Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 38,269
- 47,492
Baada ya mkwamo wa muda mrefu uliochangiwa na baadhi ya wabunge wa Marekani wenye mahaba na Putin hatimaye bunge la Marekani limepitisha kifurushi kipya cha $billion 60 kwa vita vya Ukraine.
Msaada huu mpya kwa Ukraine unajiri baada ya mwaka mmoja na nusu tangu bunge lililokuwa likiongozwa na Democrats kupitisha msaada kwa vita vya Ukraine.
Ushindi wa Republicans mwaka jana katika bunge la Marekani uliweka mkwamo wa zaidi ya mwaka mmoja na nusu kwa Ukraine kupata msaada kutoka Marekani.
Hata hivyo spika mpya wa bunge la Marekani ameamua kuwapuuza wabunge wachache wa MAGA lakini wenye sauti kubwa ndani ya chama cha Republicans waliosababisha mkwamo huo na kuamua kupeleka miswada mitatu ya usalama katika bunge iliyopewa jina la "21st Century Peace through Strength Act" ambayo imepitishwa kwa wingi wa kura.