BAVICHA kuanika kila kitu leo

Malizeni kwanza mpambano kati ya BAVICHA na Mbowe.Mbowe akitoa agizo kama mwenyekiti wa Chama Taifa kwa BAVICHA badala ya kulitii moja kwa moja kuwa mheshimiwa mwenyekiti kasema ,wao BAVICHA wanamwambia hilo tukikaa vikao vyetu kwanza tutaliangalia ndio tutoe jibu!!! Kwa hiyo wanamponda kuwa alitakiwa alipeleke kwenye vikao sio atamke tu kama mwenyekiti!!! Vitoto vya BAVICHA vimeota sharubu.Mbowe poleeeeeee Una watoto watukutu.Agizo la baba ndani ya nyumba halisikilizwi hadi watoto wakae waongee ndio waseme kwenye kikao chetu tumeamua hivi kwa lile baba yetu ulisema!! LOOO! BAVICHA wangekuwa wanangu ningewapiga nondo kama kufungwa nifungwe.Nini maana ya kuwa baba kwenye nyumba?


akome, aliwapa viroba mwenyewe mwaka jana sasa majibu ndo hayo!!
viroba noma sana.
 
hii inadhihirisha kuwa na demokrasia pana ndani ya chama hakuna mwenyekiti wa taifa ambaye ni Mungu mtu ndani ya chama,, na sio kila agizo lake ni sahihi huwa kuna room ya kujadiliana na kufikia muafaka

Tamko lenu BAVICHA mnalitoa saa ngapi? Saa hizi saa nane ujue! Kulikoni mmeufyata baada ya kumtikisia kibiriti Mbowe mkapata majibu yenu?
 
Wasipotoa karipio kwa Lowassa kwa kuwakejeli kuwa wanaenda Dodoma kuchora mistari kwenye kuta na kuwaambia chama chake hakitaki hizo harakati nitawaona tu kama UVCCM.
 
Tamko lenu BAVICHA mnalitoa saa ngapi? Saa hizi saa nane ujue! Kulikoni mmeufyata?
tulia mkuu haya mambo huwa yanapangwa kisayansi hatukurupuki uncle be patient kama wewe ni mwanahabari utapata mwaliko kama ni wale ambao hawana kazi maalumu Dar basi subiria hapa hapa utalipata tuu
 
Baraza la vijana CHADEMA leo linatarajiwa kuweka kila kitu hadharani katika mkutano na waandishi wa habari utakaofanyika makao makuu ya CHADEMA leo.

BAVICHA ambalo kwa sasa ndiyo baraza bora kabisa la vijana nchini litaweka msimamo wake kuhusiana na ombi la Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe kuwataka kusitisha msimamo wao wa kwenda Dodoma kuzuia mkutano mkuu wa CCM.

BAVICHA ambayo inaungwa mkono na maelfu ya vijana kote nchini tayari ilikwishaandikisha vijana zaidi ya 5000 kutoka sehemu mbalimbali nchini kwenda Dodoma kwa kazi hiyo.

Mkutano huo na waandishi wa habari utafanyika leo makao makuu kuanzia saa 6 nchini na utahutubiwa na viongozi wake wakuu Mwenyekiti Patrobass Katambi,Makamu Mkiti Patrick Sosopi,Katibu Mkuu Julius Mwita na Mratibu wa Baraza hilo kitaifa Edward Simbeye.

Waandishi wote mnakaribishwa!

Tutashukuru hiyo Jumamosi ijayo wakijaa kama siyo kufurika kwa wingi Dom ili askari Wetu wapate " mazoezi " mazuri ya ulengaji shabaha hasa kuanzia kichwani, mbavuni na katika ugoko.
 
tulia mkuu haya mambo huwa yanapangwa kisayansi hatukurupuki uncle be patient kama wewe ni mwanahabari utapata mwaliko kama ni wale ambao hawana kazi maalumu Dar basi subiria hapa hapa utalipata tuu

Mtaufyata tu BAVICHA.Hamuwezi kushindana na viongozi wa juu wa chama!! Siasa ni pamoja na kuheshimu viongozi wa juu wa Chama.Nyie BAVICHA sio samaki mnaoishi kwenye dimbwi lenu wenyewe.Huo ni ushauri wa bure.Take it or leave it.
 
Mkutano bado
Utasubiria sana.Huujui uwongo wa BAVICHA? Pia inawezekana wamefungiwa milango na wenye chama kuwa wasithubutu hata kuingia ofisini kufanya hicho kikao chao baada ya kumbezea Mbowe! Unajua tuwe wakweli kumbishia mwenyekiti hata wa kikao cha harusi tu sio afya sembuse chama!!
 
Mkutano bado
Mkuu CHADEMA sasa hivi kila mtu ana sharubu.Unaweza kuta huyo mtu aliyeleta hiyo habari ya huo mkutano wa BAVICHA ni mzushi tu kama yule aliyezusha kuhusu tamko la meya la kupingana na Makonda lililokanushwa na meya.

Cha kufanya ni kuwa matamko lazima yatoke kwenye ofisi za wahusika wenyewe kupitia kwa wasemaji wao official.Hizi za kupost mitandaoni uwe mwandishi wa habari au la usizitegemee na hata ukiziona zitumie tu kama za kukusaidia kuulizia ofisi husika kama za kweli au la.
 
Mtaufyata tu BAVICHA.Hamuwezi kushindana na viongozi wa juu wa chama!! Siasa ni pamoja na kuheshimu viongozi wa juu wa Chama.Nyie BAVICHA sio samaki mnaoishi kwenye dimbwi lenu wenyewe.Huo ni ushauri wa bure.Take it or leave it.
haya ni mawazo yako ya kijinga hayabudi kupuuzwa tu
 
Hata huku jimbo la hai tunapenda maandamano njooni jamani


Chadema kama wanapenda maandamano waende wakafanye jimbo la Hai
 
Jeshi la polisi limeingia mtego wa vijana wa chadema. Wameonyesha dunia wanavyotumikia ccm
 
Humu ndani uvccm sikuhizi wamebaki 4 tu wengine wamekimbia au sijuwi hawajawezeshwa.

Huu ni ukweli mchungu kwa UVCCM! Kwa sasa hakuna kabisa kijana toka UVCCM mwenye vision yoyote kuhusu Tanzo! Yamebakia magarasha tu ambayo kazi yao ni kufuata matamko tata,ya kichizi na yasiyo na tija kwa Taifa hili!
Mizee ya CCM ikishabwatuka pumba vijana hawa ni kufuata upepo tu kama bendera hawana hoja mbadala hata chembe!
Shame on you Uvccm. You must think out of the box you hooligans!
 
Back
Top Bottom