Assad.

Bahati mbaya Bunge ndilo lenye kuchukua hatua. Ila Bunge lenye UTAAHIRA aliloliacha Magufuli unategemea lifanye nini? Bunge lina wabunge 99.999% wa CCM.

Simtetei Samia kwa kutochukua hatua kwenye ropoti ya mwaka 2021/22 kama tulivyotarajia. Nchi hii inaendeshwa kwa Katiba na utawala wa Sheria. Rais hawezi kusomewa ripoti leo halafu kesho aseme kamata fulani na fulani peleka Mahakamani. Tutakuwa tuarudia UHAYAWANI uleule wa Magufuli aliyejaza watuhumiwa magereza lakini hakuna hata kesi moja aliweza kuimaliza hadi anakufa.

Upo utaratibu nankuna vyombo vya kufanya hayo mambo. Na mwenye majukumu makubwa ni Bunge.

Katiba inaruhusu Wabunge kupiga kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu kama maagizo ya CAG hayatekelezwi. Kura zikipigwa na wakashinda wanaosema hawana imani basi Rais anavunja cabinet.

Hatuitaji ubora, tunahitaji uwajibikaji

Nasikia waafrica mnalaana ; wakati wa nuhu mlimchungulia baba yenu akiwa uchi, kisha akawalaani, nasikia ile laana inawala hadi leo !

Eti ni kweli ?
 
Back
Top Bottom