Business idea: kufungua nyama choma center

Kifurukutu

JF-Expert Member
Aug 29, 2013
4,628
6,670
Igweeeee

Nimekaa nimewaza na kuwazua nifingue biashara gani ili maisha yasonge mbele hapa jijini

Wazo pekee ambalo naona linaweza kuwa tofauti kidogo na zile biashara za kuigana mwishowe kuanza kurogana ni kuanzisha NYAMA CENTER

NYAMA CENTER itakuwa inauza nyama za aina mbalimbali kama vile kuku, ngombe, mbuzi na kitimoto vyote center moja

Nyama center itaoffer nyama mishakaki, soup aina zote za nyama., lost, makange nk

Ugali chipsi na ndizi itakuwa ni sehemu ya huduma ndani ya nyama center.

Location ya biashara hii nafikiri kutafuta eneo sehemu either mbezi magufuli, goba center, makumbusho or kimara

Mtaji mpaka sasa ninakiasi cha 3M, naombeni ushauri kuhusu wazo hili
Je nitatoboa?
Mtaji unajitosheleza?
Nategemea wateja wa kawaida tu sehemu ambayo isiwe classic saaaana iwe ya kati
 
Wazo lako ni zuri but kwenye kitimoto usiiweke pamoja Tenga eneo lake maana ukanda wa pwani waislamu ni wengi na daima hawapendi kabisa kuchanganya hata vyombo ama kisu.

Hivyo kitimoto weka sehem nyingine Ili usikere watu wengine utauza!

Kilala kheri kwako. Ufanikiwe
 
Back
Top Bottom