Bomoa bomoa Kimara mwisho yaja ujenzi wa "Parkings"

Unajua sisi watanzania wa ajabu sana utajengaje barabarani?, ata kama shida yako ujenge flemu, basi kwanini usione mamlaka husika ujiridhishe?, hiyo biashara ya kununua viwanja kwa njia za panya ndio zinatutokea puani sasa
 
mkuu hizo nguvu naona wangeAmishia dodoma ambapo wanaenda! Mana kule mmhhh!!
Dodoma kuna mpango mzuri
Dar lazima ibadilishwe
hili ndilo jiji kuu na labiashara Tanzania
hakuna namna,

watu wanaongezeka kila kukicha
ilikuwa Laki 8
sasa ni milioni5
lazima tukubari maumivu ya muda.

waambie basi watanzania wasiongezeke dar
waende Dodoma kama watakubari
 
Hii si haki hata kidogo! Watu wanajinyima sana ili waweze kujenga nyumba zao. Wakati ujenzi ukiendelea Serikali inaona ujenzi ukiendelea haitii neno. Basi angalau walipwe fidia ili wakaanze upya sehemu nyingine.
Wewe hizo sheria zipo siku nyingi, hayo maneno kuwa unajenga unaonwa hayana maana, kwani kuna makosa mangapi unafanya huku ukionekana?, ukifuata taratibu zote huwezi kuingizwa mkenge
 
.....tumepokea barua za notice ya siku saba kutoka Tanroad.
Hivyo bomoabomoa iko njiani

Umejibana weeee for the past 18 years ili ujenge ka-kibanda kako. Ile unamaliza tu, unapewa notice ya siku 7 uwe umevacate eneo hilo. Kazi kwelikweli.
 
Mbona machinga wanaofanya kazi kwenye maeneo yasiyoruhusiwa hawaondolewi, na na wameruhusiwa kuendelea na biahara zao? Hawa wana tofauti gani na wale waliojenga kandokando ya barabara? Tunatekeleza sera gani hasa inayoruhusu baadhi ya mambo haramu na kukataza mengine???
 
Dodoma kuna mpango mzuri
Dar lazima ibadilishwe
hili ndilo jiji kuu na labiashara Tanzania
hakuna namna,

watu wanaongezeka kila kukicha
ilikuwa Laki 8
sasa ni milioni5
lazima tukubari maumivu ya muda.

waambie basi watanzania wasiongezeke dar
waende Dodoma kama watakubari
jiji zima lingefumuliwa maana hAlikujengwa bila hata mpangilio!
 
Hizo mita za barabara zinaongezeka kila waongezapo barabara ? Kwa kuwa wakati wa kujenga leni NNE kuna watu waliobomolewa na kwa sasa kutoka ubungo hadi KIMARA mwisho kuna leni NNE na mbili za BRT bado watu wako barabarani ?
Iitumike sheria mpya kwa nia ya kuwaumiza watu. TANROADS hawana ARDHI wenye ARDHI ni wizara ya ARDHI hivyo wanatakiwa kuwaomba wizara ya ARDHI iwaonyeshe Maeneo wanayoweza kujenga parking na kama kuna wanaoyamiliki ARDHI wataagiza wafidiwe
 
Hatimaye Jana Mh.Rais wakati anazindua mradi wa Mabasi ya Mwendokasi UDART aliwaagiza mawaziri husika kuwasiliana Na Wakala wa Barabara TANROAD kutumia Sheria za Barabara kuwaondoa Kwa kuwabomolea Nyumba wale wote waliojenga ndani ya Hifadhi ya Barabara ili eneo hilo litumike kujenga PARKINGS kubwa Kwa ajili ya wenye Magari binafsi waache Magari yao hapo Na kuingia kwenye mabasi.Mh.Rais akasisitiza kuwa Eneo hilo halina kulipwa FIDIA.
Naona watu wakibomolewa nyumba zao bila fidia na siku nyingine wakalala njaa wanaweza wakajua wajibu wao katika nchi yao na hii bomoabomoa bila fidia nimeipenda kwa sababu ina harakisha maendeleo upande mmoja lkn inawaanda watu kujua wajibu wao siyokushabikia kila kipichato
 
