42_007
JF-Expert Member
- Mar 10, 2015
- 1,561
- 824
Asubuhi ndo njia yangu ya kwenda kazini...hesabu wanazopiga hawa boda boda kuvuka pale ni majanga matupu.Yaani hapo Shekilango ni majanga. Boda wanapitaga wrong mbele ya polisi na hawakamatwi. Mfano: Gari zinaoenda mjini hupita kushoto na yanayotoka kulia. Wao boda hupita kulia kwenda mjini. Tabia hii huhatarisha maisha ya watembea kwa miguu na vyombo vingine vya usafiri. Bodaboda wanajitanua service road za UDART japo zimechorwa baiskeli na watembea kwa miguu. Naomba waajiriwe Vijana wa kusimamia sheria barabarani wakae kila baada ya nusu kilometres ya barabara kuu. Mshahara wao utalipwa toka kwenye faini watakayolipishwa Wavunja sheria za barabara. Mbona huko USA Na Ulaya sheria za barabarani hufuatwa? Boda Na Bajaj ni kero ya mjini inayotakiwa kutatuliwa. Vyombo vya moto vifuaye sheria.