Bodi ya utalii yaaswa kutumia njia za kisasa kutangaza utalii nchini

mkiluvya

JF-Expert Member
May 23, 2019
812
732
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Dkt. Hamisi Kigwangalla ameitaka Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) iwekeze zaidi katika matumizi ya njia za kisasa za mawasiliano na mbinu rahisi zenye gharama nafuu kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo hapa nchini.

Dkt. Kigwangalla ameyasema hayo jijini Dodoma wakati akizindua rasmi Bodi hiyo iliyongezewa muda wa miaka 3 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli Aprili 23 mwaka huu.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Bodi hiyo amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuiongezea kipindi kingine cha miaka 3 na kuitaka bodi hiyo iendelee kubuni na kuongeza mbinu mpya za kutangaza utalii zitakazoleta tija na matokeo ya haraka.

Amewataka wajumbe wa Bodi hiyo kufanya kazi pamoja na kushirikiana na taasisi nyingine za Wizara ili kuongezea idadi ya watalii wanaoitembelea Tanzania akiweka msisitizo katika matumizi ya mifumo ya kisasa ya mawasiliano ili kupanua wigo wa kutangaza vivutio vya utalii kuliko ilivyo sasa.

“Bodi ya utalii mnapaswa kuona fursa zilizopo na kutimiza majukumu mliyopewa kwa tija na ufanisi zaidi, namna pekee ya kufikia malengo hayo ni lazima mtumie teknolojia na mbinu rahisi za mawasiliano zenye gharama nafuu kutimiza majukumu yaleyale ya kutangaza vivutio vya utalii kisasa zaidi” Amesisitiza.

Ameipongeza bodi hiyo kwa kazi nzuri inayofanya ya kuendelea kuhamasisha shughuli za Utalii nchini na kuongeza kuwa kati ya vitu vilivyo iletea heshima sekta ya utalii Tanzania ni uwepo wa Kaulimbiu ya “TANZANIA UNFORGETTABLE” ambayo imekua chachu kwa taifa hasa katika kuitangaza sekta hiyo kitaifa na kimataifa.

Amesema kupitia kaulimbiu hiyo watalii wengi wanaoitembelea Tanzania wataendelea kukumbuka mambo mazuri na vivutio vizuri walivyoviona na kuendelea kuichagua Tanzania kuwa mahali pao pa kufanyia utalii.

Aidha, ametoa wito kwa Bodi hiyo kuendelea kuweka mazingira na kuongeza soko la bidhaa za utalii za Tanzania nje ya nchi kupitia maonesho ya kimataifa na kuwa na mkakati wa kulenga soko husika pamoja na kuonana na watu watakaouziwa bidhaa moja kwa lengo la kukamata soko katika maeneo kadhaa.

Pia ameitaka Bodi hiyo kuweka mkakati mahususi ya kukamata masoko mapya ya watalii kutoka nje ya nchi kutoka nchi za Marekani, Hispania, Urusi na nchi za Falme za Kiarabu zikiwemo za Dubai na Oman ambazo watu wake wakiwemo wasomi, wafanyabiashara, wanamichezo na watu maarufu wanapenda kwenda mapumziko ya muda mrefu na kutumia fedha nyingi kwa shughuli za utalii.

Katika hatua nyingine ameishauri Bodi hiyo kuwatumia watu maarufu na mashuhuri wakiwemo wasanii na wanamichezo watakaoalikwa mahususi kwa kazi maalum ya kutangaza utalii wa Tanzania.

“Licha ya changamoto ya ufinyu wa bajeti tunaweza kuweka mikakati ya kutangaza vivutio vyetu kwa tija na rahisi zaidi na kuifanya nchi yetu ijulikane na kuonekana na watu wengi , kuna mikakati tunaweza kuifanya mara moja tu ikadumu kwa muda mrefu, kama tukiwatumia watu mashuhuri wenye wafuasi wengi wakatembelea vivutio vyetu tuna uhakika watu wengi zaidi watafuatilia ziara zao na kufuata walichokichagua, lazima tuweke mikakati ya kuwaleta watu mashuhuri walau 5 kwa mwaka ambao sisi tutawaalika, tutapata mafanikio makubwa sana ndani ya muda mfupi” Amesisitiza Dkt. Kigwangalla.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constatine Kanyasu akizungumza wakati wa uzinduzi wa Bodi hiyo amemshukuru Rais kwa kuiongezea kipindi kingine cha miaka cha miaka 3.

Amesema kuwa katika kipindi cha miaka 3 imefanya kazi kubwa licha ya changamoto mbalimbali inazokabiliana nazo akisisitiza kwamba uwepo wa changamoto hizo ni uhalali wa kuwepo kwa bodi hiyo.

