BAVICHA wapata baraka za Mwalimu Butiama

Kwani nyie mnataka demokrasia gani wakati bungeni mnakimbia bora kiwe chama cha kujitolea kusaidia wananchi ata kujenga shule mikutano ina saidia nini sasa
 
BAVICHA WAPATA BARAKA ZA MWALIMU BUTIAMA.

Baraza la vijana wa Chadema, Taifa leo wametembelea katika kaburi la hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere wakiwa na ujumbe maalum.

Timu hiyo ya Viongozi sita imeongozwa na M/kiti wa BAVICHA Taifa, Patrobas Katambi, Katibu mkuu Julius Mwita pamoja na Katibu Mwenezi BAVICHA Taifa, Edward Simbeye.

Wamefuatana na M/kiti wa BAVICHA mkoa wa Mbeya,George Tito Mjumbe wa baraza kuu Joseph Kasambala na Katibu wa BAVICHA mkoa wa Temeke Hilda Newton.

Bavicha walikwenda kupokea baraka zote kutoka katika Kijiji cha Mwitongo alipo zaliwa muasisi wa Demokrasia na mfumo wa vyama vingi nchini hayati Baba wa taifa Mwalimu Julius Nyerere.

Lengo la BAVICHA kufika maamuzi hayo ni baada ya kuona Demokrasia aliyoiacha Mwalimu inazidi kukanyagwa na watawala, hali inayopelekea taifa kurudi enzi za ukoloni.

Kilio hicho cha Bavicha kilipokelewa na Chief Wanzagi,mkuu wa ukoo wa wazanaki na msimamizi mkuu wa familia ya Mwalimu na makumbusho ya Mwitongo yenye historia kubwa katika nchi hii.

Pamoja na hayo Bavicha wamepata fursa ya kueleza kwa kina,juu ya Mwenendo mbovu wa watawala kuendelea kukandamiza Uhuru wa vyombo vya habari,haki za binadamu na utawala bora.

Baada ya ujumbe huo mzito Bavicha waliomba baraka za Chief kwenda kutimiza adhima yao ya kulisaidia jeshi la Polisi kuzuia mkutano haramu wa Ccm tarehe 23 july na baada ya baraka hizo sasa kazi imeanza kuelekea Dodoma kuwafunda Ccm jinsi ya kutii sheria bila shuruti,kwakuwa kuzuia mikusanyiko yote ya Kisiasa ni agizo la Raisi na lazima kauli ya mkuu wa nchi itekelezwe kwa vitendo.

Imetolewa July 06

Edward Simbeye
Katibu Mwenezi BAVICHA Taifa
MUNGU AWALINDE
 
Hivi nyie ni wehu? Nyerere alisha kufa, ni sawa na kupoteza muda wenu tu. Si mgeweka picha yake na kumuomba kuliko kupoteza pesa za safari.
 
Back
Top Bottom