Baraza la Habari Tanzania (MCT) linazindua Ripoti ya Hali ya Sekta ya Habari Tanzania 2022/23 leo Julai 4, 2024

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
3,828
13,585
1000037021.jpg

LICHA YA UHURU VYOMBO VYA HABARI KUONGEZEKA TANZANIA, BADO KUNA SHERIA KANDAMIZI

Ripoti ya Hali ya Sekta ya Habari Tanzania kwa mwaka 2022/23 imeonesha pamoja na kuongezeka kwa Uhuru wa Vyombo vya Habari tangu Rais Samia Suluhu Hassan alipoingia Madarakani Machi 2021, bado utafiti kuna Sheria zinazokandamiza Uhuru wa Habari na Kujieleza

Kwa mujibu wa Utafiti uliofanywa na Dkt. Samwilu Mwaffisi, Mary Kafyome, Emmanuel Bulunde na Hawra Shamte, imeelezwa kuwa bado Waandishi wanakamatwa, wanapigwa, wananyimwa Habari, wanatukanwa au kudhalilishwa siyo tu na watu wasiojulikana bali pia na Vikosi vya Usalama na Maafisa wa Serikali

Aidha, licha ya Marekebisho ya Sheria ya Huduma za Vyombo vya Habari ya mwaka 2016, bado Sheria imebaki na baadhi ya Vifungu ambavyo vinatishia Uhuru wa Waandishi wa Habari pamoja na kuingilia Vyombo vya Habari

1000036886.jpg


JINSI VYOMBO VYA HABARI VILIVYOSHUGHULIKIA MASUALA MUHIMU YA MASLAHI YA UMMA: KESI YA DP WORLD NA SAKATA LA KUFUKUZWA NGORONGORO

Uchambuzi wa masuala haya mawili uliacha mengi ya kutamaniwa. Kesi ya DP World ilihusu uamuzi wa Serikali kutoa haki za kuendesha bandari za Tanzania Bara kwa kampuni kubwa ya usimamizi wa bandari kutoka Ghuba. Wanaharakati na vyama vya upinzani, hasa chama kikuu cha upinzani CHADEMA, walipinga hatua hiyo wakidai kuwa haitaleta faida kwa nchi na zaidi ilikiuka sheria. Kikundi cha wanaharakati kilifika mahakamani kupinga hatua hiyo, lakini hawakufanikiwa, na wamekata rufaa.

Kuhusu kufukuzwa kwa Ngorongoro, sakata hili lilihusu kufukuzwa kwa wafugaji wa Kimaasai kutoka Ngorongoro ambao wanaona eneo hilo kama ardhi yao ya asili. Serikali ilihalalisha kufukuzwa kwa sababu za uhifadhi. Wanaharakati walionyesha kwamba Wamaasai wameishi pamoja na wanyama wa porini katika eneo hilo kwa muda mrefu na walikuwa na mbinu zao za jadi za uhifadhi.

Baadhi ya wadau wa vyombo vya habari walisema kuwa Serikali ilishindwa kuunda mazingira wezeshi kwa waandishi wa habari kuripoti ukweli katika sakata la DP World na suala la uhamishaji wa Ngorongoro. Walisisitiza kuwa kulikuwa na mchanganyiko wa ukweli na uongo, na kufanya iwe vigumu sana kwa waandishi wa habari kubaini ni nani aliyekuwa akisema ukweli na ni nani ambaye hakuwa. Kila upande ulijaribu kuthibitisha kuwa ulikuwa sahihi.

1000036934.jpg

Hata hivyo, kulingana na matokeo ya utafiti, tatizo kubwa zaidi lilikuwa kwamba wataalamu hawakufanya uandishi wa habari wa kina kuhusu masuala hayo mawili. Udhaifu mkubwa ulikuwa kwamba vyombo vya habari havikufanya uchunguzi wao binafsi, hakukuwa na mahojiano ya kuelezea hali halisi na watu wenye ujuzi katika pande zote mbili, hasa upande uliokuwa ukipinga mkataba na uhamishaji, ikiwemo wananchi. Zaidi ya hayo, vyombo vya habari havikujitahidi kupata mkataba wa DP World wala kanuni za eneo la uhifadhi la Ngorongoro na kuzisoma. Kwa ufupi, vyombo vya habari vilishindwa kujitokeza na kuwapa taarifa za kutosha hadhira zao kuhusu masuala haya mawili.

Baraza la Habari Tanzania (MCT) linatarajia kuzindua Ripoti inayoangazia Hali ya Vyombo vya Habari nchini ambapo uzinduzi huo utatanguliwa na Mjadala wa Wadau wa Habari ukiongozwa na Katibu Mtendaji wa MCT, Ernest Sungura pamoja na Jopo la Wachangiaji ambao ni;
  1. Dkt. Samwilu Mwaffisi
  2. Emmanuel Bulendu
  3. Hawra Shamte na
  4. Mary Kafyome
Atakayewasilisha Ripoti hiyo kwa Umma ni Katibu Mtendaji Mstaafu wa MCT, Kajubi Mukajanga na kufuatiwa na uzinduzi utakaofanywa na Waziri Mkuu Mstaafu na Makamu wa Kwanza wa Rais, Jaji Joseph Sinde Warioba.

