Bashe: CCM ni waoga, wanafiki na wa kujipendekeza, hatuna sababu ya kuendelea kubaki madarakani

Leo Bashe atasifiwa sana maana ameongea yanayo pendwa na Bawacha lakini kesho akiongea wasiyo yapenda kuyasikia watamtukana sana!

Huu ndio unaitwa ujinga. Kwani kaungwa mkono kwa sura yake au kwa alilosema? Na mtu akisema leo lililo zuri na kusifiwa basi ni makosa kupingwa akisema la hovyo kesho?
Una onyesha una fikra mufilisi kabisa wewe, unaushabiki kama ule wa mpira kuwa hata timu yako ikicheza hovyo ni mwiko kuishauri kuwa imekosea kucheza. Unahitaji tiba asili upone
 
Akichangia kwenye bajeti ya mali asili na utalii amewaambia wabunge na serikali kuwa hawajawahi kuweka malengo haswa ya kutatua matatizo ya wafugaji na waulima, wamekuwa waoga, wanafiki na wakujipendekeza

Ameongezea CCM kwa wingi wao hawana sababu ya kuendelea kubaki madarakani kama wameshindwa kuishauri serikali kwa ukweli.



Wakitokea wabunge kama watano hivi kutoka chama tawala wakawa kama Hon. Bashe, hakika maana ya bunge kuishauri serikali itaeleweka vizuri kwa serikali na watanzania wote kwa ujumla. Kwenye mambo ya msingi tunaongea hoja na siyo misimamo ya vyama.
Hongera sana Hon. Bashe umeonyesha njia bora ya uwakilishi uliotukuka kwa wananchi na serikali yako!!!!!!!!!
 
Wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka jana,Edward Lowassa alikuwa na wafuasi na waliokuwa wanamuunga mkono katika harakati zake zilizokwama za Urais. Wafuasi na waunga mkono wake walianzia ndani ya CCM alipokuwepo kabla ya kujiunga na CHADEMA.

Wapo waliokuwa waziwazi na wale wa kujificha. Wapo waliohama naye chama kimwili na kifikra. Wapo waliohama naye kifikra lakini kimwili wamebaki CCM. Mfano wa hapa ni Wabunge wawili wa CCM. Wa kwanza ni Peter Serukamba wa Kigoma Kaskazini. Wa pili ni Hussein Bashe wa Nzega Mjini.

Serukamba wa wakati Lowassa akiwa CCM si huyu wa sasa. Serukamba yule wa 'kuwashughulikia' wapinzani 'amehama' na Lowassa. Kuhusu Bashe,amekuwa mwakilishi bora wa Lowassa Bungeni. Hoja zake,utoaji wa hoja zake,madongo ya chinichini na fikra zake,ni Lowassa mtupu. Bashe,kiukweli,amekuwa mwakilishi bora wa Lowassa Bungeni.

Siasa ina mambo sana!

Mzee Tupatupa wa 'Ulevini' Lumumba,Dar es Salaam
 
Inawezekana anasema ukweli, inawezekana hamaanishi anachosema, anataka "aonekane'...

Zamani baadhi yetu tuliwaamini sana kina Lugora, Serukamba, Kilango, Mhagama, tukidhani ni watetezi wetu kumbe wapigaji tu!
 
Aangalie kwa sababu ile kesi yake kwamba yeye sio raia ilimalizwa kichama na sio kisheria. Kuna hatari saana ya kujaribu kukata tawi ulilolikalia.
 
Huyu jamaa kaongea vizuri sana, ccm wanahitaji wabunge kama hawa, wabunge wanaoweza kusema hapana kwa ajili ya Taifa. Issue za zidumu fikra za chama sio wakati huu ambapo dunia iko kwenye utandawazi, watu wanaupeo na fikra nyingi, kwani wabunge wa ccm wangekuwa vile mbona tungekuwa na ahueni, wabunge wengine wa ccm pia wanatakiwa wabadilike.
nahis dam nyingine ya filikunjombe inaanza kuibuka...
 
Chama hivi baadhi yao wameanza kujitambua....CCM ndiyo kikwazo kikubwa katika maendeleo ya taifa hili...Hawa na unafiki ni sawa na uji na mgonjwa.
 
Tena hao CCM wanafiki sana linapokuja suala la
masilahi ya umma, na ndani ya CCM hakuna mtu aliyecommited kuwa hudumia wananchi , lakini sio wabunge wa CCMtu hata wapinzani wa kiasi fulani huungana kwa masilahi ya chama kuliko kuwahudumia na kutatua kero za wananchi. CCM na Serikali wafanye kazi ya kutatua matatizo ya wakulima na wafugaji waache mazoea.
kwa kutazama tu bila akili ya kushikiwa, CHADEMA na UKAWA ndo wanafiki no 1, waliosema edo fisadi baada ya kuja kwao wakabadili gia angani, ila watu 2, Dr slaa, na Prof. lipumba, walibaki kwenye ukweli,

ujumbe umefika, usifikiri bashe alikuwa anawaambia CCM ila CHADEMA, ila kwa kuwa hawakusoma fasihi, wao kwa akili wakajua ni CCM, hebu pimeni maneno yake, pitien uswahiba wake na yuleeeee, halafu nenda nae mstali kwa mstali utajua amewaambia ukawa a.k.a CHADEMA kuwa ni Wanafiki... ila hawajajua hyo fasihi...
 
Na kwa kuongezea nchi haitaendelea kamwe kama ni rais pekee ndie anayeogopwa na kuheshimiwa kuliko mihimili yote!
Ni lazima rais na serikali yake waliogope na kuliheshimu bunge tena wakisikia tu bunge linakaa waanze kujiweka sawa kama vile wanataka kutumbuliwa jipu!
wakisikia tu bunge limeamua au kuwaagiza jambo waseme ndio mzee kwa heshima!
Wabunge watakuwa hawatimizi wajibu wao sawasawa ikiwa ndoi wanamwogopa rais na kusema ndio mzee jambo ambalo kwa sasa ni dhahiri sana kupitia uwingi wa wabunge wa CCM.
kwa nanma hii ni vigumu kuendelea!
Namuunga mkono Bashe
 
Bashe ameanza kujitambua. Ni miongoni mwa wabunge wasema kweli tofauti na ilivyo kwa wabunge wengine wa chama chenu cha Walevi ambao wengi wao ni wanafiki. Maendeleo ya nchi hii yanakwamishwa na chama chenu cha walevi. Huu ni wakati wa kufanya mabadiliko makubwa katika mienendo yenu hapo Lumumba.
 
Heko Bashe kwa kusema ukweli amabao wengi wenu hawawezi kuthubutu kusema. Na yamkini ukaitwa kujadiliwa.
 
Back
Top Bottom