Tlaatlaah
JF-Expert Member
- May 18, 2023
- 19,947
- 21,963
Msigwa hakuwa mwanachama wa kawaida Chadema, alikuwa kiongozi mwandamizi mwenye dhamana ya kusimamia makamanda na wanachama wa Chadema kanda ya Nyasa, na alikuwa pia mjumbe wa kamati kuu Chadema Taifa.
Anajua na kufahamu mambo na vitu vingi sana ndani ya chadema. Anajua vema nia, uwezo, malengo na matarajio binafsi ya mwenyekiti na makamu wa Chadema Taifa kwa siku zijazo, kwa chama hicho.
Kuondoka kwake hapawezi kukuosa wala kuacha madhara, makovu au athari za kisiasa. Hakuondoka chadema kwasababu tu ya kushindwa uchaguzi wa kiti cha uongozi wa kanda, alichokua akikitetea. kuna mambo mazito yamechochea msigwa kuondoka chadema, siyo tu aliyoyataja wakati akijiunga CCM.
Upo mshindo na mgandamizo mkubwa sana ndani ya Chadema unakuja. Msigwa ni mtengeneza njia tu. kuondoka kwa msigwa kuna mtikisiko na impacts za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja chadema, ukubali au ukatae, politically speaking.
Believe me or not, Muchungaji Msigwa ana watu, hususani kanda ya nyasa ataondoka nao taratibu siku hadi siku, na kuinyong'onyeza au kuidhoofisha chadema kwa kiasi katika eneo hasa la nyasa.
Alidhalilishwa sana, alihujumiwa sana, alifedheheshwa sana, alidhulimiwa sana kwenye uchaguzi wa ndani kanda ya Nyasa. Haingekuwa rahisi kuvumilia manyanyaso yale yaliyochochewa na fedha za miongoni mwa waandamizi wa chama chake cha zamani.
Kuondoka kwa mchungaji msigwa kunaashiria na kuonyesha kwamba chadema haiko Salama. Kuna fukuto la chini kwa chini. Kuna vibrations katika moyo wa kila muandamizi. Hofu na hali ya taharuki na kutoaminiani imetanda chadema. kila moja yuko makini na anachosema, anachoskia na anachoambiwa na mwenzake.
Unadhani kwanini msigwa kavutiwa kujiunga na CCM na sio kwingineko?
Anaefuata ni nani baada ya Msigwa, mpaka kufikia 2025? Huyo anafuata atalekea chama gani cha siasa?🐒