Amesema kuzinduliwa rasmi kwa bodi hiyo kutaifanya itekeleze majukumu yake kwa kasi kubwa zaidi akisisitiza kwamba kupitia bodi hiyo sekta ya Utalii Tanzania itasonga mbele kwa kasi kubwa zaidi.

Mhe. Kanyasu ameitaka bodi hiyo iongeze juhudu ya kutangaza utalii na kupanua wigo wa kutangaza soko la utalii ndani na nje ya nchi akisitiza akisisitiza kwamba bado kuna mazao mengi ya utalii ambayo hayajavunwa na endapo bodi itafanya kazi yake ipasavyo Tanzania itapata mafanikio makubwa kiuchumi.

Naye Mwenyekiti wa Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii Tanzania Jaji (Mst) Thomas Mihayo akizungumza mara baada ya kuzinduliwa kwa Bodi hiyo amemshukuru Rais hiyo nafasi nyingine akiahidi kwamba bodi yake itafanya kazi kwa kasi na bidii zaidi ili kutimiza malengo ya kuitangaza Sekta ya utalii ndani na nje ya nchi.

Jaji Mihayo amesema kuwa Bodi hiyo itaendelea kutekeleza majukumu yake chini ya uongozi wa Wizara na kuitangaza kikamilifu sekta ya utalii ndani na nje ya nchi.

Bodi hiyo yenye wajumbe 6 iliongezewa muda wa kuhudumu wa miaka 3 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli Aprili 23, 2019.
 
2015
Tanzania Tourism (Unforgettable Tanzania )


Tanzania is home to some of Africa's most famous national parks and the majestic Mount Kilimanjaro rising above the Serengeti.

Most visitors will find themselves passing through Dar es Salaam and heading out on safaris and various wildlife viewing adventures.

For those who want to take a break and spend some time soaking up the sun, the beautiful beaches of Zanzibar beckon.

Off Pemba and Mafia islands is a whole other kind of natural wonder, one most appreciated by the scuba divers and snorkelers who come here from around the world to experience the coral gardens, colorful fish, and crystal clear waters
Source: Tanzania Tourism
 
22 June 2017
Tanzania Safari Tips - How to Have An Incredible Safari in Tanzania !

In this video I share my Tanzania Wildlife Safari Highlights and recommended must-see places and sights to visit:

Serengeti National Park, Ngorongoro Conservation Area and Crater, Tarangire National Park and visiting a Maasai Village.

I explore and show the range of wildlife to be seen and show them up close. I also discuss the ways to get to see them. I travelled to Tanzania on a tour with Titan Travel called "Wild Plains of Tanzania" and saw all these places and more.

For more, including the lodges I stayed in watch my other Tanzania videos and visit my focused page on my blog at http://www.tipsfortravellers.com/tanz...
Source: Tips for Travellers
 
Hii bodi kwa kweli iko vizuri sana,nahisi hata ile Safari Channel ni moja ya kazi yao...
 
June 7, 2019
Arusha, Tanzania

MAONESHO YA KARIBU KILIFAIR 2019


Source : maliasili na utalii Tanzania
 
Vipi saivi kawa mpole? Si alijifanya kuivunja hii bodi kwa madai kuwa imeshindwa "kuperfom" halafu Rais akamteulia hio hio....leo anasema wamefanya kazi nzuri
 
June 7 , 2019
Arusha, Tanzania

KARIBU - KILIFAIR 2019

KARIBU-KILIFAIR is East Africa's largest tourism fair, promoting and presenting Tour companies, Hotels, Lodges, Airlines and other tourism stakeholders based in Tanzania, East Africa and Central Africa. The fair has the character of a business networking event for the tourism industry, in combination with a community fair to attract travel interested families & expats on the weekend.


Source : Karibu Kilifair
 
May 2019
Kilimanjaro, Tanzania

330 Chinese Tourist departed from KIA - Kilimanjaro International Airport after amazing safari trip in Tanzania.

Source : Utalii popote
 
Tatizo serikali yetu inahisi kila kitu ni politics. Ina sahau kuwa kuna vitu huwa vinatengenezwa na kuimarika kwa kupitia wadau especially sekta binafsi. Kwa mfano ukienda hapo Kenya, walikuwa wanafanya vizuri sana utalii huku wakijinadi na kutumia rasilimali zetu sisi watanzania hado miaka ya karibuni tulipoanza kuchangamkia fursa, lakini influence haikuwa ya serikali bali ni sekta binafsi walikuwa wanajitutumua kibiashara na ndipo mambo yakajibu.
 
Back
Top Bottom