Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,045
- 5,573
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Mbunge wa Jimbo la Karagwe, Innocent Bashungwa ametembelea na kujionea maendeleo ya ujenzi wa Msikiti wa BAKWATA Wilaya ya Karagwe mkoani Kagera (Masjid Zahra), leo tarehe 6 Machi 2025.
Awali, Bashungwa aliungana na Sheikh wa Wilaya ya Karagwe, Alhaj Nassibu Abdu Abdalah na viongozi wa dini ya Kiislamu wa Wilaya ya Karagwe kufanya dua ya kumuombea Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na kuliombea Taifa amani na utulivu.