Muhtasari wa Ripoti

1. Sheria, Kanuni na Sera
2. Uwekezaji na Umiliki wa Vyombo vya habari
3. Uhimili/uvumilivu wa vyombo vya habari (Sustainability)
4. Vyombo vya habari vya mitandaoni
5. Misaada kwa vyombo vya habari
6. Mafunzo ya uandishi wa habari
7. Habari za Wanawake, watoto na watu wenye ulemavu
8. Hali ya vyombo vya Habari Zanzibar

WATAFITI: Samwilu Mwaffisi, Mary Kafyome, Emmanuel Bulunde, Hawra Shamte- habari za Zanzibar

Sheria, Kanuni na Sera

Utafiti umeonesha tangu Rais Samia Suluhu Hassan aingie madarakani Machi 2021 amekuwa na mwelekeo mzuri kuhusu uhuru wa vyombo vya habari na maendeleo yenye maslahi kwa waandishi wa habari na vyombo vya habari kwa jumla.

Waandishi wa habari waliohojiwa walikiri sasa kuna mazingira mazuri na uhuru zaidi wa vyombo vya habari.

Kutokana na juhudi za Rais, Shirika la Waandishi wa Habari Wasiokuwa na Mipaka (Reporters Without Borders) tarehe 3 Mei 2024 liliitangaza Tanzania kuwa nchi yenye uhuru wa vyombo vya zaidi kuliko nchi nyingine za Afrika Mashariki.

Tanzania imeshika nafasi ya 97 Mei 2024 ikilinganishwa na nafasi ya
143 mwaka wa 2023.

Hata hivyo, pamoja na mafanikio yote yaliopatikana wakati wa
uongozi wa Rais Samia, utafiti umebaini zile sheria na kanuni
kandamizi bado ziko kwenye vitabu vyetu vya sheria.

Bado waandishi wa habari na vyombo vya habari vinakutana na
madhila yanayofifisha matarajio na matakwa yao kuhakikisha
wanafanya kazi kwa uhuru na weledi zaidi. Hivyo bado iko haja ya kuendeleza jihudi za kuishawishi serikali kuihuisha sheria na kanuni zake kandamizi.

UWEKEZAJI KWENYE VYOMBO VYA HABARI

Katika kipindi cha 2022-2023 hakukuwa na uwekezaji mkubwa
kwenye sekta ya habari. Vyombo vya habari bado vinamilikiwa na watu/makampuni machache na hivyo kutoa nafasi kubwa kuushawishi (influence) umma
kwenye mambo yenye masilahi mapana kwa taifa.

Upo umuhimu wa kubadilisha sheria ili wageni waweze kuwekeza kwenye sekta ya habari wakiwa na hisa nyingi zaidi ya wazawa.

Uhimilivu wa Vyombo Vya Habari

Vyombo vya habari vya zamani (traditional media) na vya kisasa (digital media) vinakabiliwa na changamoto nyingi zinazovifanya vijiendeshe kwa taabu sana.

Miongoni changamoto hizo ni: kazi kubwa kwenye maendelo ya teknolojia, sheria na kanuni zilizopo, hali mbaya ya biashara, upungufu
wa mitaji, na kupungunga kwa matangazo.

Hivyo kuna haja ya vyombo vya habari kuwa vibunifu katika kubuni
njia mbadala za mapato katika mazingira ya sasa ya ushindani.

VYOMBO VYA HABARI VYA MITANDAONI

Matumizi ya vyombo vya habari vya mitandaoni yameongezeka na
kubadili njisi watu wanavyotengeneza na kutumia maudhui.

Aidha vimeleta mapinduzi makubwa katika nyanja za mawasiliano na
hivyo kuwapatia watanzania njia mbadala za kuwasiliana miongoni
mwao ndani ya nchi na watu wengine nje ya nchi.

Hata hivyo, vyombo vya habari vya mtandaoni vimeleta changamoto
kubwa sana kwa jamii, hasa uandishi wa habari wa wananchi (citizen journalism)

Citizen journalism inatekelezwa na watu wanaojiita waandishi wa
habari lakini hawana hata mafunzo ya awali ya uandishi wa habari.
Matokeo yake wanakiuka sana maadili ya uandishi wa habari na hivyo kuleta mkanganyiko kwenye jamii.

Kudhibiti hali hii serikali imetunga sharia, kwa mfano sharia ya Electronic and Postal Communications (Online Content) Regulations ya 2020 na ile ya Cybercrime Act ya 2015

Pamoja na nia nzuri ya sharia hizi, bado wadau wa vyombo vya habari wanaziona kuwa miongoni mwa zile sharia kandamizi zinazoadhiri uhuru wa vyombo vya habari.

