Binti anataka kuharibu penzi la mama yake kwa baba aliyemlea tangu akiwa na miaka 7

Leo Rafiki yangu kanisimulia👇🏻

Jamaa anasema, kuna mwamba alioa mwanamke mwenye mtoto wa miaka saba, akamlea yule binti kiroho safi kabisa na kwa upendo japo si bintiye akamsomesha inshot huduma zote jamaa akawa anatoa.

Baadae yule mwanamke wakafanikiwa kupata watoto wengine, sasa yule binti wa kumlea akawa mkubwa akapata kazi nje ya Tanzania now ni mtu anajiweza amejenga mjengo wake lakini bado hajaolewa. Lakini sasa Baba wa huyu binti yupo hai ila alioa mwanamke mwingine na wote wanakaa sehemu moja.

Jamaa anasema, binti anataka kufanya kitu cha ajabu sana yaani anataka Mama yake aachane na huyu mwanaume aliyemlea toka yupo na miaka saba ili Mama yake eti aolewa na Baba yake, sijui unaelewa? Yaani eti yeye awaunganishe wazee wake wakati Baba yake alioa mwanamke mwingine na akazaa naye na Mama yake pia aliolewa na akazaa watoto wengine na huyu Baba aliyemlea binti.

Sasa sijui atatumia mbinu gani kuwauganisha, dunia ina viumbe sana hii.

Mambo ni mchanganyo sana 🙌🏾
Family matters
 
You never know,huenda huyo Bint alishakuwa na uhusiano wa kimapenzi muda mrefu na huyo baba yake wa kufikia.
Bint anataka kulipa fadhila za kusomeshwa mpaka akapata maisha hayo!
Hata hivyo wazo lake la kuwaunganisha tena Wazazi wake ni jambo jema.
Changamoto ni hao watoto wa baba (kwa mke mwingine) na watoto wa mama (kwa baba wa kufikia)!
Hapo kutakuwa na vurugu mechi.
 
Binti atafanikiwa kwa kuwa ana pesa, pesa ina ushawishi.

Je. mme wa huyo mama yake mzazi yuko wapi?

Kwa mm ningekuwa ndiye mama ya binti ningekataa. as there's nothing new under this world
 
Leo Rafiki yangu kanisimulia👇🏻

Jamaa anasema, kuna mwamba alioa mwanamke mwenye mtoto wa miaka saba, akamlea yule binti kiroho safi kabisa na kwa upendo japo si bintiye akamsomesha inshot huduma zote jamaa akawa anatoa.

Baadae yule mwanamke wakafanikiwa kupata watoto wengine, sasa yule binti wa kumlea akawa mkubwa akapata kazi nje ya Tanzania now ni mtu anajiweza amejenga mjengo wake lakini bado hajaolewa. Lakini sasa Baba wa huyu binti yupo hai ila alioa mwanamke mwingine na wote wanakaa sehemu moja.

Jamaa anasema, binti anataka kufanya kitu cha ajabu sana yaani anataka Mama yake aachane na huyu mwanaume aliyemlea toka yupo na miaka saba ili Mama yake eti aolewa na Baba yake, sijui unaelewa? Yaani eti yeye awaunganishe wazee wake wakati Baba yake alioa mwanamke mwingine na akazaa naye na Mama yake pia aliolewa na akazaa watoto wengine na huyu Baba aliyemlea binti.

Sasa sijui atatumia mbinu gani kuwauganisha, dunia ina viumbe sana hii.

Mambo ni mchanganyo sana 🙌🏾
Wanawake ni makatili zaidi ya shetani mwenyewe
 
Dunia imebadilika sku zote wekeza kwenye chako hawa watoto wa wengne unajitia msamalia unalea unatunza badae anakuja kukugeuka na kua chanzo cha migogoro na mafarakano ktk familia
 
anajiangalia yeye tu, haoni kwamba kuwaunganisha wazazi wake atakuwa anawadhurumu wadogo zake haki ya malezi ya baba na mama

anataka yeye ndo awe na baba na mama wengine walelewe na mama/baba tu

pumbavu zake
 
huyo mama ndo hana akili.
Mtoto wako anakuamriaje mambo ?
So akute amelelewa na baba mwingine toka ana miaka 7, leo anaweza mpk kujenga nyumba, enheee si ni ndoa ya miaka zaiid ya 15 au 20 hiyo.

UNAWAZAJE HATA KUWAZA eti wazazi wako wavunje ndoa zao ili uwaunganishe?
MXXXIE
 
Back
Top Bottom