Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 18,961
- 47,828
Tukitaka kuwa wakweli kwa nafsi zetu, Bunge la Tanzania la sasa halina faida wala msaada kwa Watanzania. Nina hakika hata kama lisingekuwepo, hakuna ambacho kingebadilika. Hili ni Bunge ambalo chochote kinachopelekwa Bungeni na Serikali, lazima kitapitishwa kama kilivyo. Namna nyingine, tunaweza kusema ni Bunge la hasara. Wanakula kodi zetu lakini bila kuwa na msaada wowote. Hili ni Bunge kikaragosi cha Serikali. Na anayeupinga ukweli huu, basi atuwekee kumbukumbu hapa, ni jambo gani baya lilipelekwa na Serikali hii Bungeni, Bunge hili likalikataa au kulifanyia marekebisho makubwa ya msingi. Tuna mambo mabaya kabisa ama yaliyotendwa na Serikali au watendaji wa Serikali hii, yalipopelekwa Bungeni, yakaenda tu kupata muhuri wa Bunge:
1. MKATABA WA HOVYO WA IGA
Mkataba ule kwa mtu yeyote mwenye uelewa na mkweli, ni mkataba wa hovyo kabisa, kwa sababu ulikuwa unakiuka sheria za nchi, na ulikuwa unapora mamlaka ya nchi katika kuamua yale inayoyaona yana maslahi kwa Taifa. Taasisi mbalimbali, kuanzia chama cha wanasheria nchini, taasisi za dini, wasomi wabobezi, wote walilaani kwa sauti kubwa IGA ile ya hovyo, lakini Bunge liliusifia na kuupitisha kama ulivyo. Na lile kongwa bado nchi imelivaa kama maadui wa Taifa walivyokuwa wamepanga.
2. MABADILIKO YA SHERIA YA UCHAGUZI NA TUME YA UCHAGUZI
Ile sheria ni ya hovyo. Taasisi mbalimbali zilizotoa maoni, kuanzia taasisi za dini, vyama vya siasa, chama cha wanasheria nchini, n.k; wote walionesha sheria ile ni kiinimacho. Lakini Bunge liliipitisha hivyo hivyo. Yaani Rais anateua majaji, halafu majaji wanapendekeza wajumbe wa Tume ya Uchaguzi kwa Rais, halafu Rais anawateua wajumbe waliopendekezwa na watu aliowateua yeye. Hii ni kuwafanya watu wote hawana akili.
3. TAARIFA YA CAG ILIYOONESHA UFISADI MKUBWA.
Sote tunafahamu, kila mwaka kumepelekwa taarifa ya CAG inayoonesha ufisadi mkubwa ndani ya mamlaka za Serikali, lakini hakuna chochote ambacho Bunge lilifanya, tena kwa kiasi kikubwa, Spika akionesha kupinga kujadiliwa ufisadi huo mapema baada ya baadhi ya wabunge kutaka wawajadili mafisadi.
4. UFISADI WA KWENYE SUKARI
Mheshimiwa sana. Ndugu Mpina ameonesha kwa namna iliyo dhahiri kabisa, jinsi Bashe alivyotenda kinyume kabisa cha taratibu, kwa kinachoonekana kwaajili ya manufaa binafsi yake na aliowapa contracts, na amefanya hivyo kwa vielelezo vilivyo dhahiri kabisa, Lakini Spika na wabunge wake wasio na sifa ya kuitwa wabunge, waliishia kupiga tu kelele za kumshambulia bila ya kujibu hoja zake hata moja.
BUNGE KAMA HILI LINA FAIDA GANI? LINAMTUMIKIA NANI?
Bunge hili lipo kwaajili ya kulinda maslahi ya Taifa na umma au kuyaangamiza.
Bunge hili lisilo na msaada kwa Taifa, lijifunze kwa yanayotokea Kenya, watu wasiishi kwa kukariri, kuna siku yatawapata yanayowapata wabunge wa Kenye sasa hivi:
Siku zote tunasema kuwa, Mwenye Hekima hujifunza Kutokana na Makosa Ya mwenzake. Lakini ukikosa hekima, akili na uelewa, yanayowatokea wenzako, unaamini ni ya kwao tu, hayawezi kukufikia wewe.
Haya yanayotokea sasa kwa nchi nyingi za Afrika, yakianzia West Africa, ni hatua tu za maendeleo za mwanadamu. Huko Ulaya na America yalitokea sana miaka ya 1960 mpaka 1970, na leo hakuna mtawala anayewaburuza bali watawala wanalazimika kufuata matakwa ya umma. Kwa bahati mbaya watawala wa Arika bado wamelala, na kwa kuwa hawataki kubadilika, watasombwa na mafuriko.
Kwa bahati mbaya Watanzania wamelala, maana ukiangalia kwa umakini, kwa hakika yanayofanywa na Bunge la Tanzania ni hovyo maradufu ya yale yanayofanywa na Bunge la Kenya. Fikiria hawa wabunge wa Tanzania wangekuwa Kenya, wangefanywa nini!!
Mpaka sasa:
1. Polisi wamezidiwa nguvu, wamekimbia, waandamanaji wamelichukua gari la polisi.
2. Kaunti zote za Kenya zimeandamana.
3. Watu wanne wameuawa kwa risasi za polisi.
4. Waandamanaji wamevunja milango ya Bunge na kuingia ndani.
5. Wamebeba siwa, wamevunja nembo ya Bunge, wameondoka na vazi la spika.
6. Wamechoma moto ofisi ya Gavana wa Nairobi.
7. Wamechoma moto supermarket ya mbunge aliyeunga mkono mswada.
8. Wamempiga vibaya mbunge aliyeunga mkono mswada, mlinzi wake akakimbilia kanisani.
9. Wamezingira ikulu ndogo ya Rais ya Nakuru.
10. Waandamanaji wanasema kuwa mamlaka ya Bunge yapo mikononi mwao kwa sasa.
11. Spika na wabunge wote wamekimbia, bila hata ya kuahirisha bunge kama kanuni zinavyotaka.