Bei za chakula kwenye migahawa yanaposimama mabasi ya mikoani ziko juu sana

Dah mi hua naahirisha kula kabsaa, ila njia ya Dom-Chuga pale Babati chakula buku 2-3, Though ukizuga na vibiscuit unafika fresh tu kama tumbo lako halipitishi hewa ovyo.
 
Suluhisho ni usafiri na chakula chako.
Inategemea unaenda wapi
e2a0c2db9585d0433aa7a68e1b6a3fc7.jpg

ef05debea1a2f7455f9a7fc2d116b811.jpg
 
Daah hongera kwa hii post mkuu! Mwezi Wa nne nilipanda basi linaitwa Leo express wakasimama Dodoma! Yaani chakula cha mahali pale ni hovyo!! Na wahudumu Wa ule mgahawa ni jeuri, unataka kula hutaki acha! Bei 5000 hicho chakula daah Mungu nisaidie. Niliumwa tumbo sio mchezo. Wakati nikirudi May nikabadirisha Na kupanda Isamilo nikijua itakuwa afadhari nilichokikuta hapo, singida ndo hata usiseme chakula kibichi ukitaka kula hutaki acha. Wanachoangalia ni pesa yao tu..... Nadhani kuna umuhimu Wa wizara ya Afya Na watu Wa biashara kupitia maeneo haya.! Hebu fikiri basi moja lina abiria 60, je mabasi mangapi wanapata Huduma ya chakula kila Siku kwa maeneo walipo? Pato lao ni zaidi ya wafanya biashara Wa aina hiyo kwa maeneo mengine.
 
Aiseee hii issue ni balaa..pls iangaliwe soon as possible...madereva kuhongwa hela isiwe chanzo.cha kunyanyasa abiria....ebo
 
Hii nakubaliana na wewe mkuu, hawa wanafanyia biashara mazoea. No service improvement miaka nenda rudi
Hii njia ya Mbeya hayo ma-motel ni machafu balaa kuanzia aljazeera hadi kitonga,halafu bei za kipumbafu,unfair to fellow wananchi
 
Mombo kuna uharisia wa bei lkn singida na Dodoma kwanza wachafu alf vyakula vya hovyo bei juu... cku iz nikisafiri natoka nisha kula nakunywa maji na korosho tu basi
 
Njia ya mwanza dar na mbeya dar kwa upande wa chakula ni aibu sana,mpaka vyoo ni hovyo kabisa,nilichogundua ukiingia sehemu ya kula kama unasafiri ukiingia chooni ndio unapata picha,kama vyoo ni visafi hata chakula kitakuwa kizuri, chooni pakiwa ovyo usithubutu kabisa kwenda kwenye chakula,hasira itazidi mara mbili
 
Daah hongera kwa hii post mkuu! Mwezi Wa nne nilipanda basi linaitwa Leo express wakasimama Dodoma! Yaani chakula cha mahali pale ni hovyo!! Na wahudumu Wa ule mgahawa ni jeuri, unataka kula hutaki acha! Bei 5000 hicho chakula daah Mungu nisaidie. Niliumwa tumbo sio mchezo. Wakati nikirudi May nikabadirisha Na kupanda Isamilo nikijua itakuwa afadhari nilichokikuta hapo, singida ndo hata usiseme chakula kibichi ukitaka kula hutaki acha. Wanachoangalia ni pesa yao tu..... Nadhani kuna umuhimu Wa wizara ya Afya Na watu Wa biashara kupitia maeneo haya.! Hebu fikiri basi moja lina abiria 60, je mabasi mangapi wanapata Huduma ya chakula kila Siku kwa maeneo walipo? Pato lao ni zaidi ya wafanya biashara Wa aina hiyo kwa maeneo mengine.
Mmi bado nalia na TRA na TAKUKURU na WIZARA YA AFYA wote kwa pamoja waliangaloe hiliswala. Unakuta sambua ya mia mbili mtaani unauziwa elfu 2000. Inashangaza sana aisee
 
Hili ni janga kubwa kuzidi hata Lugumi kwa kuwa linamgusa kila mmoja ila nani wa kulikemea? Juzi nimetoka Tabora kuja mjini kupitia njia ya Itigi nafika Dodoma kwanza chakula ni kibichi halafu bei ndo 5000 plus na isitoshe vinywaji esp bia take away tayari muda umeshakwisha wa matumizi kuanzia February...nadhani Serikali itafanya ziara ya kustukiza kama ada!
 
Back
Top Bottom