Nehemia Kilave
JF-Expert Member
- Jan 9, 2022
- 1,433
- 3,206
View: https://youtube.com/shorts/WWmBwoKcRi4?si=MXTAzBwxQMUNtmyg
Kwanza kabisa Mungu atusamehe kwa yale yote mabaya tunayoyafanya . Lakini ifahamike mitume na manabii wanajaribu tu kumuelezea tu huyu Mungu mkuu ambae hakuna anaemjua wala kuwahi muona .
Kwa kifupi hata dini zetu za asili zilikuwa sawa tu , ni ujinga kuamini kabla ya waarabu au wazungu wazee wetu hawakuwa sahihi .
Pili binafsi niliamua kuchukua muda wangu kufuatilia sana jambo la uwepo au kutokuwepo kwa Mungu yaani muumbaji wa kila kitu .
Niligundua Mungu yupo na anaipenda hii Dunia tunayo na kwa kifupi SISI SOTE NI NDUGU TUNAPASWA KUPENDANA SANA .
Kuna sababu kuu mbili kwanini Mungu yupo :-
1. Dunia tunayo ishi imepewa uwezo wa tofauti wa kuwezesha sisi kuishi lakini pia ni Sayari ambayo imepewa Mwezi na Sayari ya Jupiter kuiilinda na majanga mbali mbali.
Kwa maana rahisi bila Gravity ya Mwezi na Jupiter dunia ingekuwa inashuhudia majanga kila siku na kuna uwezekano isingekuwepo .
View: https://youtube.com/shorts/mlwCOAQu9v0?si=cwgqFs5a9PTX-pVQ
2.Hakuna chanzo kinachoonesha na ambacho ni endelevu kuonesha namna gani binadamu alitengenezwa au anatengenezwa .
Kwa hizi sababu utagundua kuna kitu au Mtu aliyeweka na anacontrol hii Dunia hakuna namna binadamu kutokea tu na dunia kupewa ulinzi mkubwa namna hii .
Kama Mungu anavyoipenda Dunia basi naamini huko aliko anatamani na kupenda binadamu tufanye mema .
SISI NI WAMOJA hakuna aliyesahihi kuliko mwingine sababu Mungu yupo ila sote manabii ,mitume wa zamani na sasa wanajaribu kueleza Mungu yukoje na anataka nini .
Binafsi naamini Mungu yupo ila hizi dini na madhehebu ndiyo kila moja linajaribu kueleza namna gani Mungu alivyo na nini anataka . TUPENDANE hizi dini na madhehebu ni mapokeo kwa namna nilivyo fuatilia .
Muwe na Siku Njema . Special thanks to Isaac Newton kwa kusacrifice social life na kufanya mambo makubwa ambayo mpaka sasa kanuni zake tunazitumia kufanya mambo mbali mbali .
View: https://youtube.com/shorts/lkAyO2iCQxg?si=0RTf6d_gkmv4Hs-Q
View: https://youtube.com/shorts/NInhDab5lbg?si=9JyvmkIlhzCiPiNV