Beki wa Yanga Ibrahim Bacca apandishwa Cheo Jeshini, sasa ni Sajenti

Waufukweni

JF-Expert Member
May 16, 2024
2,498
7,060
Kikosi Maalumu cha Kuzuia Magendo Zanzibar (KMKM), kimempandisha cheo nyota wa timu ya Yanga SC, Ibrahim Hamad “Ibra Bacca” kutoka Koplo na kuwa Sajenti kutokana na kuonesha kiwango bora kwenye mchezo wa soka.

"Sina budi kushukuru kikosi changu kwa kuweza kunisapoti kwa kila hatua. Nitaendelea kuipambania nchi yangu," amesema Sajenti Ibrahim Bacca ambaye wazazi wake pia ni askari.

1742223304319.png
KMKM iliyomwachia Bacca kuitumikia Yanga, ni kikosi cha ulinzi cha Zanzibar ambacho kina jukumu la kulinda mipaka ya bahari dhidi ya magendo, uvuvi haramu, na vitendo vingine vya kihalifu. Pia, KMKM husaidia katika operesheni za uokoaji baharini na usalama wa majini.

 
Huyo Mkuu wa kikosi chake aliyempandisha cheo angekuwa huku bara angeambiwa ni shabiki wa Yanga.

Bacca anajituma sana, yeyote anayependa mpira bila hisia za ushabiki atakiri hilo.

Pongezi nyingi kwake, ikawe chachu katika majukumu yake.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom