Bushmamy
JF-Expert Member
- Aug 18, 2019
- 9,038
- 15,693
Baadhi ya wananchi wa Jiji la Arusha wamesikitishwa na upendeleo unaofanywa na TASAF kwa kuwapatia vijana wenye nguvu na wenye kujiweza pesa badala ya wahitaji wa mfuko huo ambao ni wazee wasiojiweza, na kaya maskini.
Akizungumzia suala hilo Mwenyekiti wa Mtaa wa Olkirowa, Kata ya Lemara iliyopo Halmashauri ya Jiji la Arusha, Albert Joseph amesema kuwa ni kweli hilo suala kama hilo lipo kwenye mtaa wake na amekuwa akishuhudia vijana wenye nguvu wakipewa pesa huku wahitaji wanaostahili kupewa fedha hizo wakikosa.
Ameendelea kusema kuwa amejaribu kulitafutia ufumbuzi suala hilo kwa kushirikisha TASAF lakini alichojibiwa ni kuwa TASAF wana vigezo vyao.
Naye, Diwani wa Kata ya Lemara, Naboth Paulo Silasi akizungumzia suala hilo amesema kuwa tatizo kama hilo halipo kwenye kata yake ya Lemara tu bali ni sehemu kubwa ya Arusha ameliona hilo kuna upendeleo katika utoaji wa fedha hizo huku walengwa wakikosa.