Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 52,947
- 119,942
Wanabodi,
Angalizo la Bandiko Hili, sijataja jina la mtu yoyote, naomba na wewe usitaje. Hapa nazungumzia title ya mtu kuitwa Mama.
Japo title ya "Mama" ni jina la heshima kwa mwanamke, kila mwanamke kuitwa mama ni heshima kubwa zaidi kwa mwanamke yoyote kuliko kuitwa tuu jina lake, hivyo Tanzania tulipobahatika kupata rais wa kwanza mwanamke, aliyepatikana kwa kudra tuu za Mwenyeenzi Mungu, tunamuita kwa utangulizi wa jina Mama.
Sasa kwa vile amekuwa daktari, kwanza nashauri tuupuuze huu ushauri wa Prof. Kironde alioutoa hapa,
View attachment 2437193 mpaka baada ya Kuongezeka Ph.D za Heshima: Kuna haja TCU watoe ufafanuzi wa matumizi ya title ya Dr. kwa Ph.D za heshima na Ph.D za ukweli? kwasabubu kwa Dr. Jakaya Kikwete ulipuuzwa, kwa Dr. Reginald Mengi ulipuuzwa, kwa nini na kwa Mama usipuuzwe?.
Nashauri kuanzia sasa huyu Mama officially, tuachane na utangulizi wa kumuita Mama, na badala yake, sasa officially aitwe Dr, ila ofisini kwake na nyumbani kwake, na kwa watu wake wa karibu, ndio aendelee kuitwa Mama?.
Lengo la kutoa pendekezo hili, ni kufuatia zile mada zangu za powers, majina yana impact kubwa kwa mhusika, hivyo kuna mambo ya metaphysical, na numerology yanayohusiana na majina na matamshi, kwenye words vibrations, kuna maneno fulani ukitamka, hayo maneno yanatoa powerful vibrations kama kwenye kitu kinachoitwa chanting kwenye dini, Hinduism na Budhism ndio wanatumia sana, ila hata Wakristu kwenye Rozari na Waislamu kwenye Tasbihi, wanatumia chanting.
Jina la Mama likitangulizwa, na kurudiwa rudiwa kunamfanya muhusika kufanya mambo ki mama mama, ki softi softi, kuwa na huruma iliyopitiza hivyo kuna maamuzi magumu atashindwa kabisa kuyatekeleza!. Mfano mtu akiisha itwa mama, ataweza kusaini death warrant?. Wakati wale "jamaa zetu" kuna maamuzi fulani hilazimika kuyachukua, na maamuzi hayo, "ukikosa tuu mara mbili, utatakiwa kuandika maelezo, kwanini umekosa".
Hao jamaa kwenye hizo operesheni maalum za kutokosa mara mbili, kabla hazijatekelezwa lazima mkuu aridhie kwa kuidhinisha kwa maandishi, naniliu zitumike!, sasa mtu akiitwa mama, ataweza kweli kusaini zile nanilii kama za Dodoma, kwenye makazi ya wale naniliu, zitumike?.
Maadam sasa huyu ni dakitari, mnaonaje sasa tukaachana kuitana mama kwenye mambo ya kazkaz halafu akaendelea kuitwa mama na watu wake wa karibu, ofisini na nyumbani kwake, lakini sisi tumuite Dr, ili hata ikibidi kumkoma nyani giladi, unamkoma tuu bila kumuangalia usoni!.
Mnalionaje hili wanabodi, jee tuendelee kumuita mama na yeye kutuita wanangu, hilo mkaliangalie, au sasa tumuite Dr, mambo ya huruma za ki mama mama aziache nyumbani na kwenye familia yake, hapa iwe kazi kazi tuu!.
NB. Hii sio mara yangu ya kwanza kuleta mada humu bila kutaja majina, hata mada hii Ikitokea kuna Kiongozi ana Macho mazuri, na umeyapenda, je, kuna ubaya kumsifia macho yake? Ni ukosefu wa heshima na adabu?
Jumapili Njema.
Paskali