Black Butterfly
Senior Member
- Aug 31, 2022
- 127
- 362
Naenda moja kwa moja kwenye hoja yangu. Kuna vitu vinafanywa na Serikali vinakera sana. Mfano. TMA walitangaza zaidi ya miezi miwili nyuma kwamba kutakuwa na Mvua kubwa za e El Nino ambazo zitaendelea hadi mwezi wa 3 mwaka 2024 lakini Serikali ilitulia bila kufanya Marekebisho ya Barabara zake kwenye Mitaa mbalimbali
Hatimaye mvua zimeanza na Barabara nyingi kwenye maeneo mengi hasa jijini Dar sala Salaam zimejaa Maji yaliyotuama kwasababu hakuna Mitaro, zimejaa Mashimo, wananchi wasio na vyombo vya Usafiri wanalazimika kuvua Viatu na kutembea katika Madimbwi ya Maji machafu wakiwemo Watoto wanaokwenda Shule.
Nimepita maeneo mengi kwenye Jimbo la Segerea, Barabara hazifai na Mbunge Bonnah Kamoli yupo tu hata hazungumzii kero hizo. Nimeenda ofisi za kadhaa za Serikali za Mitaa mfano Mtaa wa Mfaume barabara ya Mangumi haijawahi hata kupitishwa Magreda ya kukwangua tu kusawazisha.
Maafisa wa Serikali za Mtaa wenyewe wanalalamikia Serikali Kuu ikiwemo Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kutochukua hatua licha ya kufikishiwa kero za ubovu wa Barabara kwa muda mrefu.
Nashauri wenye Mamlaka kutatua shida za Wananchi mapema na sio kusubiri hadi nyakati za Uchaguzi zikikaribia Wagombea waje kuwahadaa Wananchi kwa kuomba Kura wakiahidi kushughulikia matatizo yaliyodumu kwa muda mrefu.
Soma >> Waziri Bashungwa atoa maelekezo kwa TANROADS kukarabati mifereji, Novemba 7, 2023