Binafsi siwezi kuishi na mtu anayeenda kwa Waganga wa kienyeji na Mchawi

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
25,673
61,699
Habari Wakuu!

Watibeli ni bora tufe lakini kamwe hatuwezi kuwafuata waganga au wachawi. Ushirikina na uchawi kwetu ni kama kosa la mauaji, au kosa la usaliti.

Binafsi siwezi ishi na mtu ambaye anapenda mambo ya kishirikina, anaenda kwa waganga, au anadalili za uchawi uchawi.

Mke akijihusisha kwa namna yoyote na mambo ya ushirikina au uchawi iwe kwa kusema mdomoni, kushauri, au kwenda na kuutumia uchawi au uganga huyo kwetu Watibeli tunafukuza bila kumsikiliza yeyote.

Kwa binti zetu, binti za Tibeli kamwe hatamvumilia mwanaume aliyemuoa ikiwa atagundua ni mshirikina, mchawi au anapenda mambo ya waganga.

Binti yangu, ikiwa mumeo ikatokea siku akatamka hata kwa utani kuwa uchawi au ushirikina kuna muda unasaidia. Mimi Baba yako ninakuruhusu umuache siku hiyohiyo pasipo kufikiri wala kusubiri.

Mtibeli acha nipumzike.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam

.
 
Ni vigumu sana kwa Tanzania hii kupata mwenza asiyeamini hayo mambo!

Na hiyo ndio tafsiri kuwa ni vigumu kwa ndoa za Tanzania kuwa na furaha na utulivu.
Kwa sababu Washirikina na wachawi kikawaida hawanaga furaha na utulivu.

Akiona chura anawaza ujingaujinga wake.
Akiona kilele kimemwota anawaza Uchawi.

Akiona mumewe hahudumii familia alafu anamchepuko anawaza ati mchepuko kamuwekea madawa jambo ambalo ni uongo.
 
Back
Top Bottom