Kiranja yuko sahihi japo itaumiza watu.pin za Tanrod zipo tokea 72 na wenyeji wanajua kipindi cha operation sogea.ila wenyeji wanawauzia wakuja ndio wanaona wanaonewa.huwezi kuta mwenyeji kajenga mbele.mtafute Mzee Nguma Kimara korogwe akupe historia na akuonyeshe pini za kipindi chs awamu ya kwanza.
 
Ni vizuri kufuata sheria kama zilivyoandikwa kwenye vitabu lakini tusisahau kuwa miji yetu hasa Dar es Salaam zaidi ya 70% ya maeneo hayajapimwa. Tatizo kubwa zaidi ni kwamba waliofanya na kusimamia uzembe huu ni chama cha anayeamrisha na yeye akiwa sehemu ya hilo tatizo kama anavyotuaminisha kila siku kuwa amekuwemo serikarini kwa zaidi ya miaka 20.
Naendelea kuamini kuwa ukitaka kila mtu Dar es Salaam aliyejenga maeneo yasiyostahili abomoe basi mji utabakiwa na wakazi waziofikia hata laki saba (700,000) maana wengine wamajenga kwenye mashamba yao halali na walivyoomba serikali iwapimie mizengwe ikawa mingi!
Au basi kama ni kwenda sawa basi tupitie upya hata uuzwaji wa nyumba za serikali na ikibainika utaratibu haukufuatwa basi sheria kama ilivyoandikwa ichukue mkondo ili kusiwe na wa kumlaumu mwingine.
 
Hizo mita za barabara zinaongezeka kila waongezapo barabara ? Kwa kuwa wakati wa kujenga leni NNE kuna watu waliobomolewa na kwa sasa kutoka ubungo hadi KIMARA mwisho kuna leni NNE na mbili za BRT bado watu wako barabarani ?
Iitumike sheria mpya kwa nia ya kuwaumiza watu. TANROADS hawana ARDHI wenye ARDHI ni wizara ya ARDHI hivyo wanatakiwa kuwaomba wizara ya ARDHI iwaonyeshe Maeneo wanayoweza kujenga parking na kama kuna wanaoyamiliki ARDHI wataagiza wafidiwe

Haziongezeki hata kidogo, ni kwamba kutoka katikati ya barabara iwe lane nne ama moja unapima urefu husika ndo hifadhi ya barabara.
Lakini kuna wengine wala siwaonei huruma hata kidogo, ninapoishi pamepimwa na waliweka mita 10 za barabara sasa kuna mtu anasema eti mita nne zinatosha, kajenga ukuta katwaa mita sita kati ya kumi sasa huyu akibomolewa watu watalaumu serikali kweli!!!!!!
 
Huyo kayataka mwenyewe. Nazungumzia hawa waliopembenj ya Moro road hadi KIMARA hifadhi ya Barbara iliyobaki ni mita ngapi ? Natqmbua baada ya KIMARA mwisho hifadhi bado itakuwa ni kubwa. Lakini pia serikali ya sasa imezidisha ubabe kwa kuwa imemilikk mihimili mingine yote
Hakuna Mahakama wala Bunge na hata Media
Vyote ni sehemu ya Urais
 
Hii si haki hata kidogo! Watu wanajinyima sana ili waweze kujenga nyumba zao. Wakati ujenzi ukiendelea Serikali inaona ujenzi ukiendelea haitii neno. Basi angalau walipwe fidia ili wakaanze upya sehemu nyingine.
Kwaani nayo ilikua ni kazi ya magufuli kuwaelekeza msijenge kwa barabara
 
Back
Top Bottom