Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,613
- 13,293
Bashungwa ametoa wito huo leo Agosti 09, 2024 mara baada ya kujiandikisha kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura katika Kituo cha Shule ya Msingi ya Ahakishaka, Kata ya Nyabiyonza Wilayani Karagwe Mkoani Kagera.
Bashungwa ameipongeza Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi kwa kuboresha zoezi hilo na kufanya kazi kwa weledi inayoimarisha Demokrasia nchini.
Aidha, Bashungwa amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwa kinara wa kuendelea kuimarisha Demokrasia nchini na kuendelea kuiwezesha Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi.
Naye, Fidelis Makata, Mwandikishaji wa Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura katika Kituo cha Ahakishaka, ameeleza kuwa zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura linafanyika kwa siku saba kuanzai tarehe 05 hadi 11 Agosti 2024.
Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura unaoendelea unaongozwa na kauli mbiu “Kujiandikisha kuwa Mpiga Kura ni Msingi wa Uchaguzi Bora”.