Bara la Afrika litaendelea kuitwa masikini na majina mengine ya ovyo mpaka litakapotunga na kutekeleza Sheria ya kunyonga wahujumu uchumi

Mr Why

JF-Expert Member
Nov 27, 2019
2,471
4,798
Bara la Afrika litaendelea kuitwa Masikini, Shamba la bibi etc, mpaka pale litakapotunga na kutekeleza Sheria ya kunyonga Wahujumu uchumi

Bara la Afrika limekuwa likitupiwa lawama za kila aina kwa madai ya kuwa linaonekana kama halina watu makini, nchi zake kuwa na maisha ya duni na mengineyo mengi

Pia soma Rais Samia akipokea Ripoti ya CAG kwa Mwaka 2023/2024 Ikulu Dar, Machi 27, 2025

Lawama na fedhela zote hizi zinasababishwa na kukosekana kwa viongozi wenye uwezo wa kusimamia Sheria.

Sheria nyingi zimetungwa tangu zamani lakini utekelezaji wake ni hafifu

Umasikini wa Afrika unasababishwa na kuwepo kwa viongozi Serikalini wenye tabia ya kuhujumu miradi ya Serikali matokeo yake nchi zinakosa fedha za kujiendesha nakuanza kujiingiza kwenye mikopo inayosababisha madeni makubwa yasiyolipika

Ili bara la Afrika liweze kupiga hatua kubwa kama bara la Ulaya lazima lianze kutekeleza Sheria ya kunyonga Wahujumu uchumi kinyume na hapo litaendelea kudharaulika na mataifa makubwa
 
Huo ndiyo ukweli. Itungwe Sheria ya kunyonga mafisadi, Wala rushwa na wanaotumia vibaya ofisi za umma.
 
Mkuu, pendekezo lako ni zuri, lakini anaetunga hiyo sheria si ni hao hao watuhumiwa wa makosa ya hiyo sheria? Huoni kama kuna conflict of interest hapo? Kama mauchafu yote hayo na bado tunawapa KURA huoni kama hata wananchi tuna matatizo makubwa pengine kuliko hata hao WALAJI?
 
Huo ndiyo ukweli. Itungwe Sheria ya kunyonga mafisadi, Wala rushwa na wanaotumia vibaya ofisi za umma.
China ilitunga na kutekeleza Sheria ya kunyonga Wahujumu uchumi matokeo yake Uchumi ulipanda sana mpaka ukatisha Mataifa ya Ulaya
 
Back
Top Bottom