Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,934
- 13,689
Wakuu
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Februari 3, 2025 linaendelea na mkutano wake wa 18 ambapo, pamoja na Kipindi cha Maswali na Majibu, linatazamiwa kujadili hoja za kamati.
Innocent Bashungwa - Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi
"Serikali imeendelea kuimarisha jeshi la zimamoto na uokoaji kwa kulipatia vitendea kazi ili liweze kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi, kwasasa Serikali inatekeleza mradi wa ununuzi vifa mbalimbali vya kuzima moto na uokoaji pamoja na magari 150 ya kuzima moto na uokoaji. Pindi magari hayo yatakapofika nchi yatasambazwa nchi nzima"
"Tayari Rais ametuwezesha kununua magari 12 ya kisasa, hata juzi Kariakoo ilivyotokea janga la moto jengo (TRA) kuungua mliona aina ya mtambo ambao uliweza kuzima moto kwenye jengo refu, hayo ni magari ya kisasa ya zimamoto ambayotayari tunayo lakini vilevile tupo mbioni kununua Helkopita maalum kwa ajili ya jeshi la zimamoto na uokoaji"
Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. David Silinde amesema "Tunatambua kwamba kuna changamoto ya Mbegu hapa nchini pamoja na bei na ndio maana katika moja ya jitihada ambazo Serikali inazifanya sasa hivi ni pamoja na kuweka ruzuku katika bei ya mbegu za mahindi ambazo tumeaza kutekeleza katika msimu msimu wa 2024/25."
"Lakini pili tulielekeza Taasisi ya Kuthibiti Ubora wa Mbegu Tanzania (TOSCI) kupitia kupitia makampuni yote yanayozalisha mbegu pamoja na mawakala na maduka yote yanayozalisha mbegu ili kuona kama wanafuata elekezo la bei elekezi na moja ya hatua ambazo tumezifanya ni kunyang'anya leseni wale wote wanaowauzia wakulima bei zaidi ya ile elekezi na wanauza mbegu feki"
Mbunge wa Jimbo la Mbagala, Abdallah Chaurembo amesema Shirika la Posta kwasasa linadaiwa TSh. Bilioni 54.7 hivyo kushindwa kujiendeleza na pia shirika limeshindwa kukopesheka, tuimbe sana serikali kama ripoti yetu ilivyoeleza tunaomba serikali ilichukue deni hili ili shirika hili la posta sasa liweze kukopesheka.
Mbunge wa Viti Maalum, Sylvia Sigula amesema shirika la ndege nchini (ATCL) linakabiliwa na changamoto ambazo zinakwambisha kufikia malengo yake akiitaja changamoto kubwa ni matatizo ya usanifu wa ndege yetu ya Air Bus Airbus A220-300 ambayo imekuwa na hitilafu kwenye Injini zake.
Sababu hii amedai inafanya ndege yetu kupata hitilafu za mara kwa mara na kulisababishia shirika hasara ambapo kwa mwaka mmoja ndege hizi zimesazalisha hasara ya TSh bilioni 127.3.
Mbunge wa Geita Vijijini Joseph Kasheku Musukuma amesema haina haja ya kuweka wahudumu wanaotoa huduma za ndani ya treni ya Mwendokasi (SGR) ili kuepuka shirika kupata hasara kwakuwa ndio kwanza mradi huo umeaanza hivyo haina haja ya kuweka gharama kubwa za uendeshaji.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma amesema katika jitihada za kukabiliana na mabadiliko ya kasi ya teknolojia, hasa kwa maudhui yanayopitia kwa watoa huduma za intaneti, Serikali kupitia Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imeendelea kuhuisha kanuni zinazosimamia maudhui mtandaoni ili ziweze kuendana na kasi ya mabadiliko na kuhakikisha maadili na utamaduni wa Tanzania unalindwa.
Amesema TCRA imeendelea kutoa leseni za maudhui mtandaoni kwa maombi ambayo yanakidhi vigezo vilivyowekwa, pamoja na kuwachukulia hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kuwafutia leseni watengenezaji wa maudhui mtandaoni wanaokiuka sheria na kanuni za utangazaji ikiwemo uvunjifu wa maadili.
Vilevile, amesema Serikali kupitia Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imeendelea kutoa elimu ya matumizi sahihi na salama ya mtandao.
Aidha, amesema suala la kuzingatia maadili na utamaduni wa taifa ni suala mtambuka na huanzia ngazi ya familia, shuleni na jamii kwa ujumla.
“Hivyo, kila mwananchi kwa nafasi yake anapaswa kuwa mlinzi na msimamizi wa maadili na utamaduni wa taifa letu,” amesema.