Hii habari nami nimeitazama ITV na kujaribu kulinganisha na matukio ya dizaini hii yanayotokea nchi zingine kama Somalia, Kenya nk ya watu kulipua maeneo kwa lengo la kuua na kuleta uharibifu, hili la Zenj hata halijaniingia akilini mwangu...haraka haraka akili yangu inagoma!
Ukiicheki vizuri ni kana kwamba tukio la kutengenezwa kwa makusudi flani kuanzia hata wale watu wanaohojiwa, maneno ya yule Balozi Iddi Seif.....utata mtupu!!!!!!
Kwanza walipuaji walienda wakalipua kontena lenye rangi ya njano na kijani ambazo nafikiri ndizo rangi za bendera ya Chama Cha Mazombie
Halafu mlipuko umetokea kukiwa hata hakuna watu ndani au kuzunguka maeneo yale na haikulezwa imetokea wakati gani
Hawa wanatafuta sababu za kuanza kamata kamata tu au sbb za kuahirisha uchaguzi wao huo wa kisanii ili Dr Shein na CCM wapate sababu za kuongezewa muda wa kuongoza!!
Kuna mdau mmoja aliwahi kuandika kuwa, hiki kinachoandaliwa Zenj wala hata si "uchaguzi wa marudio" bali ni usanii tu unaofanywa kwa ustadi mkubwa ili kupata sababu ya kuvifanya visiwa hivyo kutangazwa kwa hali ya hatari na kwa misingi hiyo kupigwa narufuku kwa shughuli zozote za kisiasa kwa muda usiojulikana!!