Bungeni: Taarifa ya tume ya kuchunguza matokeo mabaya ya kidato cha nne yasomwa


Usiishie kukanusha, elezea wewe standardization ni kitu gani!
hii kwa Kiswahili inaitwa achanosanifu. Yaani kupunguza muachano kati ya alama na alama. Mfano, ukiwa na wanafunzi wawili, mmoja kapata 90 na mwingine kapata 10, waweza punguza achano lao ukamshusha wa 90 hadi 80, wa 10 ukampandisha hadi 21 kumtoa F hadi D. Kwa hiyo achanosanifu wakati mwingine huwa inakula kwa waliofaulu sana na kuwapiga jeki akina nanii.
Hii kitu ina formula yake
 
hii kwa Kiswahili inaitwa achanosanifu. Yaani kupunguza muachano kati ya alama na alama. Mfano, ukiwa na wanafunzi wawili, mmoja kapata 90 na mwingine kapata 10, waweza punguza achano lao ukamshusha wa 90 hadi 80, wa 10 ukampandisha hadi 21 kumtoa F hadi D. Kwa hiyo achanosanifu wakati mwingine huwa inakula kwa waliofaulu sana na kuwapiga jeki akina nanii.
Hii kitu ina formula yake

Aksante Waridi,
cc Mkoroshokigoli
 
Last edited by a moderator:
Lukuvi anawasilisha taarifa ya tume iliyoundwa na waziri mkuu kuchunguza sababu za kufeli vibaya kwa watajiniwa wa form 4. Na mapendekezo ya nn kifanyike.

Anasema sababu zilizotolewa ni upungufu wa waalimu, mazingira magumu a kufundishia, idadi kubwa ya shule za sekondari iliyopelekea idadi kubwa ya watahiniwa.

Baraza la mitihani ninaona halina maana yoyote!kwa nini washindwe kusimamia ukweli?inamaanisha hata waliopita hawakutendewa haki.
 
jaman grading hata ikiwa D inaanza na 15 watoto wetu watafeli tu,,,,hivi mnadhan NECTA KUTOKANA NA MATOKEO HAYA HAWAJA-STANDARDIZE?WAMEFANYA HILO,NA NDO UTARATIBU HUWA HIVYO,LAKIN WATAWALA WANARUKA KWENYE SABABU,


Haina maana kua kila mtu atafaulu ila tunataka usawa, siyo mtu anaibuka na kuanzisha vitu bila kuwashilikisha wahusika wakuu.
 
Ee Mola tunusuru wanawako wa Tanzania na michezo hii mibaya inayofanywa na viongozi wa Taifa hili katika elimu yetu, Amen.
 
Tulikubali wenyewe kuwapa nchi yetu ccm sasa kila matokeo tuyapokee.
Unajua mtoto akiambiwa hayo maji ni ya moto usiguse anatakiwa afanye mambo mawili, au atii au awe muasi. Akiasi anapata cha moto. Ndicho wanapata watanzania baada ya kuwa waasi na kuweka mguu ndani ya maji yanayochemka!
:pray2:
 
Kusahihisha mitihani upya maana yake nini? Ina maana wasahihishaji (markers) wa mara ya kwanza hawakufanya kazi yao vizuri?
 
baraza letu la mawaziri halina watu credible hivi haya maamuzi ni kwa faida ya nani? wanaleta siasa kwenye taaluma, uwezo wa kufikiri wa wajumbe wa baraza la mawaziri hauna tofauti na nguchiro hata nguchiro akiona mvua inakuja anaingia shimoni kujikinga na mvua, wangekuwa ni watu wanaofikiri wasingefanya huu ujinga wa kuingia shimoni hili jambo lilikuwa wazi na sababu zinajulikana muda mrefu na viashiria vilionekana mapema hivyo walitakiwa kujiandaa mapema na kufanya turnaround kabla hali haijwa mbaya, sasa huko shimoni walikotupeleka mvua ikiwa kubwa tutafia huko.
Kwa maamuzi haya baraza letu la mawaziri limejaa dullard animals the nguchiroz, iko haja kuwa na baraza amabalo litakuwa na watu amabao wanafikiri kuliko kuwa na hawa straight animals.
 
haisaidii kubadili matokeo tu! Kuna mambo menge yanayotakiwa kufanywa kama:
kuongeza walim, vifaa vya kufundishia, nyumba za walim, mazngira mazur ya kujifunzia.................
 
