Baba aitaka Hospitali ya Aga Khan imlipe fidia ya Tsh. Bilioni 1.2 baada ya mtoto wake kukatwa mguu

BigTall

JF-Expert Member
Mar 9, 2022
541
1,304

View: https://www.youtube.com/watch?feature=shared&v=5DrxCZ8iVZs


WhatsApp Image 2025-04-19 at 10.03.34_1eb6b337.jpg


Mwanaume anayefahamika kwa jina Ally Mkii, Mkazi wa Msongola Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam, ameishtaki Hospitali ya Aga Khan iliyopo Jijini Dar es Salaam imlipe fidia ya kiasi cha Shilingi Bilioni 1.2 kutokana na madai yake kuwa mtoto wake amekatwa mguu wa kulia kwa uzembe katika Hospitali hiyo.

Ally amefungua shauri hilo la madai Namba 26889/2024 katika Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala ndogo ya Dar es Salaam, chini ya Jaji Hussen Salum Mtembwa akiwa na madai kwamba mtoto wake alifanyiwa uzembe wa kimatibabu na kusababisha kuondolewa kwa mguu wake uliokuwa umeumia kwa kujikwaa akiwa anacheza na wenzake.

Wakili wa utetezi wa upande wa mashtaka, Wakili Pasensa Kurubone alifafanua kwamba shauri hilo la madai limefunguliwa katika Mahakama hiyo, ambapo washtakiwa ni hospitali hiyo pamoja na daktari aliyehusika na matibabu ya mtoto.

Amesema "Kimsingi shauri hili ni la madai dhidi ya hospitali hiyo pamoja na daktari mwajiriwa wa hospitali hiyo aliyesababisha madhara ya mtoto, na mteja wangu katika shauri hilo anasimama kama kimvuli cha mtoto aliyesababishiwa madhara na wakati yanafanyika alikuwa na umri wa miaka miwili na kwa mujibu wa kisheria hawezi kusimama mwenyewe mahakamani.

Alisema kuwa mteja wake anadai fidia ya unafuu iliyotokana na madhara yaliyopelekea mguu wa mtoto wake kukatwa na kutaka kulipwa fidia ya unafuu kiasi cha Sh Milioni 700, na Sh Milioni 500 kama nafuu za ujumla ikiwemo usumbufu.

Alisema baada ya kuwasilisha maombi yao ya fidia, upande wa wadaiwa walileta pingamizi wakidai kwamba Mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza shauri hilo kwa sababu ni masuala ya kitabibu yanayopaswa kusikilizwa kwenye mabaraza ya wakunga.

Hata hivyo baada ya mapingamizi hayo, Jaji Mtembwa wiki iliyopita alitoa uamuzi wa kutupilia mbali na kudai kuwa maombi ya walalamikaji yanamsimgi na hivyo kesi hiyo upangwa kuendelea Aprili 30, 2025 itakapo kuja kwa ajili ya kutajwa ili kupanga namna ya uendeshaji wa shauri hilo.

Upande wa Mlalamikaji Ally Mkii, baba mzazi wa mtoto aliishukuru Mahakama hiyo kwa kutenda haki baada ya kutupa mapingamizi ya upande wa utetezi na kuona kwamba ipo kesi ya msingi ya kusikilizwa.

Akisimulia mkasa wa mtoto wake, Mkii alisema kwamba Mwaka 2022 mtoto wake akiwa anacheza na wenzake mtaani aliumia na kupelekwa katika Hospitali hiyo ya Aga Khan katika Tawi la Mbagala.

Alisema baada ya kufika mtoto wake alifanyiwa kipimo cha picha (Xray)na baadaye kuamuliwa kupelekwa katika hospitali kubwa iliyopo Jijini Dar ambapo alifanyiwa kipimo na kugundulika kuwa mguu umevunjika na kufungwa POP.

Alisema alirejea nyumbani akiwa na mtoto na ndani ya siku nne aliona maendeleo ya mtoto sio mazuri na kuamua kumrejesha tena katika hospitali hiyo na baada ya kufika alifanyiwa Kipimo cha CT Scan na Ultrasound na kugundulika kuwa damu haitembei kwa sababu POP ilikuwa imebana, ilifungwa vibaya na kumshauri mguu ukatwe.

"Sikukubaliana na hilo niliomba niende hospitali kubwa ya Taifa Muhimbili na nilipofika waligundua kuwa damu haitembei na kushauri pia mguu ukatwe haraka na ukicheleweshwa mtoto anaweza kupoteza maisha, nilikubaliana na mguu kukatwa ili kunusuru maisha.”

Chanzo: Gadi TV
 
Hili liwe fundisho na kwa wengine, hata wale hindu mandal walimhudumia mwanangu vibaya hadi leo mkono umepinda, sijui na mimi niwasweke ndani hawa, fursa hii

Hawa wahindi ni hawajali kabisa huduma bora
 
Back
Top Bottom