Baadhi ya wadada huwa mnawapoteza watu wa kuwasaidia sababu ya njaa zenu

Choosen85

JF-Expert Member
Jun 22, 2022
931
2,186
Wakuu people's
Yale majizi 👉 kidumu

Aisee nilikwenda duka moja kupata huduma nikamkuta mdada mmoja tukazungumza hapa na pale nikaomba namba basi tukaanza mawasiliano na nikamuweka wazi kwamba nimempenda na akanielewa.

Akaanza kunishirikisha mambo yake kwamba alikuwa na mume wametengana sababu mumewe hamataki tena na ameoa mke mwingine na alimtesa sana.

Hapo dukani kaajiliwa tu na anaishi kwa bosi wake nikaamuliza wanakulipa shs ngapi akasema elfu 40 nikamwambia si mbaya sn sababu anaishi kwa bosi wake.

Nikamshauri kama kweli anania ya kusonga mbele basi anatakiwa apange room yake mi tamsaidia kodi ya miezi mitatu na baadhi ya vitu kama godoro akasema sawa ngoja ajipange.

Nikapata wazo nyumbani kwangu kuna vitu kibao vya kufanyia biashara kama ya chips au mama ntilie nk nikawaza atakapokuwa tayari kupanga room nimfungulie biashara mojawapo ili aachane na hiyo kazi ya kulipwa elfu 40 kwa mwezi hili skumgusia ili nilimwambia kama anaweza kufanya biashara akasema anaweza kabisa.

Sasa kilichonileta hapa ni kwamba siku moja usiku tukiwa tuna-chat akasema ooh hana amani nikamuuliza kwanini akajibu ooh mama yake amekabwa na watu wasiojulikana na wamenyang'anya kila kitu pamoja na pesa ya kikundi na anatakiwa alipe pesa za watu 😀 na yeye ndo wa kumsaidia kuilipa mi nikawapa pole kisha nikamwambia utawezaje kulipa hiyo hela kwa mshahara huo sasa akasema hata hajui afanyaje mi nikamwambia bnafsi siwezi kumsaidia hilo ukizngatia ndo kwanza tumeanza mahusiano kisha nikalipotezea hilo.

Zikapita kama siku 2 tukawa tunawasiliana vzuri tu sasa juzi namsalimia ananambia ooh leo hata sijui takula nn nikamuuliza kwann akajibu ooh hela ya mboga ameisahau nyumbani na hapo hana hela ya mboga 😀 mkumbuke alinambia anaishi kwa bosi wake. Mi nikamuliza ww ulisema unaishi kwa bosi wako sa mambo ya mboga na wewe wapi na wapi wakati wewe mambo hayo hayakuhusu unaishi kwenye mji wa watu.

Akasema kwani kakosea kuniambia nikamjibu hapana ila mi ninashangaa unaishi kwa bosi halafu wewe ndo unatakiwa utoe hela ya mboga 🤣. Hilo nikalipotezea akili ikakaa sawa kwamba huyu mdada hamna kitu anataka kunivuna tu hakuna jipya hapo nikamblock na nikaachana naye.

Sasa enyi wadada wakati mwingine mpunguze njaa na vibomu visivyo na kichwa wala miguu aisee mnapoteza watu wa muhimu sana kwenu wa kuwatoa hatua 1 kwenda nyingine ila njaa zenu zinawaponza sana. Huyu nilikuwa na nia ya kumsaidia kabisa ila kwa upuuzi huo wa kujaribu kunipiga vibomu nani anaweza wanaweza mambwiga tu.

NB: wale wanaoona eti namind vihela vidogo kama hivyo ni wao na akili zao tu mimi hata shs 50 ina thamani kubwa maana kwenye bil 1 ukitoapo shs 50 tayari siyo bil 1 tena.

Je, wakuu maamuzi yangu ni sahihi au si sahihi.🤔
 
Ndiyo maisha yalivyo wewe unaweza kujiona wa muhimu kwa mtu kwa kumfanyia mema ila yeye akawa haoni umuhimu wako na haitaji uwepo kwenye maisha yake, so atatengeneza drama za kitoto paka ukimbie.

Wewe uliamini analipwa elf 40? angekubali kufanya hiyo kazi?
Aisee hujui kuna watu wanalipwa elfu 30 tu kwa mwezi ww unashangaa elfu 40 shukuru Mungu una pa kuamkia asubuhi na unapata pesa nyingi mpk unashangaa mtu kulipwa elfu 40 kwa mwezi. Wapo wanaotafuta hata elfu 20 kwa mwezi hawapati. Jitoe akili tu.
 
Ulikutana na kausha damu pro, huyo ni aina ya wanawake ambao wanaamini kupewa/kupokea/kutatuliwa matatizo yao(yakiwemo ya kipuuzi) ni jukumu la lazima la wewe mwanaume as long as umeonesha nia ya kuwa nae kwenye mahusiano. Halafu mbaya zaidi hata shukrani hawanaga, siku ukiacha tu kutimiza hayo utakutana na maneno ya shombo.... na wakati wewe unafanya hayo yote unakuta kuna kijana wa ovyo hapo mtaani kwao anambinua anavyotaka bila kumsaidia chochote.
 
Aisee hujui kuna watu wanalipwa elfu 30 tu kwa mwezi ww unashangaa elfu 40 shukuru Mungu una pa kuamkia asubuhi na unapata pesa nyingi mpk unashangaa mtu kulipwa elfu 40 kwa mwezi.
Wapo wanaotafuta hata elfu 20 kwa mwezi hawapati. Jitoe akili tu
Sasa nimejitoa akili kwanini?
Hilo ni swali niliuliza kama unaamini analipwa 40k wewe unaleta mambo ya kushukuru nina pa kuamkia.
Mtu anakudanganya mambo ya kitoto sana ndo maana ninakuuliza umeamini analipwa 40k kwa mwezi?
 
Wanawake wengi hata kuangukia kwa wanaume wasio mpango wa Mungu sababu ni tamaa. Unakuta msichana anakutana na kijana smart kabisa kichwani ila ana maisha ya kawaida kabisa hapo ataona km huyo siyo mtu sahihi. Akikutana na mhuni kavalia suruali chini ya matako na madred kichwani na mapetepete mkononi ndiyo anaona kapata.

Wakishaolewa utaskia "ninanyanyiska", mara oh mwanaume Malaya, hanijali na blablaa kibao. Ukiangalia shida ni tamaa na kujifanya wa mjini kupenda muonekano wa nje akasahau kuna akili inayouendesha huo mwili (sura na six pack).
 
Umeamua sawa kabisa. Huyo ameendekeza njaa na hana nia njema. Anajijali peke yake. Huyo hana tofauti na demu mmoja, nilimwambia nimtoe lunch tu akanambia nimnunulie kwanza gauni jipya la kutoka nalo siku hiyo. Hovyo kabisa! Nilimblock kutokea hapo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom