Bodi ya Mkopo imenikata wakati haikunisomesha, tafadhali nisaidieni nimechanganyikiwa!

>> hapo watakuwa Wamekukata Kutokana na ELIMU ulioipata hiyo na Sio BODI >>maana Yake ni Kwamba HR wako Anakufanya ''chumio'' kwa miezi kadhaa.
 
Kama hujatumia hela zao wana ujasiri gani wa kukukata? Wewe fungua kesi ili hata hiyo amri ya kusitisha makato wapelekewe na mahakama
 
Itakuwa ulipata mkopo ila kuna mjanja alikuwa anapiga shoo hadi mwisho unamaliza chuo......usikate tamaa wafuate maana wemebadili namna ya kuwaibia watu. HESLB sio watu wazuri....wanafanya kazi kwa unafki ofisini
 
Mwajiri wako ndiye aliyeingiza makato ya Loan bodi kwenye Mfumo wa mishahara yaani Human Capital Management system Wengi huiita Lawson Hivyo jitahidi kabla ya tarehe tano mwezi wa tatu uwe umeshawasiliana naye ili akuondoe kwenye mfumo husika kama alikuingiza kimakosa baada ya tarehe tano makato hayataweza kuleta effect kwenye mshahara ujao. kuhusu swala la kukurejeshea kiasi ulichokatwa kimakosa huyo mwajiri wako anapaswa kukuandikia barua akiieleza Loan Board makato yaliyowasilishwa kwao yakikuhusu ww yamefanyika kimakosa hivyo loan board wataku refund but hakikisha anaambatanisha nakala ya deduction sheet pamoja na vielelezo vyote muhimu.
Njia hiyo itakusaidia kwa wepesi kuliko kukimbilia mahakamani.
 
Pole sana!

LAKINI mimi nafikiri imefikia wakati ambao "kila mtu abebe msalaba wake mwenyewe."

Ukitaka kulalamika sawa, ukitaka kwenda mahakamani ni sawa, ukiamua ku mute ni wewe!

Kazi kubwa tuliifanya 2015, lakini mkatupuuza.

[HASHTAG]#Kila[/HASHTAG] mtu abebe furushi lake mwenyewe#
 
Pole mkuu,

Hawa jamaa hawakua na database ndo maana waliweka hadi watu ambao hawakuwai kufika hata chuo......walikua wanabahatisha tu
Ni kweli paka marehemu walikuwa wanasoma wanapewa na mkopo na wanafanya kazi wanapokea pesa mwisho wa mwenzi wanakopa daaa tanzania ni pasua kichwa ni bora utawale kama baba riz ukijifanya ww mjuaji hii nchi wauni ni wengi sana
 
Asante kwa ushauri wenu mzuri baadhi naona mnaingiza na utani lkn sio mbaya.....hatua lazima nichukue ili makato yasitishwe maana ni maumivu kwangu
 
Tanzania mambumbumbu wengi mno ,sasa unlialia nini huku fursa imejitokeza.Serikali hii haina huruma na wananchi wala watumishi wa umma.Fungua kesi ya madai upate pesa ujenge
 
Wadau habari za mchana,

Mimi naishi Mwanza jiji ni mtumishi ambaye bodi ya mkopo ya elimu ya juu haikuwai nilipia hata dhumuni lakini mshahara wagu wa mwezi huu wamenikata 107,000/-.Nimeenda ofisini kwao PPF PLAZA ofisi za Kanda ya ziwa nimejilijisha ni wao wamenikata hiyo hela na kujua pia nitarudishiwaje pamoja na namma ya kusitisha makato haya.

Maelezo walionipa eti niandike barua na niweke kiambatanisho kwa maana ya salary slip then nisubili siku 12 nitarudishiwa fedha yangu na kusitisha makato hayo. Basi wakati nipo ndani naandika hiyo barua ghafla walikuja watumishi wanne nao wakilalamika kwamba makato bado yanaendelea ndo ikabidi kuuliza kulikoni jamani, ndo wakanisimulia na kunionesha barua zao za tangu mwezi NOV 2016 juu ya kulalamikia makato hayo na kibaya zaidi mwezi huu yameongezeka kutoka 8% hadi15% wakati bodi haikuwai wasomesha na hatua za kusitisha makato nazo ofisi haizishughuliki.

Nahisi kukata tamaa wadau nisaidieni hatua za kusitisha haya makato ya bado kwa sisi ambao hatukusomeshwa na bodi na maelezo ya ofisini ni uongo mtupu.
Kiongozi usiwe na hofu utaratibi waliokuambia Utarudishiwa.mie nilikuwa mhanga kama wewe .kipindi cha nyuma bodi walikuja kuonana HR wa LGA wao wakaorodhesha yeyote aliyegraduate wakijua alipata mkopo wakati equivalent kipindi hicho tulinyimwa .nilivyoanza kukatwa niliwafata wakati huo wako TIRDO msasani na vielelezo vya vya risiti ya chuo ya tuition fees .cha kwanza walinipa barua ya kumuelekeza mwajiri Wangu(DED)asitishe makato na baada ya miezi kadhaa hela zote zilizokatwa zilirudishwa kwenya akaunti yangu.Hivyo usihofu kama kweli hukuwahi kupata mkopo, fata taratatibu walizokwambia hela itarudi.
 
Tafuta wakili fungua kesi, hapo kwa harakaharaka unaweza kuwafungulia kesi zaidi ya tatu (Ila hakikisha unamuhaidi hakimu kitu baada ya kesi ili ieende fasta mana kesi ipo wazi kwako):
  1. Wame affect cash flow yako kwa maana baadhi ya matatizo uliyokuwa nayo yameshindwa kutatulika kwa wakati na hivyo wamekuongezea matatizo. (Interest)
  2. Wamekusababishia msongo wa mawazo kwa kutokutatua matatizo yako kwa wakati.
  3. Wameingia kwenye account yako bila idhini yako kwa sababu ilitakiwa wakujulishe kwa barua ku declare deni lako kama ni sahihi au la.
 
Mtu WA kusitisha mkopo ni bosi wako mkuu.
Mfuate yeye Mwambie kakuingiza Kwenye makato ambayo hayakuhusu.
Ni Sawa na mtu akuingize Kwenye makato ya benk wakati haina mkopo na wewe.
 
Serikali haina pesa sasa itakusanya vip pesa ya miradi ni pamoja na kutumia nguvu.. hamkusikia na mahakama inatakiwa iwe chanzo cha mapato
 
Hii nchi inaendeshwa kihuni sana.taasisi zote zinaongozwa na wahuni na villaza
 
Back
Top Bottom