Benard Membe: Musiba hasimami tena na kujifanya yeye ni Mungu Mtu. Huko uliko naomba hela zangu

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
1,665
8,805
“Niwaambie Watanzania wenzangu hakuna Mtanzania awe Ndovu au sisimizi mwenye kusimama juu ya sheria hakuna aliye juu ya sheria, ukimdhalilisha mwenzako ukadhani kwamba utaendelea kupiga miluzi na kufurahia kana kwamba wewe umefika Duniani kama Kiongozi au ndio mkubwa au Mungu Mtu, Mahakama Kuu ni jibu kwamba ukidhalilishwa fika Mahakamani uitafute haki yako nimefika hapa kwa niaba ya watanzania wote na Viongozi Wastaafu walionyanyaswa na kudhalilishwa na Mtu huyu"

"Naomba wajue hili halitotokea tena, hasimami tena kudhalilisha Wazee na Viongozi wake, hasimami tena na kujifanya yeye ni Mungu Mtu, hasimami tena kuwatukana Watu walioifanyia kazi Nchi hii kwa uaminifu na uadilifu wote, anasimama Mtu kwa kutumwa na kulipwa akadhani kwamba ataendelea kuishi Duniani katika hali hiyo hamtomuona tena akifanya hivyo na Musiba huko uliko naomba hela zangu"

Bernard Membe

Pia, soma=> Mahakama yaamuru Cyprian Musiba kulipa faini ya Tsh bilioni 6 kwa kumchafua Bernard Membe
 
Mzee msamehe kijana alikuwa anatafuta maisha.

Ajira wakuu hawakutoa kila mtu alibuni njia zake za kujipatia kipato wengine tuliamuaga kuwa wamachinga hata sisi tunahama tu taratibu kwa amri ya serikali sikivu ya mama yetu Mh Samia.

Ukimsaheme utajiongezea thawabu.
 
Ila linaweza kukunyang'anya nyumba yako kukufanya uishi kwa wasiwasi ukihofia udhalili na mengine kama hayo. Kifupi deni halifungi kwa maana ya selo ila kifungo chake moyoni ni kibaya sana
Musiba hana hela, kwa hiyo kwanza watafirisi mali yake kwenye kesi moja tu ya Fatma, ukiongeza na hii ya Membe ataonekana hatekelezi amri ya mahakama, hapo sasa ndio atafungwa.
 
Back
Top Bottom