Bob Manson
JF-Expert Member
- May 16, 2021
- 4,291
- 8,200
Ni nani hasa anayeitwa Black Pope? Na kwa nini jina hili halijulikani sana kama la White Pope (Papa wa kawaida wa Vatican)?
Wengi hawajui kuwa ndani ya Kanisa Katoliki kuna mtu mwenye mamlaka makubwa, lakini ambaye haonekani hadharani, Jesuit Superior General.
Huyu si papa mweusi kwa maana ya rangi ya ngozi, bali ni cheo kinachomwelezea Jesuit General – kiongozi wa juu kabisa wa shirika la (Jesuits) ambalo ni mojawapo ya mashirika ya kidini ya kanisa katoliki lenye ushawishi mkubwa duniani.
Taasisi ya Jesuits na Black Pope wanahusishwa ya baadhi ya mambo yafuatayo:
Mamlaka Halisi ya Kanisa na Dunia
Black Pope ndiye mwenye mamlaka halisi ya Kanisa Katoliki, akimpita hata Papa Mweupe (anayejulikana zaidi). Inadaiwa kuwa Black Pope anadhibiti siasa, uchumi, na taasisi za kidini kwa siri kubwa huku akiwa nyuma ya kivuli cha mamlaka ya kiroho.
Kudhibiti Dunia (NWO)
Jesuits ni sehemu muhimu ya agenda hiyo, wakishirikiana na vikundi vingine vya siri, wanaonekana kama wasimamizi wa ajenda ya serikali moja ya dunia inayotawaliwa au itakayo tawaliwa na wachache walioko juu.
Historia ya Mapinduzi na Vita
Kulingana na baadhi ya vyanzo, Jesuits walihusika katika kupanga mapinduzi na vita kadhaa duniani mfano mapinduzi ya french revolution, vita vya dunia, na hata kuundwa kwa taasisi kama IMF, UN, na EU kwa ajili ya kufanikisha ajenda zao za udhibiti wa uchumi wa kidunia.
Ushawishi kwenye Elimu na Ujasusi
Mashule yanayo milikiwa au kuanzishwa na Jesuits yanasemekana kuwa vituo vya mafunzoya kipekee na nidhamu maradufu, ambapo viongozi wengi wa kisiasa na kifedha duniani wamepitia. Pia wana ushawishi mkubwa katika mashirika ya kijasusi kama CIA, na kuwa wanatumia elimu kama njia ya kueneza ajenda zao.
Mamlaka ya Kiroho ya Giza
Jesuits wanaaminika kuwa wanafanya ibada za siri, wakichanganya mafundisho ya kidini na mafumbo ya kale (occultism) wakitumia nguvu zisizoeleweka au kufahamika kwa watu wa kawaida na waumini walio wengi.
Binafsi nimefahamu yote haya baada ya kusoma kitabu hiki ambacho mambo yao mengi yameelezwa kwa kina.