Baada ya Kutuaminisha kuwa Hukumu ya Bernard Morrison ni leo, hatimaye mambo yawa Magumu kwa Yanga SC mpaka 14 Agosti, 2021

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
59,949
119,214
Ushauri wangu wa bure tu Kwenu huu muda mwingi ambao mnautumia kutaka Kuwaaminisha Mashabiki zenu kuwa mnashinda Kesi dhidi ya Mchezaji Bernard Morrison na leo imegonga mwamba tena kwa Hukumu yake kutolewa mngeutumia katika Kusaka Wachezaji wazuri wa Kukiimarisha Kikosi chenu Kibovu.

Ndani ya Mwezi Mzima mmekuwa mkihangaika Kuwaaminisha Mashabiki zenu kuwa Leo ndiyo Leo na nasikia mlijazana kama Mchwa Klabuni Kwenu Kufuatilia Mwenendo wa Kesi ambayo mliamini itakuwa upande Wenu Kimaamuzi mkasahau kuwa Wakili wa Kizungu aliyeko pale CAS ni Wakili Njaa na Mbabaishaji kama huyu Wenu Alex Mgongolwa na hatimaye Kesi imerushwa tena tarehe mpaka 14 August, 2021.

Nakumbuka Mtaalam wa Sheria za Soka hasa za CAF na baadhi za FIFA Mzee Ismail Aden Rage mwanzoni kabisa aliwaonya kuwa kwa Kesi yenu ilivyo huko CAS mnaenda kutoka patupu na Pesa yenu mliyotoa inapotea bure mkampuuza kwakuwa Yeye ni Mtu wa Simba SC.

Juzi juzi tu hapa katika Mkutano wenu Mkuu Kipenzi chenu wana Yanga SC na Rais Mstaafu Mzee Kikwete nae aliwaambieni kuwa achaneni na hiyo Kesi na msonge mbele na mambo ya Msingi hamkumuelewa pia na sasa taratibu mnaanza Kuumbuka na mtakuja Kuumbuka zaidi hiyo tarehe 14 Agosti, 2021.

Na mlivyo Majuha nasikia leo mkiamini kabisa Hukumu itakuwa upande wenu na mtashinda mlikuwa mmeshawaandaa Watangazaji na Wachambuzi wa Redio pamoja na Wahariri wa Habari za Michezo nchini ili wainange mno Simba SC Redioni na katika Magazeti yao ya Michezo sasa imekula Kwao ( Kwenu ) Kudadadeki.

Kwakuwa hamna Akili sasa nawaibieni Siri kuwa Kitendo cha Mahakama hiyo ya CAS Kuahirisha Hukumu leo ni kwamba wanataka Kujiridhisha kutoka TFF (ambayo Yanga SC mnaichukia mkisema ina Usimba mwingi) juu ya walivyoiamua Kesi na Kuiamua na kwakuwa TFF nao wameshawachokeni safari hii nao ( TFF ) wataambatanisha mpaka vile Vielelezo vyenu (Yanga SC) vya Kufoji (Kughushi) Saini ya Mchezaji Bernard Morrison na zile Fomu zenu Mbili ambazo zilisainiwa Kurasa za mbele tu na siyo zote kama ambavyo Sheria za Mkataba zinavyotaka duniani kote.

Kama ninawaona vile mlivyonuna sana.
 
Ushauri wangu wa bure tu Kwenu huu muda mwingi ambao mnautumia kutaka Kuwaaminisha Mashabiki zenu kuwa mnashinda Kesi dhidi ya Mchezaji Bernard Morrison na leo imegonga mwamba tena kwa Hukumu yake kutolewa mngeutumia katika Kusaka Wachezaji wazuri wa Kukiimarisha Kikosi chenu Kibovu.
Yanga ni taasisi, na sio mtu!

Na kama ni taasisi, kesi dhidi ya Morrison hawezi kukwamisha kusaka wachezaji wengine kwa sababu idara inayohusika na makesi ni tofauti na idara inayohusika na kusaka wachezaji wengine!!

On top of that, ni ule tu ubishi wa kuuza ng'ombe kwa kesi ya kuku kutaka kukomoana! What I mean, Yanga ishinde au isishinde, wala hawana mpango na huyo mchezaji!

Ingekuwa lengo ni kushinda ili imtumie huyo mchezaji,ndi[po labda tungesema "badala ya kuhangaika na Morrison, busara ni kutafuta replacement isije at the end Yanga inaangukia pua, na wakati huo muda wa usajiri umepita!"
 
Yanga ni taasisi, na sio mtu!

Na kama ni taasisi, kesi dhidi ya Morrison hawezi kukwamisha kusaka wachezaji wengine kwa sababu idara inayohusika na makesi ni tofauti na idara inayohusika na kusaka wachezaji wengine!...

