Bora mahusiano yakulize huku una hela kuliko kulizwa na hela huna 😔

Mwanasayansi Kalivubha

JF-Expert Member
Feb 4, 2024
308
822
BORA MAHUSIANO YAKULIZE HUKU UNA HELA KULIKO KULIZWA NA HELA HUNA 😔

Mahusiano ni eneo ambalo linazungumzwa sana ikiwa ni kiashiria kuwa wengi hujihusisha huko ila pia changamoto ni nyingi sana huko .

Usipojidhibiti utajikuta muda mwingi unafikiri tu mahusiano kuliko mambo mengine na huo ndio mwanzo wa KUJIUA /KUUA AU KUCHANGANYIKIWA NA KUBAKI MASKINI.

Kibaya zaidi ni kuteswa na vyote viwili UMASKINI NA MAHUSIANO , mateso yake ni mabaya sana kwa sababu utajiona kama unaonewa kwa sababu huna pesa kumbe ni uhalisia tu wa mahusiano ulivyo.

Usikubali uteseke na vyote na hasa kwenye pesa hapo acha mahusiano yakutese ukiwa tayari na pesa na tena usikubali mahusiano yakutese kiasi cha kukosa nguvu za kutafuta pesa.

#mwanasayansi Saul kalivubha.
Fikia Ndoto Zako.
 
Kwel kabisa mkuu

Niliwah kuishiwa pesa nikaanza kumkwepa mpenz wang,siku moja nikamkuta na jamaa,nikajikuta naumia sana hapo ndo nilipogundua kuwa kumbe nilikuwa nampenda sana

Baada ya hilo tukio nikataman niachane nae mazima lakin ajabu nilishindwa kumsahau,ikabid nianze kumtafuta na kumshawish turudiane,katka kumsumbua sana nikaona demu anataka kunirudia tena na wakati huo mimi ni apeche alolo,kila demu akikaribia kurudi nawaza nitampa nini

kUkosa hela ni kubaya sana
 
Wanaume wengi ni emotional unstable ndio maana wanawake wanatake advantage yaani mwanaume una kazi na hela kidogo unapata unapelekeshwa na mwanamke kama gari bovu mimi wanawake wanasema nina dharau ila kuliko kupelekeshwa na mwanamke bora nipige bakari nondo yaani hela nikupe na dharau uniletee I wish I could be IGP.
 
Yaani uwe na hela then ulizwe na mapenzi? Itakuwa utoto unakusumbua bado
 
Kwel kabisa mkuu

Niliwah kuishiwa pesa nikaanza kumkwepa mpenz wang,siku moja nikamkuta na jamaa,nikajikuta naumia sana hapo ndo nilipogundua kuwa kumbe nilikuwa nampenda sana

Baada ya hilo tukio nikataman niachane nae mazima lakin ajabu nilishindwa kumsahau,ikabid nianze kumtafuta na kumshawish turudiane,katka kumsumbua sana nikaona demu anataka kunirudia tena na wakati huo mimi ni apeche alolo,kila demu akikaribia kurudi nawaza nitampa nini

kUkosa hela ni kubaya sana
Nimecheka saaaana
 
Back
Top Bottom