"Bora ukosee kujenga kuliko kukosea kuoa" ni msemo wa kijinga kabisa. Unajua gharama za ujenzi wewe?

Nilitumia miaka zaidi ya 10 nyumba yangu kukamilka kabisa,gharama sitataja ila itoshe kusema nyumba yangu ni ya thamani kuliko wanawake wote niliowahi kuoa au kuwa nao kwenye mahusiano.

Leo hii ukibomoa hako kajumba kangu umenimaliza,kuja kuijenga tena sio rahisi,lakini huyu mke hata akiondoka leo mwezi mmoja navuta mwingine

Hapa naongelea nyumba za kuanzia milioni 30 sio hizo slope za Singida

Tusidanganyane
Mkuu ..hivi nyumba ya mil 30 ikoje? Maana mm navyojua nyumba ya maana ni aghalau mil 70-100
...maana kwa mjini kiwanja tu kizuri ni 15m mpaka 20m..
 
Mkuu ..hivi nyumba ya mil 30 ikoje? Maana mm navyojua nyumba ya maana ni aghalau mil 70-100
...maana kwa mjini kiwanja tu kizuri ni 15m mpaka 20m..
Zipo mkuu hasa mikoani,nyumba ya milioni 30 inaridhisha ,ujenzi kwa mikoani uko chini na hazina mbwembwe inaweza isiwe na plumbing sijui tiles au gypsum na bado ikaonekana nzuri
 
Subiri nakuombea ukosee kuoa kisha ulinganishe na huo upuuzi unapusema.

Ndipo utajua kwanini Elon Musk, Jeff Bezos tajiri namba moja na mbili waliacha wake nabhawataki kusikia habari za wake.

Hiyo kauli ina maana kubwa sana. Hata hako kajumba kako utatamani kukaboa au kutoingia humo.

Anyway, ukikua utajua
Tatizo kung'ang'ania maisha na mtu ambaye anaumiza moyo wako kila siku. Unakaaje na mtu ambaye anakuharibia maisha yako? Hata siku moja sitakubali ndoa iniharibie maisha yangu.
Bora kuachana
 
na me huo msemo niliuelewa hivyo huenda mwandishi ana akili nyingi kama tulivyoambiwa wanawake tuishi nao kwa akili. Mwandishi asibezwe hoja anayo.

kuna jamaa alisema ukiona mke wako mkorofi na una miliki mali za thamani hati zote za nyumba andika jina la mama yako mzazi wakija kuangalia wanakuta mume hana chochote kwahiyo huyo mke anakuwa amekosa alichokikusudia.
Na ukitangulia wewe na mama kama kuna wtt mshawakosesha haki zao.
Mke hata akikutoa ndani ya nyumba walau uhakika wa wtt wako kutokupata tabu upo
Nimewaza tu
 
Back
Top Bottom