Sioni mantiki ya kurudia kusahihisha mtihani as lengo la kamati lilikuwa kutafuta sababu ya kufeli na kiwango cha elimu kushuka mwaka hadi mwaka. Kuna wanafunzi waliojiuwa baada ya matokeo kutoka kusahihisha kutawasaidia nini hata kama wamefauli baada ya kusahihisha tena. Kama ni mfumo wangekubali tu kuwa ni mbovu watafute suluhu. Ya mtaala usahihishaji waalimu na mengine waliyogundua lakini sio kurudia kusahihisha na kufuta matokeo.
Kusahihisha mitihani upya maana yake nini? Ina maana wasahihishaji (markers) wa mara ya kwanza hawakufanya kazi yao vizuri?
 
  • Thanks
Reactions: SMU
no CCM mwaka 2015,Maamuzi gani haya jamani?tumeshaambiwa hakuna walimu,no vifaaa wao wanafuta matokeo na yakisahihishwa yakaja vilevile?kwa nini wasitibu mizizi?sikubaliani na kufutwa kwa matokeo
 
Sababu za matokeo mabaya 10 ila mbinu ya kurekebisha tatizo ni moja tu.

Standard za kimataifa zimetupiliwa mbali. Hii ndio Tanzania. Tusubiri ya kidato cha sita
 
Serikali ya zimamoto tu hii. Watahiniwa wangapi wamejiua/wameozeshwa/kubebeshwa mimba? wengine wameshahama kwenye utaratibu wa masomo na kujiingiza kwenye utafutaji wa pesa kama za u-house girls.

Serikali ijenge shule na kusomesha walimu bure.
 
Kusahihisha mitihani upya maana yake nini? Ina maana wasahihishaji (markers) wa mara ya kwanza hawakufanya kazi yao vizuri?

Ni mfumo mbovu wa elimu tu mkuu SMU. NECTA inapaswa kufutwa na kuanzishwa upya
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: SMU
Kuwa ccm ni laana!! Tufiakwa najitemea mate kifuani.............!
 
Safiiiiii, hapa atakayepingana na tume basi mchawi , ikiwezekana waangalie CA za hao wanafunzi kutoka shule walizosoma na mitihani ya mock pamoja na kusahihisha upya kwa waliofeli
 
....serikali ya ajabu sana hii....wanataka kusafisha madudu yao ya kutojali elimu kwa kuwatwisha mzigo necta.....watoto wamefeli kidato cha nne kwa kuwa hawajui kitu na wala si kusaishiwa vibaya mitihani....watoto wajinga wamefeli....huu ukweli serikali bado hawajaukubali....wamekaa wamesomeana taarifa na tume...sasa wanakuja kufuta matokeo....yangu macho....nasema hakika mitihani hata kama ikisahishwa tena wale watoto watafeli tena tu...tena safari hii wanaweza kufeli zaidi....Leo serikali inataka kudanganya umma kuwa hakukuwa na standardization kwenye kusahihisha mtihani!!!....yaani wanaingiza siasa kwenye utendaji wa necta.....na wabunge wanashangalia kama mazuzu!!..yaani this country!!!.......yaani wabunge na mawaziri wanashangilia kufutwa kwa matokeo!!!kweli!!!.....yaani mzigo wameutwisha kwa necta.....kweli only in TZ....Yaani necta wawafelishe watoto kwa manufaa ya nani????hivi serikali hii inaongozwa na watu gani!!!!
 
Back
Top Bottom