nkongu ndasu
JF-Expert Member
- Jan 19, 2013
- 22,532
- 6,615
haa haa wakati upinzani wakimponda kitwanga mlisema rais asiwasikilize upinzani. leo kaondolewa sifa kedekede kwa JPM. duh hii kazi ya kusaka UDC noma....
Acha unafiki;mtu aliyejisifia kuwa alichukua muda mrefu kufanya vetting kabla hajateua leo inaonekana aliteua mlevi unataka kumsifia?
Halafu Mapungufu ya Mwigulu ni nini hasa maana haya majungu na unafiki unaotaka kuleta hapa hayalisaidii taifa
Huo ni mtizamo wako, ukiambiwa thibitisha unaweza?Lizaboni,hakika hilo halina ubishi. Rais Magufuli hana urafiki kwenye kazi.
bado Upo gheto Kwa Lugumi ? Nasikia kitwanga anakuja kukudai pesa zake alizokupa umtetee Mtandaoni , Ushikaji bado upo Kwa Magufuli mpaka awatumbue akina Mwakyembe wa mabehewa chakavu , Dau wa NSSF na Dili la daraja na viwanja Kigamboni , NIDA na wale ambao mmeanza kupiga magendo ya sukari kupitia mgongoni kwake kimya kimya .Wadau, amani iwe kwenu.
Kuna madai kwamba Rais John Pombe Magufuli ni rafiki wa karibu na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ambaye ameng'olewa kutokana na kosa la kuingia Bungeni akiwa amelewa, Charles Kitwanga. Tena baadhi ya wabunge wa Upinzani wakiongozwa na Godbless Lema walisikika wakisema kuwa Rais Magufuli hawezi kumchukulia hatua Waziri huyo kwa kitendo chake cha kufanya biashara na Wizara anayoiongoza, kwa vile tu ni "MSHKAJI" wake.
Kabla hata mate yao hayajakauka, Rais Magufuli kafanya maamuzi ya kumng'oa Waziri huyo tena kwa kashfa kubwa ya kuingia Bungeni akiwa amelewa. Rais Magufuli angeamua kumuondoa tu kwenye baraza la mawaziri Charles Kitwanga bila ya kutoa sababu ama angeweza kufanya mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri kwa kumuondoa Kitwanga na wengine ambao wameonekana wana Mapungufu kama Januari Makamba na Mwigulu Nchemba. Hata hivyo, Rais Magufuli hakutaka kuwa mnafiki. Akaamua kuchukua hatua kwa wakati.
Ninaamini kuwa hata wale wanaojiita watetezi wa haki za binadamu ambao wanapinga utumbuaji majipu hawatadiriki kupanua vinywa vyao kupinga uamuzi wa Rais. Ninaamini pia hata viongozi wa upinzani wakiongozwa na Freeman Mbowe na Tundu Lissu ambao siku zote wamekuwa wakidai kuwa Rais Magufuli hafuati katiba na Sheria wakati wa kutumbua Majipu kwa kutotoa nafasi kwa watumbuliwa kujieleza hawatadiriki kusema chochote.
Rais Magufuli yupo sahihi siku zote na kwa hili la Kitwanga hakika amedhihirisha kuwa Serikali yake haina mambo ya Kishkaji.
Wana mapungufu gani mkuu Lizaboni?wengine ambao wameonekana wana Mapungufu kama Januari Makamba na Mwigulu Nchemba. Hata hivyo, Rais Magufuli hakutaka kuwa mnafiki. Akaamua kuchukua hatua kwa wakati.
Lizaboni ni Fisadi wa pesa za utetezi wa Majipu sasa yupo gheto Kwa Lugumi kajificha anaogopa kudaiwa na Kitwanga alikula pesa zake nyingi akimdanganya watamtetea .haa haa wakati upinzani wakimponda kitwanga mlisema rais asiwasikilize upinzani. leo kaondolewa sifa kedekede kwa JPM. duh hii kazi ya kusaka UDC noma....
Lizaboni kampigia simu Mwakyembe ampatie gheto ahamie kwake Kwa ajili ya kumtetea asitumbuliwe juu ya mabehewa chakavu anadai Kwa gheto Kwa Lugumi si salama kwake kwani mda wowote kitwanga atatimba huko kumdai pesa zake alizompa Kwa ajili ya propaganda Mitandaoni .Wana mapungufu gani mkuu Lizaboni?
Haaa haaaa nimekuelewa mkuuLizaboni kampigia simu Mwakyembe ampatie gheto ahamie kwake Kwa ajili ya kumtetea asitumbuliwe juu ya mabehewa chakavu anadai Kwa gheto Kwa Lugumi si salama kwake kwani mda wowote kitwanga atatimba huko kumdai pesa zake alizompa Kwa ajili ya propaganda Mitandaoni .
Lizaboni lipo Uvunguni Kwa Lugumi limejificha baada ya kusikia kitwanga anaenda huko nyumbani Kwa LugumiHebu usinichoshe bhana huna jipya.unajitetea nini sasa?
Kama wezi wa Chenji ya Rada, Bunge la katiba , escrow , NIDA , NSSF walivyokuwa wasafi ccm .Kitwanga akihamia ukawa tu anakua msafi hapo hapo
Acha picha liendelee
Akithubutu kuwang'oa January Makamba na Mwakyembe ndipo Watanzania wengi wataamini Kauli mbiu ya kutumbua Majipu , kinyume na hapo ccm ni ile ile .Kuna maswali na aina fulani ya kebehi kutoka kwenye kivuli cha CCM (upinzani) kuhusu utendaji wa Rais, km
1) Rais afuati sheria!
2) Rais anakurupuka katika maamuzi yake!
3) Rais haongozwi na mfumo!
Kutengua uteuzi wake wa Waziri Kitwanga, pamoja na kuchukua muda mrefu kupata Baraza la Mawaziri ni ushahidi mmojawapo wa hayo.
Mimi ninavyomwelewa Rais Magufuli ni jinsi anavyotekeleza kaulimbiu yake "hapa kazitu" kwa vitendo. Anapiga vita siyo tu uzembe na ubadhirifu wa watumishi wa Serikali yake, rushwa na ufisadi katika jamii, ila kubwa zaidi ni vita dhidi ya KUFANYA KAZI KWA MAZOEA.
Kufanya kazi kwa mazoea kuna tafsiri nyingi, mojawapo na mbaya zaidi ni kutanguliza urafiki, undugu, kuzoeana, nk katika maofisi na kazini.
Wenye macho hawaambiwi tazama wala wenye masikio...