Betting sio biashara halali

Mtoa mada utakuwa umeliwa sana kwa kubet hovyo hovyo mpaka umegeuka kuwa mwanaharakati. Me siwezi kuacha kubet kabisa aisee, na ikitokea serikali imezuia huu mchezo, naweza kuhama kwenda kuishi nchi ambayo mchezo huu upo.

Sijawahi kufanya biashara inayonipatia faida nyingi kama hii ktk maisha yangu. Me daily huwa natafuta 1.60 or 1.80 ya odds, naweka milioni moja, naondoka zangu. Nna mwezi wa kumi sasa mfululizo napata faida ya kati ya laki nne mpaka laki sita kila siku kwa mtaji wangu huo wa milioni moja.

Nakushangaa sana unavyoeneza uongo huo wa uharamu. Ni bora kwenye kujenga hoja yako labda ungetuhusia kiimani/kiroho walau ungetushawishi kwa kumuhofia mungu wetu.
...ngoja kwanza,
..kwamba ndani ya miezi hiyo 10 umetengeneza faida si chini ya milioni 120;
.....kwanini hujaongeza mtaji ili upate zaidi
 
Hawa ndo wale wa jero jero then wanataka milioni kumi
 
Biashara ni biashara iwe na faida au hasara. Mfano kuna faida gani ya kuuza cigarettes na pombe. Lakini ni biashara
 
Kitu haramu hakiwezi pewa leseni
Kama wamepewa leseni maana yake ni halali, na inalipa kodi.
Afu fata mambo yako
 
Kwa wale wote wanaotetea Beting kama BIASHARA HALALI, nasema siyo. Na haijalishi kama serikali imeruhusu au la, swala ni kwamba hii siyo biashara halali kwa sababu zifuatazo;
www.amkamtanzania.com
Sijajuwa kama ni wizi, maana hizi kampuni zimesajiliwa na zina leseni. Ila sijaona tofauti kati ya ku bet na kununua na kuuza hisa?! Maana zote zinaendana, kuuza na kununua hisa wadau huafuatilia bei za mazao, kampuni, bidhaa n.k. Sawa na betting! Wakifuta betting basi wafute uuzaji na ununuaji wa hisa aise..
 
Upo sahihi kabisa , Betting inaweza pia kua Kichaka cha wahalifu kujificha . Namuomba mr Makonda aliangalie Hili
 
Nashukuru huu mchezo hata siujui ila nawaona watu wanajazana kwenye chumba na kubeba makaratasi tu.
Kweli unafanya vijana wawe wavivu wa kufanya kazi.
 
...ngoja kwanza,
..kwamba ndani ya miezi hiyo 10 umetengeneza faida si chini ya milioni 120;
.....kwanini hujaongeza mtaji ili upate zaidi
Nakiri kuwa matumizi yangu ya fedha ndio sio mazuri. Nipo Dar sasa ni mwezi wa nane, nipo naishi hotel na natumia gari ya kukodi. Matumizi yangu binafsi kwa siku moja si chini ya laki mbili, mpaka mbili na nusu.

Najipanga vema kwa msimu ujao, ntakuwa nimepata apartment na ntakuwa nimenunua gari yangu. Hapo ndio ntaongeza mtaji mkubwa. Naplan kuwa ntapata si chini ya milioni mbili kwa siku, maana ntaanza kuweka milioni tano kwa odds zilezile (1.60/1.80). Betting inaweza kuwa ndio mkombozi wa maisha yangu aiseee....
 
Tuachie mtaji wetu, serikali yenyewe inabana ajira so kubet ni lazima. Naona unanimalizia mb zangu Bure kwa hili bandiko lako.
 
MATAJIRI NA WAFANYABIASHARA WOTE DUNIANI WANACHEZA HUU MCHEZO IWEJE MASKINI KAMA WEWE UJE UTOE PUMBA
 
Ni kweli kabisa,
Ila wao wanacheza kama sehemu ya burudani, na siyo mkakati wa kupata fedha, kama ambavyo vijana wengi wa kitanzania wanajidanganyw.
Unakuta mtu ana elfu 2 anapanga kwenda kubet apate elfu 20 ya kuendesha maisha yake, huu ndiyo ujinga unaoumiza vijana wengi.
Hao sasa ni elimu yakuelewa mambo ndio maana ukaitwa mchezo na sio kitu kingine.
 
Hawa ndo wale wa jero jero then wanataka milioni kumi
Inaweza kuwa hvyo. Hzo ni crazy betting, hata me huwa nacheza ticket unaweka elfu 2, ikipita ni milioni tano au saba. Ni ngumu sana huwa ni kubahatisha tu. Sure betting ndio kama nilivyosema hapo awali. Weka elfu moja upate elfu moja na mia nne au na mia tano. Nakuhakikishia utakula daily..
 
Back
Top Bottom