B-12-XXL ya Clouds FM kibarua chake matatani

BABA TUPAC

JF-Expert Member
Sep 30, 2015
1,527
3,810
Ukiona unafanya kazi kwa mhindi akaja muhindi mwenzake akasema umfundishe kazi ujue baada ya mwaka mmoja huyo mhindi ndio atakuwa boss wako.

Kuna dogo anaitwa Kennedy The Remedy huwa anatangaza XXL na B Twelve, B 12 ndio anayemfundisha kazi. Kiufupi ni kwamba huyu dogo ndio anaandaliwa ili kumuondoa B twelve kwenye XXL, ni lazima ufikiri ili uelewe hili ninalolizungumza. B Twelve kama atakaa sana pale XXL basi mwaka ujao ndio mwisho na Kennedy The Remedy atakuja kuwa mtangazaji hiyo show. Rejea kilichomkuta Dina Marios

Wapo watakaopinga lakini naomba thread hii ibaki kama reference.
 
aah wapi ana mahaba yake tu huyo, dozen level nyingine, ndo maana EA wakamleta dulla mchana maana sam hakuuweza ule mziki
 
Kennedy anafundshwa kazi kivipi wakati alikua mtangazaji EA Radio...pia Kennedy ni replacement ya Fetty....Kennedy kahama EA radio kama gadner alivyo hama clouds
 
Yani we mleta thread sijui unawaza nin, hv unajua xxl mpka inaisha saa kumi wanaskika watangazaji wangap? na anayecontrol mzigo wote ni nan? na hv unajua kuwa dozen kile kipindi ni chake na yeye ndo alitoa wazo la kumleta kennedy amreplace fetty?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…