BBC: Mapinduzi ya mafuta Tanzania yamekwama kutokana na ukosefu wa vituo vya mafuta

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
2,201
5,584
Mapinduzi ya nishati ya magari yanazidi kushika kasi nchini Tanzania, lakini ukosefu wa vituo vya kujazia gesi unalifanya mchakato huo kusuasua.

Kama ilivyo kwa Nigeria na baadhi ya nchi nyingine barani Afrika, Tanzania imeanza kukumbatia gesi asilia iliyoshindiliwa (CNG) kama mbadala wa petroli na dizeli.

CNG inaonekana kuwa safi zaidi na rafiki kwa mazingira kuliko mafuta hayo ya kisukuku, lakini gharama yake ya chini zaidi ndio kivutio kikubwa kwa takriban madereva 5,000 katika nchi hii ya Afrika Mashariki ambao wameanza kutumia gesi hiyo, hasa madereva wa biashara.

Idadi hii ni sehemu ndogo ya magari yaliyopo Tanzania, lakini wale waliopokea mabadiliko mapema wanafungua njia ya kukubalika kwa upana zaidi kwa CNG - ambapo serikali inaripotiwa kutaka matumizi karibu ya jumla ifikapo katikati ya karne hii.

Tanzania ina akiba kubwa ya gesi chini ya bahari, na kwa wale wanaojaza gesi hiyo, gharama ya CNG inaweza kuwa chini ya nusu ya gharama ya petroli.

Hilo lilimshawishi mmiliki wa teksi, Samuel Amos Irube, kutumia takriban shilingi milioni 1.5 za Kitanzania ($620; £495) kubadilisha gari lake lenye magurudumu matatu – linalojulikana kwa jina la bajaji – kuwa linalotumia CNG.

Lakini sasa, akihitaji kujaza gesi mara mbili kwa siku, mara nyingi anatumia muda mwingi akisubiri kwenye kituo cha kujazia gesi katika jiji kubwa la Dar es Salaam kuliko anavyotumia kupata kipato.

Kuna vituo vinne tu vya kujazia gesi katika kitovu cha biashara cha Tanzania.

Akiwa na hasira ya kimya kimya, anasema lazima asubiri angalau saa tatu kila anapotaka kujaza gesi, lakini akiba anayopata inamfanya avumilie, kwani hutumia tu asilimia 40 ya kile ambacho angepoteza kwa petroli yenye kiasi sawa.

Foleni zinazotembea polepole za magari kwenye kituo cha CNG cha Ubungo zinaonekana zikiendelea chini ya barabara. Hali ni ya utaratibu – kuna mistari mitatu wazi, moja kwa magari na miwili kwa bajaji – lakini ukeraji ni wa wazi.

Medadi Kichungo Ngoma, ambaye tayari amesubiri kwa saa mbili kwenye foleni, anatazama magari yaliyoko mbele yake huku akisubiri kando ya gari lake la kubeba mizigo lenye rangi ya fedha.
 
Back
Top Bottom