Mkuu Dawasco ni zaidi ya wanaharamu..wanakata maji kwa deni elfu 20 afu kurudisha maji uwalipe elfu 30 ..Juzi nililipa nikaunga mwenyewe wakaja juu nikawapiga mkwara wakapotea washenzi sana wale.Kukata maji wamefanya ndio mradiGharama ya kurudishiwa maji ya 30,000/= ni kubwa mno kwa sababu hakuna kazi yeyote inayofanyika zaidi ya kuchomoa kitufe baada ya kuzungusha koki kufunga maji na kurudisha maji ni vivyo hivyo kuchomeka kitufe na kuzungusha kulia kufungua maji.Ujambazi sio lazima umkabe mtu koromeo umpore mali yake lakini huu mtego wa panya wa kutuma bili katikati ya mwezi kwa lengo la kulipwa reconnection fee ya maji sh. 30,000 ni ujambazi uliovuka mpaka.Hata kama watarudisha gharama ya zamani ya sh.15,000 bado kubwa tu.Kuzunguka na kitufe cha kunyongea koki kufunga na kufungua maji sio kazi inayolingana na pesa wanazolipwa.Meneja wa Dawasco wa kipindi hiki kweli ni kiboko anaijua hela kuliko watu wote.
Ukiona hivyo ujue hizo kazi walipeana kindugu.. Hakuna aliyesota..Dawasco ni jipu !! Niliwaacha wakate tu maji, call centre yao majanga !! Haina msaada wowote.
Ukiwa upo zako Tandale akusubiri urudi ndio akusomee mita yako hana wateja wengine? Au unataka akufuate usiku?. Cha muhimu fahamu kuwa natumia maji ya watu na natakiwa kulipa kila mwezi, hivyo natakiwa kutenga some amount ya maji yao, based on your average monthly consumption hawatakusumbua kabisa.Mkuu ni kweli pia walete utaratibu msomaji bili anapokuja soma awepo either muhusika kuhakiki kinachosomwa na kinacholetwa kama bili
Unataka wewe wakuache ujiandae kulipa, ila maji yao wewe unayatumia tu, lipeni bills za watu.Sio lazima uwazungikie wote tarehe 30 halafu uwapelekee bili kesho yake, unaanza mapema na hata ukipeleka bili katikati ya mwezi sawa lakini usubiri na yeye ajiandae akulipe mwisho wa mwezi, sio kukata maji ovyo kama kukomoana.
Hiyo walishindwa wamerudia kizamani wanasoma kisha wanatuma meseji,Yaani DAWASCO ni jipu la hovyo kabisa,wanachofanya sicho kabisa.Wanakera sana.Bora uletwe utaratibu wa prepaid kama luku.Wanalazimisha sh 30,000 za wizi halafu hizo pesa unaambiwa ukalipie crdb siyo kwa maxmalipo,au mpesa au airtel money kisa ni account tofauti ya kufanyia wiziSiku hizi wanatembea na mashine kama za efd au max malipo, wanasoma na kuprint bili hapo hapo. Hawajajipanda tu vizuri
Hapa inatakiwa wateja tuandamane kwa waziri hakuna jinsiGharama ya kurudishiwa maji ya 30,000/= ni kubwa mno kwa sababu hakuna kazi yeyote inayofanyika zaidi ya kuchomoa kitufe baada ya kuzungusha koki kufunga maji na kurudisha maji ni vivyo hivyo kuchomeka kitufe na kuzungusha kulia kufungua maji.Ujambazi sio lazima umkabe mtu koromeo umpore mali yake lakini huu mtego wa panya wa kutuma bili katikati ya mwezi kwa lengo la kulipwa reconnection fee ya maji sh. 30,000 ni ujambazi uliovuka mpaka.Hata kama watarudisha gharama ya zamani ya sh.15,000 bado kubwa tu.Kuzunguka na kitufe cha kunyongea koki kufunga na kufungua maji sio kazi inayolingana na pesa wanazolipwa.Meneja wa Dawasco wa kipindi hiki kweli ni kiboko anaijua hela kuliko watu wote.
King'amuzi cha dstv, Zuku, startimes unalipia kiasi gani? unit 1 ya maji nadhani ni shs. 1,119 ambayo ni sawa na tank la lita 1,000. Sasa ukijikuta unashindwa kulipia maji ya shs.30,000 basi jaribu ku opt kutumia maji ya matorori na bozza uone raha yake. Ninadhani Dawasco ndio wenye rate kubwa ya maji kuliko mamlaka zingine za maji.Matatizo ya bill za maji yamekuwa yakilalamikiwa na wateja mara nyingi na hakuna ufumbuzi wowote unaopatikana.Seikali ya awamu ya tano imedhamiria kuwapunguzia matatizo na kero zilizowatesa kwa kipindi kirefu.Tanesco wameshusha bei ya umeme na kuondoa service charge,serkali imeondoa karo mashuleni,wizara ya afya matibabu bure bila kuchangia gharama zozote kwa watoto,waja wazito, wazee na watoto.Sasa wizara ya maji nayo inapaswa kuingilia kati kuwapunguzia Watanzania kero za maji.Haingii akilini mtu amekatiwa maji kwa kushindwa kulipa bili ya sh.8,000 halafu anapigwa faini ya sh 30,000 ya reconnection.Mimi mwenyewe nimewahi kupigwa faini hiyo baada ya kukatiwa maji kwa bili ya sh.12,000.Waziri mqenye dhamana na hii Dawasco anatakiwa aingilie kati sasa kwa sababu maji ni muhimu zaidi kuliko umeme na shule.Binadamu hawezi kufa kwa kukosa umeme au masomo.LAKINI MAJI NDIO UHAI WENYEWE, viumbe hai vyote vikikosa maji vitateketea vyote.