Bank imeuza dhamana(gari) bila kumpa taarifa mmiliki

mkushite

JF-Expert Member
Sep 2, 2021
636
1,497
Ndugu wanasheria, rafiki yangu anaomba msaada wa kisheria ili apate haki yake.

Alichukua mkopo bank na kuweka gari yake kama dhamana, ila kwa bahati mbaya akachelewesha marejesho mpaka dhamana yake ikakamatwa na madalali.

Hiyo gari yake imeuzwa bila yeye kupewa taarifa ya mnada, anakuja kushtuka baada ya kutumiwa ujumbe na bank kwamba gari yake tiyari imeuzwa kwenye mnada uliofanyika wiki moja nyuma.

Je kisheria hii imekaaje?,
na kama anataka kudai haki yake aanzie wapi?
 
Rudi kwenye mikataba mliyoosainishana wakati anachukua mkopo...
 
Ndugu wanasheria, rafiki yangu anaomba msaada wa kisheria ili apate haki yake.

Alichukua mkopo bank na kuweka gari yake kama dhamana, ila kwa bahati mbaya akachelewesha marejesho mpaka dhamana yake ikakamatwa na madalali.

Hiyo gari yake imeuzwa bila yeye kupewa taarifa ya mnada, anakuja kushtuka baada ya kutumiwa ujumbe na bank kwamba gari yake tiyari imeuzwa kwenye mnada uliofanyika wiki moja nyuma.

Je kisheria hii imekaaje?,
na kama anataka kudai haki yake aanzie wapi?
Haki gani tena apo si aliwekea dhamana iyo gari au sijaelewa??
 
Aachane nalo hilo gari msaada gani wa kisheria utakuja bila kukuongezea gharama !? Gari ni kitu unaweza weka nia ukikpata tu tena kwa mwaka mmoja . Jifunze kukopa kwa ajili ya maswala yenye return
 
Kama wakili Msomi! Rejea mkataba, kama hauna kipengele cha Dhamana kufidia mkopo bila makubaliano, basi ufungue hata kesi ya kuibiwa Gari🤗
 
Mikataba ndio ina haki za pande zote mbili kawaida ukikiuka mkataba kinachofuatia ni hicho kilichotendeka.
Mf. "Mkopo usipolipwa ndani ya siku husika basi dhamana iliyowekwa itauzwa bila taarifa zaidi kwako kwaajili ya kufudia mkopo na gharama zote zilizoongezeka."

Angesoma vizuri mkataba kabla ya kusaini na kuchukua mkopo
 
Back
Top Bottom