hahahah jamani si mlikuwa mnasema anawaponda ccm.Vasco da Gama bonge la mnafki naona anajikosha tu hapo star tv.anaNyemelea ubalozi ambao dokta Pombe hawezi hata kumpa.najiskia kichefuchefu nitarudi akimaliza kuongea
Pamoja na Mwalimu kujenga heshima ya chama, CCM now sheeda siyo nyumbani siyo mataifa ya juu . CCM imepoteza mwelekeo.
mwacheni azungumze makamanda. tatizo lenu mnataka kusikia habari zinazowa favor tu. zikiwa opposite mnakasirika. huu ni upumbaf na ulofa mmeshaambiwaMembe ameonekana kuzungumza kana kwamba amelazimshwa na chama chake kufanya navyo.Kwa kumuangalia nimeona akiwa anajaribu kukitetea chama hili kisionekane kina mkwaruzano.
Yote juu ya yote ajapinga kile ambacho gazeti la Mwananchi limeandika kumuhusu.Ameishia kuwakejeli watu anayewaita,kwa maneno
yake"wanafiki".Kwa maana hawakumuunga mkono Magu tangu awali,ila alipoukwaa urais wanajotokeza na kuanza kujinasibu kumuunga mkono.Hili ni dongo kwa Bashe.
Kilichonisikitisha kutoka kwake aliposema:mwana ccm yoyote anayekihama chama hapaswi kuruhusiwa kurejea tena,na anapokivua nguo chama huko pia ashughulikiwe huko huko.Akitolea mfano wa jinsi chama cha ANC SouthAfrica kilivyokuja na sera ya "gate valve" kwa wale wanaotoka na kuhamia vyama mbadala kutoruhusiwa kuwa wanachama wa chama hicho,pale wanapojisikia kufanya hivyo.
Membe amejidharirisha kuomba mahojiano maalumu kuonyesha alivyosurrender pressure kutoka kwenye chama chake.
Tatizo anaogopa kufunguka kwa baadhi ya mambo na anabaki kujikanyagakanyaga tu.
ukishakuwa mwafrika unakuwa na sifa za kila aina, moja hatusimamii tunachoamino, leo unasema hiki, kesho unakanaa kama sio ww.Ni kweli Mkuu nimemuona Membe amejichanganya sana.
Amesema wazi kuwa ufutwaji wa matokeo yote huko Zanzibar kumeishangaza dunia, hasa ukitilia maanani kuwa uchaguzi ule ulikuwa na waangalizi toka Marekani, Jumuiya ya Ulaya, African Union na SADC na waangalizi wote hao walitoa taarifa zao kuwa uchaguzi ule ulikuwa huru na haki, kwa hiyo walishangazwa mno na uchaguzi ule kufutwa wote.
Hapo hapo Membe anajicontradict mwenyewe kwa kusema ili mradi Jecha keshatangaza tarehe ya marejeo ya uchaguzi huo tarehe 20/03/2016 kwa hiyo anavisihi vyama vyote vishiriki uchaguzi wa marejeo!!!
Hakika kutokana na kauli hizo za Membe nimeamini kuwa almost 100 percent ya wanaccm ni wanafiki waliobobea!
umeangalia Tv gani? Unachofikiria ni tofauti na alichoongea Membe Star Tv, bavicha hamfai kabisa kuwa source ya habari.Naona Star TV sasa inaanza kutumika kumbomoa Magufuli kama wakati ule ilivyotumika usiku na mchana kumpigia kampeni. Nadhani Dialo amesubiri sana fadhila kutoka kwa Magufuli kaona hakuna dalili sasa kageukia upande mwingine.
Tatizo wewe point hujazisikia, ubongo wako na kila kitu kinachotengeneza mfumo wako wa fahamu kilikuwa kinaacha point zipite na kulazimisha hizo point ziwe pumba.Yaani huyo Membe ameongea pumba tupu hapo Star TV.
Wakati huo huo anasema dunia inashangaa inakuwaje Jecha afute hadi matokeo ya walioshinda nafasi ya uwakilishi hadi kupewa vyeti vya ushindi huo na wasimamizi wa uchaguzi huo.
Lakini hapo hapo anaendelea kusisitiza kuwa wanaccm wakusanye nguvu huko Zanzibar ili kufanya kampeni ya nguvu ili wapate ushindi wa kishindo wakati huyo Jecha wao tayari kwenye tangazo lake amepiga STOP kampeni zozote kwenye uchaguzi wa marejeo.
Tatizo sio mtu kuwa na double standard, tatizo ni ufinyu wa upeo wa kufikiri wa bavicha, kila kitu wana twist ili wakipende.ukishakuwa mwafrika unakuwa na sifa za kila aina, moja hatusimamii tunachoamino, leo unasema hiki, kesho unakanaa kama sio ww.
Double standard hizi zipo africa tu
Wanatushangaa na sisi tunaendelea kuwashangaza. Ona ulichokiandika halafu angalia ulivyo na jeuri ya kutusi mwenzio.Tatizo wewe point hujazisikia, ubongo wako na kila kitu kinachotengeneza mfumo wako wa fahamu kilikuwa kinaacha point zipite na kulazimisha hizo point ziwe pumba.
Sasa ni nini haujamuelewa?? Kasema dunia ilishangaa sio kufutwa kwa uchaguzi, ufutwaji wa uchaguzi umewahi kutokea, dunia imeshangaa kwa nini UFUTWE UCHAGUZI WOTE NA SIO KULE AMBAKO MATOKEO YALIKUWA NA KASORO??
Bavicha msifosi mambo yawe upande wenu, tumieni na akili aliyowapa Mungu ya kuzaliwa tu inatosha kudadavua haya mambo, sio lazima ufike hata la nne. Ni akili ya kuzaliwa tu.