Mwanongwa
JF-Expert Member
- Feb 15, 2023
- 541
- 532
Kwa mfano katika masoko ya Sido, Mwanjelwa, Kyela, Tukuyu na Makambako kuna watoto wengi ambao umri wao ni kati ya Miaka 13 hadi 17 na walitakiwa kuwa shuleni lakini sasa wameajiriwa na wafanyabiashara hao.
Kabila ambalo limekuwa maarufu kuajiri Watoto kwenye maduka ni hawa ndugu zetu kutoka mkoa wa Njombe, Wilaya ya Makete (Wakinga).
Wakinga wamekuwa ndiyo kabila ambalo limekuwa mstari wa mbele kwenye hizo ajira za Watoto maeneo mbalimbali ya Biashara hapa jijini Mbeya.
Wabacgokifanya mara nyingi ni kwenda vijijini kwao na kuchukua watoto wa ndugu zao na kuja nao mjini ili kuwatumikisha.
Wanapofika Mjini, Watoto hao hufanya kazi kwenye maduka hayo kwa muda mrefu kwa malipo ya chakula tu mpaka pale atakapotimiza muda ambao wamekubaliana na Boss husika ndiyo anakabidhiwa mtaji.
Ukiwauliza wenye maduka kwamba kwa nini wanafanya hivyo majibu yao ni kwamba hawajawaajili bali wanawasaidia tu kazi ndogondogo.
Kama hawa wanawasaidia kazi ndogondogo kwa nini wasiwaweke Watoto wao ndiyo wawasaidie hizo kazi?
Watu wa Ustawi wa Jamii siyo kwamba hawajui jambo hili wanalijua vizuri kabisa sababu nao ni wateja wa maduka hayo na hao watoto wanawakuta.
Kwa hapa Sido kuna mtaa unaitwa Mtaa wa Sharifu Makoba, ndiyo watoto hao wanapatikana kwa wingi kwenye maduka ya Wakinga.
Kuna hiki kisa nilikutana nacho katika Soko la Makambako, kuna mtoto wa kiume alikuwa anasoma kidato cha pili katika Shule ya Sekondari Kijombe iliyopo Wilayani Wanging'ombe.
Mwanafunzi huyo aliamua kuacha shule baada ya ndugu yake mmoja kufika Kwa wazazi wake na kumuomba ili akawe msaidizi wa dukani na wazazi walikubali, hiyo ni baada ya kuahidiwa kuwa watakuwa wakitumiwa pesa kila mwezi, kwa kifupi walimgeuza mradi mtoto wao.
Mtoto huyo yeye aliahidiwa kufunguliwa biashara pindi atakapokuwa kuwa ametumika dukani hapo kwa muda wa miaka mitano.
Sisi Watanzania tunatakiwa kuwa kitu kimoja kupambana na ajira za utotoni maana watoto wengi wanakatisha masomo kwa kukimbilia kuajiliwa.
Shemeji zangu Wakinga na jamii yote kwa jumla tuachane na tabia ya kuajiri watoto wadogo badala yake tuwasaidie kutimiza ndoto zao Kwa kuwalipia ada na siyo kuwapa ajira.