Binafsi siwezi kuishi na mtu anayeenda kwa Waganga wa kienyeji na Mchawi

Nakuunga mkono asilimia mia,kaka epuka dada anayependa ushirikina mara ana tudawa amechanganya na mafuta kimbia,kuna siku atakulisha nyama ya bundi.
Dada chunguza vizuri familia unayotaka kuolewa usije ukaolewa kwa washirikina,wanao wanaweza kufanyiwa kitu siyo.
Namshukuru mama yangu na shangazi yangu nilipowambia nimepata mchumba waliniambia kwa msisitizo niwe makini,niijue familia nakotaka kuingia nisije olewa familia ya wachawi ama washirikina.
N.B
Happy 30 years kaoe sasa
 
Habari Wakuu!

Watibeli ni bora tufe lakini kamwe hatuwezi kuwafuata waganga au wachawi. Ushirikina na uchawi kwetu ni kama kosa la Mauaji, au kosa la usaliti.

Binafsi siwezi ishi na mtu ambaye anapenda mambo ya kishirikina, anaenda kwa waganga, au anadalili za uchawi uchawi.

Mke akijihusisha kwa namna yoyote na mambo ya ushirikina au uchawi iwe kwa kusema mdomoni, kushauri, au kwenda na kuutumia uchawi au uganga huyo kwetu Watibeli tunafukuza bila kumsikiliza yeyote.

Kwa binti zetu, binti za Tibeli kamwe hatamvumilia mwanaume aliyemuoa ikiwa atagundua ni mshirikina, mchawi au anapenda mambo ya waganga.

Binti yangu, ikiwa mumeo ikatokea siku akatamka hata kwa utani kuwa uchawi au ushirikina kuna muda unasaidia. Mimi Baba yako ninakuruhusu umuache siku hiyohiyo pasipo kufikiri wala kusubiri.

Mtibeli acha nipumzike.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam

.
Mtu anayewaza ushirikina au waganga ni kipimo namba moja cha Umasikini.
Tupo mbali sana kwa sasa kimaendeleo ya kiteknolojia kuwaza mambo kama hayo
 
Nakuunga mkono asilimia mia,kaka epuka dada anayependa ushirikina mara ana tudawa amechanganya na mafuta kimbia,kuna siku atakulisha nyama ya bundi.
Dada chunguza vizuri familia unayotaka kuolewa usije ukaolewa kwa washirikina,wanao wanaweza kufanyiwa kitu siyo.
Namshukuru mama yangu na shangazi yangu nilipowambia nimepata mchumba waliniambia kwa msisitizo niwe makini,niijue familia nakotaka kuingia nisije olewa familia ya wachawi ama washirikina.
N.B
Happy 30 years kaoe sasa

Ahsante sana Mkuu kwa kunitakia kheri ya kuzaliwa.

Usiombe ukajikuta kwenye familia za washirikina, hakika utakuwa mtu asiye na bahati. Sio kwa mume au kwa mke. Yeyote kwenye familia akishakuwa na mambo ya kishirikina familia hiyo ipo kwenye shida kubwa.

Watibeli kuoa/kuolewa ni lazima sio hiyari. Labda mtu afariki akiwa mdogo lakini kama amefikisha miaka 40 lazima awe ameshaoa/ olewa
 
Sasa mbona ndoa nyingi zitavunjika, hivi kuna wanaume ambao sio washirikina bongo hii??
Hawa wenye chale mpk kwenye mstari wa pumbunyo!!! Labda useme mataifa ya magharibi huko

Hapahapa Tanzania wapo maelfu ya vijana ambao hata kwa mganga hawapajui, pia hawaamini katika Uchawi na ushirikina.

Ingawaje kama ulivyosema wanaoamini ni wengi zaidi.
 
Ukitafuta wachawi kwenye maisha yako utakutana nao mpaka uchanganyikiwe na ukitafuta watu wema utakutana nao sana Its all about mindset

Sio kila ulichonacho kwenye maisha ulikitafuta.
Nakubaliana na wewe kuwa yapo mambo ambayo unaweza kuyaset kupitia akili yako (minset) lakini kwenye maisha mambo mengi hutokea Kwa nasíbu (by chance).

Unaweza ukawa hutaki kuoa au kuolewa na Mchawi au mshirikina lakini ukapata mshirikina au mchawi pasipo wewe kujua.
Au mwenza wako akaja kubadilika akapenda hayo mambo huko mbeleni.
 
Hapahapa Tanzania wapo maelfu ya vijana ambao hata kwa mganga hawapajui, pia hawaamini katika Uchawi na ushirikina.

Ingawaje kama ulivyosema wanaoamini ni wengi zaidi.
Labda wavuta bangi wale wanaosema “ Uchawi hauendi kwa mentali” ila hawa wengine tunapishana nao sana kwenye vilinge 😂😂😂😂
 
Back
Top Bottom