Barabara ya kwenda kwa mzee wa upako daraja la kamba Mbeya

Mkuu mtafuteni mchungaji maarufu au mgawa kikombe cha dawa feki apige kambi kwenu mtapata daraja chapchap
 
Hivi karibuni tumeshuhudia jinsi wananchi wa Rungwe Mbeya wanavyotaabika kuvuka mto kwa kamba, akina mama wakiwa na mizigo yao huvuka mto huo kwa kuning'inia kwenye kamba mithili ya nyani au mwanajeshi anayevuka vikwazo kipindi cha vita, hali ile inahatarisha maisha ya wananchi na wakazi wale, lakini ni hivi karibuni tumeshuhudia rais akiwa anaahidi kujenga barabara ya kwenda kanisani kwa mzee wa upako.

Kati ya daraja lile na barabara ya kwenda kwa mzee wa upako ni kipi kilihitaji pesa ya haraka kwa ajili ya kujengwa?

Kwanini Rais hakuelekeza pesa hizo katika uje wa daraja lile ili kuokoa wale akina mama wanaoning'inia kwenye kamba kama nyani.

Rasimali za taifa zigawanywe sawa Tanzania sio Dar es Salaam tu.
NImeipenda hii. Hivi ni kweli kuwa hawa hawana shida zaidi ya wale wa kwenda kwA mZee wa uPAKO?
1465849662672-jpg.356289
 
Wajitahidi tu hiyo nayo ni moja ya kazi....hapa kazi tu.Mzee wa upako alikuwepo mabadiliko wacha awekewe mkeka.
 
Lete takwimu zifuatazo

1.Onyesha kuna watu wangapi wanaotumia hilo daraja linalotumia kamba (population)
2.Kuna shughuli zipi za kiuchumi zinazofanyika kwenye hilo eneo
3.Kodi za serikali zinazokusanywa kutoka kwa watu wa eneo hilo ni kiasi gani
4.Hilo daraja huwa wanavuka wakitokea wapi kuelekea wapi na kwa ajili ya shughuli zipi au kitu gani?
5.Je eneo wanaloishi ni eneo salama au hatarishi kitaalamu?
Una akili kama za jesca
 
hv kila kitu mpk afanye raisi.....nafkiri kuna levels za uongozi akipata taarifa atalishughulikia
 
Nilimuelewa sana Mbowe kwenye kampeni za uchaguzi wa raisi wa mwaka 2005 pale Furahisha Mwanza kuwa nchi hii hili itawalike kwa haki ni lazima kuwe na utawala wa majimbo.
Maana huu utawala wa Raisi kuamini Dar ikiwa salama ndio Tanzania yote kuwa salama maendeleo ya Nchi hadi arudi Yehova hapo.
 
Hivi karibuni tumeshuhudia jinsi wananchi wa Rungwe Mbeya wanavyotaabika kuvuka mto kwa kamba, akina mama wakiwa na mizigo yao huvuka mto huo kwa kuning'inia kwenye kamba mithili ya nyani au mwanajeshi anayevuka vikwazo kipindi cha vita, hali ile inahatarisha maisha ya wananchi na wakazi wale, lakini ni hivi karibuni tumeshuhudia rais akiwa anaahidi kujenga barabara ya kwenda kanisani kwa mzee wa upako.

Kati ya daraja lile na barabara ya kwenda kwa mzee wa upako ni kipi kilihitaji pesa ya haraka kwa ajili ya kujengwa?

Kwanini Rais hakuelekeza pesa hizo katika uje wa daraja lile ili kuokoa wale akina mama wanaoning'inia kwenye kamba kama nyani.

Rasimali za taifa zigawanywe sawa Tanzania sio Dar es Salaam tu.
Inawezekana ile video clip hakuiona ungefanyika mpango atumiwe hata kwa Whatsapp na clips nyingine nyingi za maeneo mengine yenye shida kuliko hiyo barabara ya kwa huyo mpakwa mafuta. JK namba yake ilikuwa inajulikana sijui huyu namba yake ni ipi. Halafu mtoa uzi ingekuwa vizuri ukaatach kale ka video clip kwenye uzi wako kwani kuna watakaosoma lakini hawakuwahi kukaona ile video ya wale watu walivyokuwa wananing'inia kwenye kamba kuvuka ule mto
 
Huyu jamaa basi tu sasa hapo mama watu ana hatari mbili kwenda na maji au kwenda na mamba. Halafu eti nimechaguliwa na masikini ndo hivi kweli ni fedheha mbele za mungu.
Husijeshangaa kati ya wanaovuka hapo 70% wanasisiem mkuu
 
Mi nilidhani ndo huyu mlisema kachaguliwa Mungu, sasa kwa nin asijenge kwanza njia ya wanaoenda kanisani?
 
Back
Top Bottom