Jana nimeshuhudia vurugu za kutisha mtaani wakati wa kilichodaiwa kuwa zoezi la kukamata pikipiki zinazodaiwa malipo ya SUMATRA. Hali ilikuwa ya kutisha baada ya bodaboda kuanza kurusha mawe ovyo na kuzua taharuki kwa wapita njia.
Bodaboda kisheria wanatakiwa kulipa kodi hiyo kila mwaka kwa SUMATRA, na wengi wamekuwa wakikwepa kulipa hivyo kuikosesha serikali mapato halali.
Bodaboda wanalalamika kuwa pikipiki zao zinapokamatwa hufanyika uporaji mkubwa wa vipuri huko SUMATRA, hivyo kuwaingiza kwenye gharama za ziada wanapotoka kukomboa mali zao.
Naishauri serikali kukusanya mapato haya ya SUMATRA kwa utaratibu kama ule wa EWURA. Wizara ya uchukuzi wakae pamoja na wizara ya Fedha kuona makadirio ya makusanyo kwa mwaka ni kiasi gani, waangalie pesa hiyo inaweza kupatikana kwa kuongeza senti ngapi kwa kila lita ya mafuta itakayouzwa (nasema senti nikiamini kwa mauzo ya mafuta ya mwaka hiyo bajeti ya SUMATRA itafikiwa bila tatizo).
Faida za utaratibu huu ni ugumu wa kukwepa kulipa kwa upande wa mlipaji, na urahisi wa ukusanyaji kwa serikali kuliko huu utaratibu wa kishamba wa kurushiana mawe mtaani na kusababisha usumbufu kwa wasiohusika.
Nawasilisha.