Angalia unaibika kwa mambo ya kiswahili acheni morrison ale maisha yake.

Ushauri wa bure huu
 
Ushauri wangu wa bure tu Kwenu huu muda mwingi ambao mnautumia kutaka Kuwaaminisha Mashabiki zenu kuwa mnashinda Kesi dhidi ya Mchezaji Bernard Morrison na leo imegonga mwamba tena kwa Hukumu yake kutolewa mngeutumia katika Kusaka Wachezaji wazuri wa Kukiimarisha Kikosi chenu Kibovu.

Ndani ya Mwezi Mzima mmekuwa mkihangaika Kuwaaminisha Mashabiki zenu kuwa Leo ndiyo Leo na nasikia mlijazana kama Mchwa Klabuni Kwenu Kufuatilia Mwenendo wa Kesi ambayo mliamini itakuwa upande Wenu Kimaamuzi mkasahau kuwa Wakili wa Kizungu aliyeko pale CAS ni Wakili Njaa na Mbabaishaji kama huyu Wenu Alex Mgongolwa na hatimaye Kesi imerushwa tena tarehe mpaka 14 August, 2021.

Nakumbuka Mtaalam wa Sheria za Soka hasa za CAF na baadhi za FIFA Mzee Ismail Aden Rage mwanzoni kabisa aliwaonya kuwa kwa Kesi yenu ilivyo huko CAS mnaenda kutoka patupu na Pesa yenu mliyotoa inapotea bure mkampuuza kwakuwa Yeye ni Mtu wa Simba SC.

Juzi juzi tu hapa katika Mkutano wenu Mkuu Kipenzi chenu wana Yanga SC na Rais Mstaafu Mzee Kikwete nae aliwaambieni kuwa achaneni na hiyo Kesi na msonge mbele na mambo ya Msingi hamkumuelewa pia na sasa taratibu mnaanza Kuumbuka na mtakuja Kuumbuka zaidi hiyo tarehe 14 Agosti, 2021.

Na mlivyo Majuha nasikia leo mkiamini kabisa Hukumu itakuwa upande wenu na mtashinda mlikuwa mmeshawaandaa Watangazaji na Wachambuzi wa Redio pamoja na Wahariri wa Habari za Michezo nchini ili wainange mno Simba SC Redioni na katika Magazeti yao ya Michezo sasa imekula Kwao ( Kwenu ) Kudadadeki.

Kwakuwa hamna Akili sasa nawaibieni Siri kuwa Kitendo cha Mahakama hiyo ya CAS Kuahirisha Hukumu leo ni kwamba wanataka Kujiridhisha kutoka TFF ( ambayo Yanga SC mnaichukia mkisema ina Usimba mwingi ) juu ya walivyoiamua Kesi na Kuiamua na kwakuwa TFF nao wameshawachokeni safari hii nao ( TFF ) wataambatanisha mpaka vile Vielelezo vyenu ( Yanga SC ) vya Kufoji ( Kughushi ) Saini ya Mchezaji Bernard Morrison na zile Fomu zenu Mbili ambazo zilisainiwa Kurasa za mbele tu na siyo zote kama ambavyo Sheria za Mkataba zinavyotaka duniani kote.

Kama ninawaona vile mlivyonuna sana.
Mbona umepanic kuliko Morrison Mwenyewe siu utulize mshino mpaka hiyo 24, 8, 2021.
 
Mbona umeandika ki mahaba zaidi kuliko weredi..??

Hata uzoefu wa kesi za kwetu huku huna achilia mbali hizo za nje, kesi kusomwa au kusikilizwa ni jambo moja na kesi kutolewa hukumu ni jambo lingine.

Taarifa waliyotoa CAS ni kuwa shauri limesikilizwa na hukumu itatolewa tareh 14 August au kabla ya hapo.

Sasa katika hili lipi wewe limekutatiza!!
 
Angalia unaibika kwa mambo ya kiswahili acheni morrison ale maisha yake..
...ushauri wa bure huu
Duh!!! Hivi unajua ulichoandika!!

Naaibika kivipi? Niaibike kwani mimi ndie niliyefungua shauri dhidi ya Morrison?

Unanipa ushauri mimi kwani mimi ndie nimefungua shauri kwa ajili yaMorrison?

Au kuna mahali nilipoonesha kuunga mkono au kupinga suala la Morrison kufunguliwa shauri?!

Bila shaka utakuwa Shabiki wa Simba wewe...
 
Pole kwa ujinga wako. Suala la kusikiliza na kuhukumu ni la mahakama. Umeonyesha umbumbumbu wako maana hata Mzee Aden Rage aliwahi sema mashabiki wa Simba ni mbumbumbu. Wewe tuliza chupi kubwa kama ile ya Morrison usubiri hukumu. Useless.
 
Back
Top Bottom