Bilioni 20 alizotoa mwekezaji MO Dewji kwenye club ya simba ni changa la macho?

msovero

JF-Expert Member
Jun 30, 2019
863
1,531
Nimefuatilia kwa ukaribu mahojiano ya mwenyekiti mpya wa bodi ya club ya simba bw. Salum Abdallah katika kipindi cha sports HQ kinachorushwa na kituo cha redio cha E-fm, nimegundua kuna ukanjanja mkubwa kuhusu bilioni 20 alizotoa mwekezaji Mo Dewji katika club yake hiyo ya simba.

Kama mtakumbuka siku Mo dewji ameitisha mkutano na waandishi wa habari 'press conference' kukabidhi kitita hicho cha pesa aliwatolea uvivu na kuwashukia vikali wale wote waliokuwa wanasema kuwa hana pesa.

Katika kuwathibitishia kwamba anazo, mwekezaji Mo Dewji alisema maneno machache yafuatayo, nanukuu "Lakini kuna watu wanasema Mohammed Dewji hana pesa, leo hii nakabidhi cheki ya Sh 20 Bilioni za hisa asilimia 49 kwa klabu ya Simba," hivyo Mo dewji alithibitisha kwamba ana pesa kwa kuonyesha checki hiyo yenye thamani ya bilioni 20 za kitanzania kama malipo ya 49% ya hisa alizowekeza katika club ya simba.

Lakini katika hali isiyo ya kawaida katika mahojiano ya jana, mwenyekiti mpya wa simba bw. Salum abdallah "Mr Try again" alikanusha vikali kwamba mwekezaji Mo dewji hakutoa cheki bali alitoa Transaction notes. Sasa kwa kuanzia ili kupata undani na ukweli wa hizo bilioni 20 tujiulize ni kwanini watu hawa wawili kauli zao zina kinzana? Mwingine anasema ni cheki, mwingine anasema ni transaction notes, je ukweli kuhusu hili ni upi?

Kuhusu benki kilipowekwa kiasi hicho cha pesa, mwenyekiti anasema pesa zimewekwa kwenye akaunti maalum ila hataji jina la benki kwa mdai kuwa ndivyo walivyokubaliana. Je, hayo makubaliano ya kutotaja jina la benki ni kati ya nani na nani? Mwekezaji na benki au mwekezaji na uongozi wa club? Je, kwanini benki kilipowekwa kiasi inafanywa kuwa siri? Nani ana monitor hiyo akaunti maalum kilipowekwa kiasi hicho cha pesa? Kwanini kiasi hicho cha pesa kiliwekwa kwenye akaunti maalum na sio akaunti za kawaida za club ya simba?

Hatahivyo, kupitia jicho langu la tatu la kimchezo nimegundua kuna changa la macho katika hizo bilioni 20 zilizotolewa na mwekezaji 'Mo'.

kwakuwa amesoma upepo wa club katika msimu huu kuwa sio mzuri ameona ajivue mapema uenyekiti na kumwachia swahiba wake amtunzie siri ili ukanjanja huu usibumbuluke kwani kama simba ikiendelea kufanya vibaya uwanjani, mashabiki na wanachama watataka kujua mapato na matumizi ya club hasa kujua matumizi ya hizo bilioni 20 hewa alizozitoa mwekezaji kanjanja 'Mo' na kama itatokea wanachama wakahoji matumizi ya hizo bilioni 'hewa' ndio utakuwa mwanzo wa mwekezaji huyo kanjanja kutangaza kujiuzulu kuwa mwekezaji wa club hiyo. MUDA UTASEMA...
 
Sasa club inajiendeshaje mdau maana pesa za wadhamini hazitoshi hata kidogo
 
Kwani huko.uto jezi.timu inapata shilingi ngapi ..?.
 
Mo alidai anaendesha club ya simba kwa hasara ,ila kiukweli jamaa anapiga pesa nyingi hapo simba 49% ni pesa nyingi mno
 
Hawana majibu labda wataishia kunitukana tu ndicho wanachoweza
Hivi wewe kwarukwaru pale simba unachochote ulichowahi kuchangia, hata kununua tu kibendera!?
Hizo pesa hata zisipowekwa wewe inakuhusu nini!?
Tuseme Mo hajatoa kitu, then nenda wewe ukatoe hizo hela sasa upewe timu!
Moja wapo ya dalili za kuwa shoga ni umbea hasa ukiwa mwanaume nisaidieni nyingine ili nijue
Naona mtoa mada umeshaanza kupata majibu kutoka kwa wenye Moo wao. Hatari sana.
 
Wanataka kujua benki iliyopokea hundi ya bilioni 20 kutoka kwa mwekezaji kanjanja 'Mo' kwanini inafanywa siri? Kitu gani kinafichwa?
Nenda makao makuu ya club pamoja na kadi yako ya uanachama utapewa muongozo pesa zimeweka benki gani
Ila huku mtandanoni tutazidi kusokomeza ndani huo mwiko ulioko nyuma
 
Back
Top Bottom