Mtafiti Pro
Member
- May 5, 2018
- 20
- 7
Kwenye nyumba zetu tunazoishi au maeneo mbalimbali ya biashara, changamoto ya umeme wa kushea ni kero kubwa kutokana na kutegemea mfumo wa kushea mita moja ya umeme (LUKU).
Katika mfumo huu ni ngumu kutambua matumizi ya umeme kwa mtu binafsi, ni ngumu kudhibiti matumizi ya umeme kwa mtu binafsi wala haizuii mtu asiyechangia kununua umeme kukosa umeme pale wengine wanaponunua.
Kwakuwa mahitaji ya umeme yanaendelea kukuwa kwa kasi hasa kwenye nyumba za wapangaji, fremu za biashara, masokoni, viwandani n.k maendeleo ya teknolojia yameweza kutufikishia kifaa hiki kiitwacho PREPAID ENERGY METER.
Kutokana na mahitaji ya kisheria, na kwakuwa ufungaji wake unategemea umeme kutoka kwenye mita kuu(LUKU) mita hii itakuwa sahihi zaidi tukaita PREPAID ENERGY SUBMETER au kwa kifupi SUBMETER inatosha.
IJUE PREPAID SUBMETER
Hii ni aina ya mita inayotumika kupima matumizi ya umeme(Kwh) kwa mtumiaji/watumiaji husika kwa kupitia mfumo maalum wa malipo kabla(Prepaid).Ufanyaji wake kazi ni kama mita ya LUKU kwa sababu ina mfumo wake wa kupata token ambazo zikiingizwa kwenye mita hiyo ndio itawasha umeme upande huo uliofungiwa na endapo units zitaisha kwenye submeter umeme hautoendelea kuwaka(utakatika) mpaka ziingizwe tena token.
kimsingi, mita hii hupokea umeme kutoka kwenye mita kuu lakini ili iruhusu umeme kufika kwa mtumiaji ni lazima uingize token.Ni kama vile mita ya LUKU inavyopokea umeme kutoka kwenye nguzo haiwezi kuruhusu umeme kufika mjengoni mpaka uingize token.
Katika nchi ambazo shirika la usambazaji umeme ni moja mfano hapa kwetu Tanzania sheria hairuhusu kuunganisha mita hizi kabla ya mita kuu (i.e LUKU) hivyo ufungaji wake hufanyika ndani ya mfumo wa wiring, hivyo mita ya LUKU itabaki kuwa Main halafu hii nyingine itakuwa Sub.
Na ili kuweza kufurahia zaidi mita hii ni vema zifungwe kuanzia mbili (2) na kuendelea.Sababu ya kufanya hivyo ni kuhakikisha kuwa hakuna upande wowote utakaokuwa unapata umeme kutoka kwenye mita kuu moja kwa moja bila kudhibitiwa na submeter.Likifanikishwa hili mfumo utafanya kazi kwa ufanisi, utazuia maswali mengi na utaeleweka haraka hata na watu wenye uelewa wa chini.Ni kwa sababu, endapo units zitaisha upande mmojawapo umeme utakatika upande husika bila kuathiri upande mwingine.
Kinyume na hapo,yapo maeneo ambayo hufungwa moja kutokana na mahitaji ya mteja kutokana na sababu mbalimbali.Kwa mfano mwenyenyumba anataka kumdhibiti mpangaji wake asitumie umeme ikiwa hajanunua unaweza kufunga submeter moja.Vilevile ikiwa mpo wapangaji wengi baadhi mnaelewana kwenye kununua umeme lakini baadhi ni wasumbufu kununua umeme, mnaweza kuwadhibiti hao wasumbufu wasitumie units zenu ikiwa units zao zimeisha na hawakununua tena.
Hivyo, ukifunga submeter moja bado itafanya kazi yake kwa ufanisi lakini inahitaji ufafanuzi wa kiufundi kulingana na mahitaji yako na mazingira husika.
Ikiwa uelewa wako mdogo utakuwa unapiga simu kila siku kutaka kuelekezwa inafanyaje kazi.
Kwa kumalizia tu ni kwamba,
ππππππ ππππ πππππ πππ ππππππ ππππππππ ππππ:-
Ukihitaji kupata huduma hii hakikisha unawasiliana na mkandarasi mwenye uzoefu na kazi hizi asiyekuwa na tamaa ya pesa kwanza kabla ya kukupa elimu. Mimi nimefungiwa na hawa jamaa wanaitwa DARWAT CRAFTERS, unaweza ku-google ukaona kazi zao.
Wanajua sana kuhusu hizi submeters na hawajaweka tamaa ya pesa mbele.Kama wakikuona huwaelewi wanakuambia usiwe na presha jipe muda wa kujifunza taratibu, ukibarikiwa kuelewa wapigie kwa sababu hawataki kusumbuana na wateja baada ya kutoa huduma.
Unaweza kuangalia kazi zao Instagram, Facebook, Twitter au Linkedlin kwa jina DARWAT CRAFTERS au unaweza kuwapigia simu.
0653535595/0694240393.