johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 85,044
- 143,778
Sheikh wa mkoa wa Arusha Sheikh Shaaban Bin Juma akiambatana na viongozi wengine wa BAKWATA mkoa wa Arusha leo, Mei 07.2024 ameongoza sala maalum ya kumuombea kheri Mkuu wa mkoa wa Arusha Paul Christian Makonda ili aweze kufanikiwa kwenye programu yake maalum inayoanza kesho Mei 08.2024.
Makonda atakuwa na siku tatu maalum za kusikiliza na kutatua kero mbalimbali za wananchi wa Arusha kuanzia kesho Mei 08 hadi 10.2024 zoezi ambalo litafanyika kwenye ofisi za Mkuu wa mkoa hio mjini Arusha.
Sheikh Shaaban Bin Juma amempongeza Makonda kwa maono yake ya kuja na programu ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi, akisema programu hiyo ni sehemu ya kuhakikisha Arusha inakuwa na amani, usalama na matumaini ya kutosha kwa wananchi na wageni wanaofika mkoani humo.