Bodi ya Mikopo Elimu ya Juu (HESLB) yaja na 'Kampeni ya Fichua' kuwasaka wadaiwa sugu

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) leo (Ijumaa, Juni 28, 2024) imezindua Kampeni Maalumu inayolenga kuwashirikisha wananchi kwa kutumia simu na mitandao ya kijamii, kuwafichua wadaiwa sugu wa mikopo ya elimu ya juu.


Kampeni hiyo, inayofahamika kama #Fichua imezinduliwa jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Dkt. Bill Kiwia ambaye amesema kampeni hiyo itaendeshwa kwa miezi miwli kuanzia leo, Juni 28.

Lengo la Kampeni ya #Fichua

“Kampeni hii inalenga kuwashirikisha wananchi kutimiza jukumu la kizalendo la kuwafichua wadaiwa wa HESLB wenye kipato lakini hawajitokezi na kuanza kurejesha,” amesema Dkt. Kiwia katika mkutano na wanahabari.

“Tumeipa jina la #Fichua – KUWA HERO WA MADOGO ili kuhamasisha wananchi kushiriki katika urejeshaji wa mikopo iliyoiva ili iwanufaishe wengine – hatua ambayo bila shaka itawawezesha vijana wengi zaidi kupata elimu ya juu na wewe mwananchi kuwa SHUJAA wao,” ameongeza Dkt. Kiwia.

Utaratibu wa kuwafichua wadaiwa sugu

“Ili kutoa taarifa za wadaiwa, mwananachi anapaswa kutuma majina ya mnufaika, chuo alichosoma, eneo analofanya kazi, jina la kampuni anayofanyia kazi au anayomiliki na eneo ilipo kampuni hiyo,” amesema Dkt. Kiwia.

Ameongeza kuwa mwananchi anashauriwa kutuma taarifa hizo kwa barua pepe (fichua@heslb.go.tz); kutuma ujumbe wa WhatsApp (0739 66 55 33); kupiga simu kwenda 0736 66 55 33 kati ya saa 2:00 asubuhi hadi saa 10:00 jioni.

Njia nyingine ni pamoja na kutembelea tovuti www.heslb.go.tz na kuwasilisha taarifa kupitia kiunganishi cha ‘e-Mrejesho’. Pamoja na njia hizi, wananchi pia wanaweza kutuma ujumbe (DM – Direct Messages) kwenda Instagram, X (zamani Twitter) au Facebook kwa jina la ‘HESLB Tanzania’ LILILOTHIBITISHWA na lenye ‘blue tick’.

Maoni ya wadau-wanafunzi

Akizungumzia kampeni hiyo, Japhet Makyao, mwanafunzi wa mwaka wa tatu wa Shahada ya Udaktari na Upasuaji katika Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala – Tanzania (KIUT) ameipongeza HESLB kwa ubunifu huo na kuwataka wadaiwa sugu wenye vipato kurejesha.

“Ukweli ni kuwa, mimi hadi sasa hivi mwaka wa tatu, bila Bodi ya Mikopo, nisingeweza kufika hapa … ningependa kuona waliowezeshwa kusoma na wana kipato, wajitokeze ili vijana wengine kama mimi wanufaike,” amesema Japhet mara baada ya uzinduzi huo.

Kwa upande wake, Khadija Sultan, mwanafunzi wa mwaka pili, Shahada ya Usimamizi wa Biashara katika Chuo Kikuu cha Tumaini – Dar es salaam (DarTU) ameishukuru Serikali kwa kumuwezesha kusoma na kuwaomba wadaiwa kumaliza kurejesha mikopo yao.

“Mimi ni yatima, nimepoteza wazazi wangu wote wawili nikiwa bado mdogo sana, bila Serikali nisingeweza kusoma kabisa … hivyo ninawaomba wale ambao hawajaanza kurejesha, au wanaorejesha kwa wasiwasi kuanza kurejesha,” amesema Khadija.

Ni Nini maoni yako juu ya huu ujio wa fichua wadaiwa sugu wa HESLB.

View attachment 3028553
Shida hamjaweka dau
 
Uwe na siku njema.
Na we pia kaka.
Ila wajitahid kuweka mifumo mizur ili kuepusha loop holes kama hiz za matumiz mabaya ya pesa za umma kwa kigezo cha kutafuta wadeni wao.
Maana mwisho wa siku mnazundua kampeni za mamilion ili kurudisha pesa ambazo hamna uhakika kama kampeni hizo zitafanikiwa...
Mnazidi kutumia pesa ambazo hazikupaswa kutumika ndio maana wemgine tunaona ubadhirifu huu ni sawa na wizi tu
 
Hapa wangewatafuta Mana database wanayo wawasiliwane nao, Kama hawana kazi iwatafutie kazi ili wakate hela zao.
Mie nashangaa huko juu Kuna hela za Mana zinapigwa Ila hawaanzishi kampeni kuwa acheni wizi wa Kodi za wananchi ili vijana wasomee.
Waza Kuna mtu anakodi software kutoka India kwa bilioni 78 just kufuatilia umeme umekatika wapi..
Hatujawa serious na kusimamia Mali zetu kwa wachungu.
Kwanza mfano chai ikulu bajeti yake ni bilioni ngapi.

Hela tunazonunua magoli tungesomesha vijana wangapi may be.

Tuweni serious kufuatilia hela ambazo huwa cag anaibua jamani kuwa zimetumika vibaya hao watu wafukuzwe kazi,wafungwe, wengine wanyongwe, pia tuna miktaba Kama 200 ya ovyo tuiweke wazi tu renew iyo contracts kwa terms zenye manufaa na nchi yetu.
Mbona dp world walisemehewa Kodi na mktaba wa milele sijui kelele zikapugwa ndio ikakubalika walipe na hatujui Kama wanalipa.
So why na wasomi wasisamehewe hela Mana Kodi za ama pesa za watanzania na sio za mtu binafsi.
Naweza nikaandika mpaka kesho.kuna symbion, epa,iptl etc
 
Back
Top Bottom