MISAADA KWA MAENDELEO YA VYOMBO VYA HABARI

Katika kipindi cha 2022-23 misaada kwa maendelo ya vyombo vya habari imekuwa michache sana.

Hali hii imetokana na wafadhili kusitisha misaada yao ya kuendeleza vyombo vya habari hapa nchini.

Hata hivyo, kuna vyombo vichache vya habari vilipata misaada ama ya mali ama ya fedha au vyote viwili kutoka kwa wafadhili wa nje ya nchi.

Jitahada za vyombo vya habari vyenyewe kuwasaidia wafanyakazi wao na kugharamia shughuli za maendeleo hazikufanikiwa kwa kiwango kikubwa kutokana na upungufu wa fedha.

MAFUNZO YA UANDISHI WA HABARI NA WELEDI.
KIWANGO CHA NTA 4,5,6

Vyuo vya habari vinavyofundisha kwa kiwango cha 4,5,6 vinafanya vizuri kwa sababu vitatumia CBET
Wanafunzi wanamaliza vyuo wakiwa na stadi za uandishi wa habari, hivyo wanafanya vizuri wanapokwenda kwenye vyombo vya habari.

VYUO VIKUU

Wanafunzi wanaomaliza katika vyuo vikuu - hawana stadi.

SABABU:

i. Wanafunzi ni wengi kuliko vifaa vya kufundishia.
ii. Mitaala yao ni ya KBET.
iii. Wahadhiri wengi hawana uzoefu katika fani ya uandishi wa
habari - wanafundisha nadharia.
iv. Graduate Point Average (GPA)
TCU inataka GPA ya 4.0 na mtu kufundisha chuo kikuu.

Wanafunzi wanaomaliza chuo wasiokuwa na uzoefu
ndiyo wenye GPA ya 4.0 au zaidi
Waandishi wa habari wenye uzoefu wana GPA ya chini ya 4.0.

Hata wenye 3.7 na 3.9 walipogunduliwa waliachishwa
kufundisha muda wa ziada (part time)

V. Wanafunzi kukosa utashi (passion) wa uandishi wa habari
Wanachukua somo la uandishi kwa sababu wamechaguliwa na mfumo wa TCU. Hivyo wanataka cheti kuliko stadi.
VI. Elimu ya sekondari
  • Lugha ya kufundishia vyuo vikuu na kiingereza.
  • Wanafunzi wengi wana matatizoi ya lugha ya kiingereza
  • Hawana stadi za mawasiliano - communication skills.
Walitumia mtaala wa KBET. Hivyo wanakariri sana kuliko
kutenda.

HABARI ZA WANAWAKE, WATOTO NA WENYE ULEMAVU

Sauti zao bado hazisikiki

Sauti za wanawake zimeanza kusikika ukilinganisha na miaka 10 iliyopita.

SABABU: Kuongezeka kwa harakati za haki za wanawake.
Kuongezeka kwa wahariri wanawake.

Utafiti pia ulilenga kutazama ufanisi wa utendaji wa wahariri
wanawake.

Wanafanya vizuri lakini wanakabiliwa na changamoto

i. Waandishi wa habari wanaume hawawaheshimu kama
wanavyo waheshimu wahariri wanaume
ii. Wamiliki wa vyombo vya habari hawawaamini hata kama
wanafanya vizuri.
iii. Waandishi wa habari wanawake hawawapi "support"
walioitazamia.

Pia Soma:

 

Attachments

  • 1000036662.jpg
    1000036662.jpg
    628.5 KB · Views: 5
  • 1000037038.jpg
    1000037038.jpg
    92.7 KB · Views: 3
  • 1000037033.jpg
    1000037033.jpg
    44.5 KB · Views: 5
Baraza La Madaktari Tanzania wanatumia Kifupi cha MCT , Pia Baraza Habari Tanzania wanatumia hicho hicho Kifupi MCT...!

Mmojawapo itabidi abadilishe..!
 
View attachment 3033081
Baraza la Habari Tanzania (MCT) linatarajia kuzindua Ripoti inayoangazia Hali ya Vyombo vya Habari nchini ambapo uzinduzi huo utatanguliwa na Mjadala wa Wadau wa Habari ukiongozwa na Katibu Mtendaji wa MCT, Ernest Sungura pamoja na Jopo la Wachangiaji ambao ni;
  1. Dkt. Samwilu Mwaffisi
  2. Emmanuel Bulendu
  3. Hawra Shamte na
  4. Mary Kafyome
Atakayewasilisha Ripoti hiyo kwa Umma ni Katibu Mtendaji Mstaafu wa MCT, Kajubi Mukajanga na kufuatiwa na uzinduzi utakaofanywa na Mjumbe wa Bodi ya Baraza la Habar, Dkt. Joyce Bazira.

Pia Soma:

waogawaoga tu
 
Back
Top Bottom