Katiba ya Kenya ya nini? Sheria za nchi yetu zinatosha kumng'oa. Tatizo la nchi yetu kuna ombwe kubwa la utawala wa sheria. Watu wanajaribu kuongoza nchi kwa ubabe na kufuata hisia zao na siyo katiba na sheria.
Povu kuubwa linakutoka.... ukiulizwa una ushahidi gani kuhusiana na hivyo vyeti feki huna... kumbe maneno ya kuambiwa... ukiulizwa umeshawahi kuviona hivyo vyeti feki basi kwa hao waliokuambia.... hujawahi kuviona. ukiulizwa kwanni hao wanaodai vyeti feki hawaendi mahakamani kufungua hiyo kesi ya jinai ili mhusika afukuzwe kazi na kufungwa.... huna majibu. Watanzania lini tutaacha huu uzumbukuku na unyumbu?
- Tunajua kabisa ni kosa la jinai mtu kufoji vyeti. Anapashwa kufukuzwa kazi na kufungwa. Tingatinga alinza na gia hiyo hiyo ya msako wa vyeti feki. Wengi wamepoteza kazi, wengi wamekimbia kazi. Hiyo sheria mbona haina meno kwa mtu fulani? Double standards in udikteta wa hali ya juu.
- Kavamie na wewe kituo cha utangazaji ulazimishe wahusika watangaze unachotaka uone nini kitatokea. Tena nenda mchana tu hata bila wembe mkononi. Lakini mtu kafanya kituko ambacho hatujawahi kukishuhudia nchini kabla na baada ya uhuru na anadunda tu. Why? because sheria inakuwa sheria mtu mmoja akijisikia. It is a shame to my country and utter nonsensical governance!